Tuesday, August 26, 2014

Baba ya gaidi asadikiwa kuwa mpiganaji wa Al-Qaeda.

Nguvu zatumika kwa Rais Salva Kiir na Riek  Machar ili kuleta amani 

Juba, Sudani ya Kusini - 26/08/2014. Rais wa Sudani ya Kusini na kiongozi wa kundi linalo pingana na serikali yake wamesaini  mkataba wa kusimamisha vita vya wao kwa wao na kupewa siku 45 kuunda serikali ya muungano.

Rais Salva Kiir na Riek Machar, walikubali kusaiani makubaliano ya kusimamisha mapigano, baada ya jumuiya ya shirikisho la maeneo ya Afrika Mashariki - IGAD na jumuiya ya kimataifa kutishia kuweka vikwazo kwa yoyote atakaye pinga kusimamisha mapigano.

Akiongea mara baada ya kusainiwa makubaliano ya kusimamisha vita kati ya serikali ya rais Kiir na kundi linalo muunga mkono  Riek Machar, waziri mkuu wa Ethiopia Hailemaria Desalegn alisema ''tumetoa ujumbe kamili kwa viongozi wa Sudani ya Kusini yakuwa kitendo chochote cha kuchelewesha  kutimiza makubaliano ya amani hakitakubaliwa na ikitokea hivyo basi hatua zitachukuliwa.''

Tangu kuanza kwa vita kati ya serikali ya rais Salva Kiir na kundi linalo muunga mkono Riek Machar, maelfu ya watu  wameuwawa na zaidi ya milioni mbili kukimbia makazi yao na kati ya hao 100,000 walikimbilia katika maeneo ya ofisi za umoja wa mataifa zilizopo nchini Sudani ya Kusini na kufanya ndiyo makazi yao.

Mgogoro wa uongozi ulikuwa ndiyo chanzo cha  vita nchini Sudani ya Kusini, baada ya rais Salva Kiir kumfukuza kazi Riek Machar, ambaye alikuwa makamu wake wa urais

Baba ya gaidi asadikiwa kuwa mpiganaji wa Al-Qaeda.

New York,, Marekani - 26/08/2014. Baba mzazi wa mtuhumiwa ambaye aliye mchinja mwandishi wa habari, yupo jela nchini Marekani akisubiri hukumu ya kuhusika katika mauaji, kupanga mauaji na kulipua mabomu.

Adel Abdel Bari 54, ambaye anashitakiwa kwa kuhusika katika milipuko ya mabomu yaliyo tokea nchini Kenya na Tanzania 1998, ambapo ofisi za balozi zilizopo nchini humo zililipuliwa kwa mabomu na kusababisha maafa makubwa  na mauaji ya kutisha.

Habari  za kikachero zimethibitisha  kuwa '' Bari ni baba  wa mpinajii wa kundi la ISIS Abdel Majid Abdel Bari au kwa jina la John, ambaye inasadikiwa ndiye aliye fanya kitendo cha kinyama, kwa kumchinja mwandishi habari James Foley ambaye alikuwa raia wa Marekani''

 '' Bari alikuwa akiongoza katika kuunganisha mawasiliano ya  wapiganaji wa kundi la Al-Qaeda walio  kuwepo nchini Kenya na makao makuu ya Al-Qaeda''

'' Na vile vile inaminika alikuwa mmoja wa kiongozi na mwanajeshi a mwenye  cheo cha juu, na alikuwa karibu saana na Osama bin Laden.''Ziliongeazea habari hizo za kikachero.

Adel A Bari, ambaye hapo mwanzo alishikiliwa na polisi nchini Uingereza kwa muda miaka 14, kwa kushukiwa kuhusika na makosa ya kigaidi, aliachiwa huru baada ya kukosekana ushahidi, lakini baadaye alikamatwa na kupelekwa Marekani kwa kutakiwa kujibu mashitaka kama hayo.

Syria ipo tayari kushirikaiana na Marekani.

Damascus, Syria - 26/08/2014. Serikali ya Syria imesema ipo tayari kushirikiana na Marekani katika kupambana na kundi la kigaidi la ISIS.

Akiongea kuhusu ni nini kifanyike ili kukabiliana na kundi la ISIS, waziri wa mambo ya nchin wa Syria Walid Moallem amesema '' juhudi zozote za kukabiliana na kundi la ISIS zinakaribishwa, na tupo tayari kushirikiana na Marekani kwa kupitia mwamvuli wa umoja wa mataifa wa kupambana na ugaidi duniani.''

Maeleozo ya waziri Moallem, hayakujibiwa na serikali ya Marekani, kwani Marekani ni moja ya nchi inayo pinga kuwepo kwa utawala wa rais Bashar al Assad, ambaye serikali yake imekuwa ikipambana na magaidi wa kundi la ISIS, ambo wamekuwa wakipata misaada kutoka serikali za Magharibi ili kuing'oa madarakani serikali ya rais Bashar al Assad.







No comments: