Christiano Ronaldo, achaguliwa kuwa mchezaji bora wa FIFA msimu wa 2008-229, ndoto yangu imekamilika"Waulizeni wale wanao nijua"

Christiano Ronaldo alishinda kwa kupata kura 446, kwa kuwashinda kwa kura nyingi, Lionel alipata kura 281 Messi na Fernando Torres kura 179.
Ronaldo, alitoa mchango mkubwa katika timu yake ya Man United, kuweza kufunga magoli 42, na kuiwezesha timu hiyo kuwa mabingwa wa ligi ya Uingereza kwa msimu wa 2008-2009.
Vilevile , Christiano Ronaldo,alifunga goli la pekee, lililo iwezesha timu yake Man United kutwaa ubingwa wa vilabu bingwa vya Ulaya msimu wa 2008-2008, katika fainali liyo fanyika jiji Moskow.
Picha hapo juu anaonekana , Christiano Ronaldo, akiwa ameshikia, kombe la vilabu bingwa vya Ulaya,baada ya timu yake kulitwa taji hilo jijini Moskow.
Picha ya pili anaonekana, Christiano Roanaldo, akishangilia baada ya ya kunga goli alilo funga wakati timu ya taifa ya Ureno ilipo kuwa katika moja ya mashindano ya kuwania fainali kombe la Ulaya.
Rais mtarajiwa Baraka Obama, amchagua, bi Hillary Clinton, kuwa waziri wa mambo ya nje.



Bi,Hillary Clinton, ambaye alikuwa mpinzani wake, wakati wa kumchagua mgombea pekee atakaye gombania kiti cha uraisi nchini Amerika.
Rasi mtarajiwa Baraka Obama, alisema ya kuwa , Hillary Clinton ni mwaminifu na mfanyaji kazi bora na anafaa kuwa katika serikali itakayo leta mabadiliko nchini Amerika na kimataifa.
Picha ya hapo juu anaonekana, rais matarajiwa , Baraka Obama, akitangaza baraza la mawaziri. kulia ni bi ,Hillary Clinton na kushoto ni makamu wa rais Joe Biden
Picha ya pili hapo juu anaonekana , bi Hillary Clinton, akinyoosha kidole gumba , kuashiria ya kuwa sasa Amerika mambo yake yatakuwa safi.
Picha ya tatu, wanaonekana, rais mtarajiwa Baraka Obama na bi Hillary Clinton wakiwa pamoja wakati wa moja ya kampeni za kumchagua Baraka Obama kuwa rais wa Amerika.
Nasikitika na kutokuwepo na umakini wa uchunguzi, hata hivyo ninamaliza muda wangu nikiwa kichwa juu."Asema rais George Bush"

Rais George Bush alisisitiza kwa kusema anasikitika ya kuwa hali ya uchumi duniani imekuwa mbaya wakati wa uongozi wake.
Kutofanyika kwa umakini katika uchunguzi ya kuwa Irak ilikuwa ina tengeneza siraha za nuklia, ni hali ambayo ina nisikitisha saana,lakini kitendo cha kumn'goa madarakani Saddam Hussein kilikuwa cha halali, alisisitiza tena rais George Bush.
Rais, George Bush, ambaye atakabizi madaraka kwa rais mchguliwa, Baraka Obama, Januari 20, alisema ya kuwa anamatumaini , historia itakapo andikwa, basi atakumbukwa ya kuwa alikuwa rais, asiye nunuliwa na siasa na alifanya maamuzi magumu inapo bidi ili kuilinda nchi yake aliyo ipenda na kuiongoza,na nina maliza muda wangu nikiwa nimenyanyua kichwa changu juu.
Picha hapo juu anaonekana rais , George Bush, akiwa anatafakari hali halisi ya uongozi wake.
Matendo ya ugaidi nchini India ya leta mvutano kwa maasimu wawili.



Magaidi hao walilipua kwa mabomu na kuwapiga risasi watu wasio na hatia na kusababisha mauaji ya kitika Sinagogi la Wayaudi ,Hotel ya Taj Mahal na maeneo mengine tofauti.
Ugaidi huo umeleta mvutano mkubwa kati ya Pakistani na India ambao ni maasimu wawili wa muda mrefu.
Kwa mujibu wa serikali ya India, mipango yote ya kigaidi ilifanykia nchini Pakistan na kundi lianalo julikana Deccan Mujahedeen ambalo inaemekana lina uusiano na magaidi hao.
Hata hivyo serikali ya Pakistan, imekanusha madai hayo, na kutaka ionyeshwe ushaidi kuhusu madai hayo.
Picha hapo juu anaonekana mmja ya makomando wa jeshi la India,akilenga kwa makini katika eneo ambapo milio ya risasi inatokea.
Picha ya pili, anaonekana mmoja , ya makomando akikimbilia katika eneo lake tayari kuanza kazi yake.
Picha tatu, moto na moshi mweusi unaonekana ukitokea katika moja ya jengo la Taj Mahal Hotel, baaday ya kulipuliwa na magaidi.
Japan kuondoa majeshi yake ifikapo mwisho wa mwaka.

Tokyo,Japan- 28/11/08. Serikali ya Japan, imesema yakuwa ita maliza mkataba wake wa kijeshi nchini Irak ifikapo mwisho wa mwaka.
Akiongea hayo, waziri wa mkuu wa Japan, Taro Aso, amesema yakuwa, kamati ya ulinzi ya Japan, imeona mafanikio yaliyo fanywa na Wairak kiulinzi na kukuza demokrasi nchini humo.
Jeshi la Japan, lilikuwa na kazi ya kulisaidia jeshi la washiriki waliongozwa na jeshi la Amerika katika maswala ya anga na ulinzi kwa ujumla.
Picha hapo juu ni ya waziri mkuu wa Japana, Taro Aso, akiongea mbele ya baadhi ya viongozi wa nchi.
No comments:
Post a Comment