Waziri Mkuu wa Uingereza awekwa njia panda na ISIS na rais Bashar al Assad.
Wakiongea kwa nyakati tofauti, viongozi hao walisema '' Ili kuweza kukabiliana na wimbi la kundi la ISIS, ipo haja ya kushirikiana na serikali ya Syria, ambayo inauweza kupambana na kundi hilo,kwani itakuwa nivugumu kwa serikali za magharibi kupambana na kundi hilo peke yao.''
Saga hiyo ambayo inamwandama waziri David Cameron, imekuja baada ya picha za mauaji ya mwandishi wa habari wa Marekani James Foley kusambazwa mitandaoni na kundi la ISIS na kudai kuwa wale wote wanao isaidiia Marekani wajiaandae na malipo kutoka kwa kundi hilo.
Kundi la ISIS ambalo hapo awali lilikuwa linapambana na serikali ya rais Assad, na kuungwa mkono na serikali za Magharibi, lilibadirisha mwelekeo wake nchi Irak, na kuwa mpinzani wa nchi za Magharibi, jambo ambalo limeleta tishio kwa nchi hizo.
Kutokana na uamuzi wa kundi la ISIS kugeuka kupingana na sera za nchi za Magharibi nchini Irak, limefanya Marekani na washiriki wake kuaanza kulishambulia kijeshi kundi hilo na kulifanya kundi hilo kutangaza vita na nchi za Magharibi.
Hadi kufikia sasa, kuna idadi ya raia 500 wa Uingereza ambao ni wapiganaji wa kundi la ISIS, ambao inahofiwa wakirudi nchi Uingereza wanaweza kuwa watu wahatari kiusalama wa nchi.
Urusi ya fanya kweli kwa mara nyingine.
Moscow, Urusi - 23/08/2014. Serikali ya Urusi, imetangaza kuwa imefanikiwa kupeleka misaada ya kiuutu nchini Ukraini na magari yaliyobeba misaada hiyo yamerudi salama.
Akiongea baada ya kurudi salama magari hayo, naibu waziri wa misaada na dharula wa Urusi Eduard Chizhikov amesema '' magari 227 aina ya maroli yamerudi salama, baada ya kushusha misaada nchi ya kiutu nchini Ukraini''
Akiongea kuthibitishwa kufika kwa misaada nchini Ukraine, mkuu msaidizi wa umoja wa matifa katika masuala ya haki za kibinadamu na dharula Valerie Amos, amesema ''nimeweza kuongea na wakazi wa Slavyanks ambao wamekimbia kutokana na vita,na kushuhudia misaada waliopata.''
''Kikubwa kinachotakiwa ni kwa jumuiya ya kimataifa na kuangalia upya hali ya utoaji wa misaada ya kiutu, kwani wote tunakubaliaana kuwa kunahaja ya kutoa misaada kwa watu walikumbwa na matatizo ya vita vinavyo endelea nchini Ukraine.'' Aliongezea bi Valerie Amos.
Hata hivyo kitendo cha magari hayo ya kutoka Urusi kuingia bila ruhusa ya serikali ya Ukraini kimelaumiwa na Marekani na washiriki wake, lakini serikali ya Urusi imesema haitatilia maanani lawama hizo kwani Urusi imefanya jambo la kiutu na ''hakuna kitakacho zuia Urusi kutoa misaada ya kiutuu inapohitajika Urusi kufanya hivyo''
Misaada hiyo ambayo ilipelekwa katika mji wa Lugansk, baada ya serikali ya Urussi kuamua kuingiza misaada hiyo ambayo ilikaa mpakani kwa muda wa wiki ambapo serikali ya Kiev ilikuwa inapinga kuingia kwa misaada hiyo nchi Ukraini, kwa madai inaweza ambatanishwa na siraha kwa ajili ya wapinzani serikali hiyo.
No comments:
Post a Comment