Wakaribbean waomba rais mteule wa Amerika, Baraka Obama, kuondoa vikwazo kwa serikali ya Kuba.
Saint John's,Barbuda - 09/12/08.Jumua ya nchi za Karibbien, zimemwomba rais mchaguliwa wa Amerika, Baraka Obama, kuondoa vikwazo vilivyo wekwa kwa serikali ya Kuba.
Akiongea hayo, waziri mkuu wa Antigua na Barbuda, W Baldwin Spencer,ambaye ni mwenyekiti wa jumuia ya nchi za Karibbien, amesema hayo wakati wa mkutana wa viongozi wa nchi hizo ulio fanyika Santiago de Kuba.
Hata hivyo , rais mteule wa Amerika, Baraka Obama, alisema yakuwa serikali yake itapunguza baadhi ya vikwazo kwa wananchi wa Kuba,lakini vikwazo vitabakia mpaka hapo serikali ya Kuba itakapo badilisha msingi wake wa kisiasa.
Picha hapo juu, anaonekana rais mtuele wa Amerika, Baraka Obama, akisikiliza kwa makini wakati alipo udhulia moja ya mikutano ya kampeni ya kugombania urais wa Amerika,na aliahaidi mabadiliko makubwa katika serikali yake ikiwa atachaguliwa kuwa rais wa Amerika na kukuza ushirikiano na jumuia ya kimataifa ili kurudisha hazi ya Amerika na wanachi wake.
Mamia ya waumini wa dini ya Kiislaam, wamaliza kutimiza moja ya nguzo za dini.
Mecca,Saudi Arabia - 09/12/08.Maelfu ya waumini wa dini Kiislaamu,wametiza wajibu na nguzo za dini ya Kiislaamu, baada ya kukamilisha hija kwa kufuata njia zote alizo fanya Mtume Muhammad ( S . A . W).
Kwenda Hija, ni muhimu kwa kila Muislaamu, endapo atajaliwa kufanya Hija wakati uzima wake, alisema, mmoja ya Mahujaji.
Picha hapo, juu wanaonekana baadhi ya waumuni wa dini ya Kiislaamu wakiwa wamepumzika karibu na mlima Arafat.
Picha ya pili wanaoneka, baba na mtoto wake wa wakitupa mawe, ikiwa ni ishara ya kumpiga shetani na mambo yake yote.
Picha ya tatu,wanaonekana mamia ya waumini, wakizunguka mnara wa Kabba, ambao nu moja ya jiwe ambalo limebakiwa ambalo lilijengwa na Mtume Abraham( Ibrahim), na nimuhimu kwa kila Muislaamu akijaliwa kulitenda na kutimiza katika uzima wake.
Pakistan yaweka ngumu kuwapeleka raia wake nchini India.
Islamabad,Pakistan - 08/12/08. Serikali ya Pakistan, imesema ya kuwa haita wapeleka washukiwa wa maafa ya ulipuaji wa mabomu na kusababisha mauaji ya watu 172 na zaidi ya 300, walijeruhiwa.
Brussels, Belgium - 2/12/08.Jumuia ya Ulaya, imekubaliana kwa pamoja kuwapokea na kuwapa hifazi wakimbizi, 10,000 kutoka nchini Irak, waliopo kwenya makambi ya kikimbizi nchini Syria na Jordan.
Brussels, Ubeligiji - 6/12/08. Mahakama ya haki za binadamu ya jumuia ya Ulaya - European Court of Human Rights (ECHR), imesema kufukuzwa kwa wanafunzi wa kike wawili waliokataa kufua vitambaa vya kichwa, halikuwa tendo la kukiuka haki za binadamu.
No comments:
Post a Comment