Mwanana mama mwenye umri wa miaka 70 ajifungua mtoto.
Jimbo la Haryana, India-15/12/08. Mwanamke mwenye miaka 70,(amjaliwa kupata mtoto), kujifungua mtoto wa kike, akiwa ni mwanamke wenye uri mkubwa katika historia ya India na dunia.
Mwanamke huyu, Rajo Devi, alijifungua kwa kufanyiwa upasuaji, alisema ,mganga aliye muhudumia, Dr Anurag Bishnoi, na amganga alimalizia kwa kusema, bi, Rajo Devi yupo katika hali nzuri.
Picha hapo juu, anaonekana mwamama, Rajo Devi na mume wake pamoja na mtoto wao wa kike baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini.
Ziara ya mwisho ya rais, George Bush nchini Irak ya kutwa na mkasa.



Mkasa huo,ulimkuta rais, George Bush,wakati alipo kuwa akiongea na waandishi wa habari, mjini Baghdad, na mmoja ya wandishi wa habari kumtupia viatu na kudai ya kuwa hakutimiza haadi aliyo itoa wakati akiwa madarakani na sasa anaondoka na kuiacha Irak katika hali ngumu.
Rais, George Bush, aliendelea na ziara yake kama kawida, na kueleka nchini Afghanistan.
Mwandishi wa habari huyo, ambaye julikana Muntazer al-Zaidi, amechukuliwa kama shujaa nchini Irak kwa kitendo chake hicho.
Hata hivyo, Muntazer al Zaidi, alikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi.
Kufuatia kukamatwa kwa Muntazer al-Zaidi, kumefanya wananchi wa maeneo tofauti nchini Irak,kuandamana kudai ya kuwa Muntazer aachiwe huru.
Picha hapo juu wanaonekana, baazi ya wananchi nchini Irak, wakiandamana kudai ya kuwa Muntazer al-Zaidi, aachiwe huru.
Picha ya pili, inaonyesha matukio ya aina tofauti,wakati rais, George Bush na waziri mkuu Nuri al-Maliki wakati walipo kuwa wakiongea na waandishi wa habari.
Picha ya tatu, anaonekana, Muntazer al-Zaidi akilusha kiatu kuelekea alipo simama rais , George Bush na waziri mkuu wa Irak Nuri al-Maliki.
Picha ya tatu, anaonekana waziri mkuu wa Irak,Nuri al- Maliki, akijaribu kuzuia kiatu bila mafanikio kisimfikie usoni rais George Bush,lakini hata hivyo kiatu hicho akikuweza kumzuru rais George Bush baada ya kukikwepa kiatu kilichotupwa na Muntazer al Zaidi.
Pakistan na Uingereza kushirikiana kupamabana na ugaidi"$ million 9 kutumika".



Waziri mkuu wa Uingereza, Gordo Brown, alitembelea pia, kiserikali za nchi za India,Afganistan na Pakistan.
Picha hapo juu wanaonekana,rais wa Pakistan, Asif Ali Zardari na waziri mkuu wa Uingereza, Gordon Brown, mapema walipo kutana mjini Islamabad.
Picha ya pili, wanaoneka madereva wa maroli yanayo chukua mizigo ya jumuia ya kijeshi ta NATO, wakiwa wamekaa chini, huku hawajui la kufanya, baada ya maroli yao kulipuliwa pamoja na baadhi ya magari ya kijeshi ya jumuia hiyo mapema hivi karibuni.
Picha ya tatu, wanaonekana waziri mkuu wa Uingereza, Gordon Brown, akiwa na waziri mkuu wa India, Monmohan Singh, wakati walipo kutana nchini India
Kongo na Rwanda zalaumiwa kwa machafuko ya liopo nchini Kongo.



Katika repoti, iliyo wasirishwa kwenye Umoja huo,imesema yakuwa, serikali ya Kongo, imekuwa ikishirikiana na kundi moja la Kihutu, (FDLR) Force for the Liberation of Rwanda lililo kimbilia nchini Kongo, baada ya serikali inayo ongozwa na rais, Paul Kagame kuchukua madaraka.
Na ripoti hiyo, ilisema yakuwa serikali ya , Rwanda imekuwa ikimsaidia, mpinzani mkuu wa serikali ya Kongo, Laurant Nkunda, ambaye anatetea masrahi ya watusi waishio nchini Kongo.
Ripoti hiyo ilisema ya kuwa Kongo na Rwanda zinapigana vita kwa kutumia makundi haya na kusababisham madhara makubwa kwa wananchi na jamii nzima, hasa katika maeneo yenye vita.
Uingereza kuanza kutoa wanajeshi wake mapema mwaka 2009.

Hata hivyo, serikali ya Uingereza ilisema yakuwa, watakuwepo wanajeshi kati ya 300 hadi 400 watakao kuwa na kazi ya kulifundisha jeshi la Irak.
Hapo ujuu wanaonekana, baazi ya wanajeshi wa Uingerereza, wakiwa kazini katika eneo moja nchini Irak.
Israel ya wachia Wapalestina"Ishara ya kumuunga mkono rais.



Kuachiwa kwa Wapalestina hao, kumekuja kama ishara ya kumuunga mkono rais wa Palestina, bwana, Mahmoud Abbas, ambaye anawakati mgumu kisiasa, hasa kwa kupata upinzani kutoka kwa chama cha Hamas.
Picha hapo juu wanaonekana wanachama wa Hamas,wakiandamana kwenye mji wa, Gaza kuazimisha miaka 21,tangu chama cha Hamas kilipo anzishwa.
Picha ya chini, wanaonekana Wapalestina, ambao wameachiwa wakikaribia kukutana na ndugu zao.
Picha ya tatu wanaonekana, wakina mama,wakishangilia kwa hali ya juu,wakati wafungwa wa Kipalestina walipowasili kwenye maeneo ya Wapalestina.
No comments:
Post a Comment