Monday, December 8, 2008

Wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi na usalama ya Blackwater, kizimbani kujibu kesi ya mauaji.

O.J.Simpson,akutwa na hatia na kufungwa miaka 15 jela.

LasVegas,Amerika,05/12/08.O.J Simpson, aliyejuwa mchezaji maarufu wa mipira wa watu wenye misuri-American Football, amehukumikwenda jela miaka 15, baada ya kukutwa na hatia ya kuvunja sheria na kuhatarisha maisha ya jamii.
O.J. Simpson, alikutwa na hatia,baada yeye na rafiki yake kuamua kwenda kuchukua vitu walivyo dai ni vya O.J . Simpson katika duka moja lilipo mjini humo.
Hukumu ya O.J. Simpson na mwenzake, ilitolewa na jaji Jackie Glass.
Hata hivyo wanasheria wa O.J.Simpson, walidai watakata rufaa, kwani kuna baadhi ya vifungu vya sheria vilikiukwa wakati wakuendesha kesi hii.
Picha hapo juu anaonekana, jaji, Jackie Glass, akiongea kabla ya kutoa hukumu ya kifungo kwa O.J.Simpson cha miaka 15 jela.
Picha yapili, Inatimiza ule usemi useamao,msiba kwa jilani kuna shibe ya muda,hapo anaonekan mmoja ya wachuuzi wa biashara ndogo ndogo, akiuza vichika funguo vikiwa na picha za O.J.Simpson.
Picha ya tatu anaonekana, O.J. Simpson, akiongea mbela ya jiji, kwa kudai yakuwa alikuwa anachukua malizake, na hakujua kama alikuwa nanafanya makosa ama kuvunja sheria.
Wafanyakazi wa kampuni yaulinzi na usalama ya Blackwater, kizimbani kujibu mashitaka ya mauaji.
Utah,Amerika,08/12/08.Wafanyakazi watano wa kampuni ya ulinzi na usalma ya Blackwater, wamejisalimisha wenyewe kwenye vyombo vya usalama mjini Utah, ili kujibu mashitaka ya zidi yao zidi ya mauaji ya rais nchini Irak, wakati wakiwa kazini.
Kwa mujibu wa mwanasheria wa wafanyakazi hawa,alisema ya kuwa wateja wake walikuwa kazini wakati wa mashambulizi hayo yalipo tokeana walikuwa wanajilinda na mashambulizi, baada ya kushamuliwa na watu wasio julikana.
Picha hapo juu wanaonekana,wafanyakazi wa kampuni ya usalama na usalama, ambao wanakabiliwa na mashitaka ya mauaji.
Picha pili ni ya gari, ambayo ilikuwa moja wapo lililo kutwa kati ya mashambulizi ya wafanyakazi wa Blackwter.
Poland yawa na wasiwasi kufuatia mkataba wa usalama wa kulinda NATO.
Slupsk, Poland,04/12/08.Wachunguzi wa mambo ya kiusalama nchini Poland, wamesema yakuwa kupitishwa kwa makubaliano kati ya serikali ya Poland na serikali ya Amerika, ili kuwekwa mitambo ya kivita nchini humo kumeleta wasiwasi na hisia tofauti.
Akisema haya, ni mmoja ya wanajeshi wa Poland, Bronislaw Nawak, alisema yakuwa ,ikiwa makubaliano haya yata endelea kama yalivyo kubaliwa, basi Poland itakuwa ndiyo chambo cha mashambulizi yoyote yatakayo tokea kwa kuzingatia na maelezo yaliyo tolewa na uongozi wa mjini Moscow,alimaliza kwa kusema Bronislaw Nawak.
Hata hivyo, jumuia ya Ulaya, imekubaliana kwa pamoja kuwekwa kwa mitambo hiyo ya kivita nchini Paland.
Picha hapo juu ni picha ya mizimga ya kivita ambayo huenda zikaweka nchini Poland,ambapo serikali ya Washington inadai ya kuwa mizinga hiyo ni kwa ajili ya kulinda NATO na mashambulizi kutoka Iran na Korea ya Kusini.
Serikali ya Afghanistan, yataka muda maarumu wa kuwepo kwa jeshi la kimataifa.
Kabul,Afganistan - 29/11/08. Rais wa Afghanistan,Hamid Karzai,amesema ya kuwa itakuwa ni muafaka endapo majeshi ya kimataifa yatewaka muda maarumu wa kuwepo nchini humo.
Akiongea mbele ya ujumbe wa kamati ya usalama wa umoja wa mataifa, ya kuwa endapo kutakuwepo na muda maarumu utakao wekwa kwa majeshi haya kuondoka ili kuweza kupanga ni jinsi gani kutakuwepo na makubaliano ya kisiasa kati ya makundi yanayo pingana na serikali.
Nchini Afghanistan, kundi la Taliban, ndilo kundi kubwa linalo ongoza mashambulizi zidi ya serikali na majeshi ya kimataifa.
Picha hapo juu, anaonekana rais, Hamid Karzai, akiongea mbele ya wajumbe wa kamati ya usalama ya umoja wa mataifa.
Picha ya chini, ni mmoja ya mwanajeshi wa jeshi la kimataifa, akiwa anakura doria katika moja ya mji nchini Afghanistan.

No comments: