Thursday, December 18, 2008

Hali ni ngumu kwa Joseph Koni,"Umoja wa matifa waomba kuunga mkono"

Muhusika wa mauaji ya halaiki ya Rwanda afungwa maisha.

Arusha, Tanzania - 18/12/08.Aliyekuwa mmoja ya maafisa wakuu wa jeshi la Rwanda, Theoneste Bagasora mwenye umri wa miaka 67, ameukumiwa kwanda jela maisha, baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika moja kwa moja katika mauaji ya halaiki yaliyo tokea nchini Rwanda mwaka 1994, ambapo zaidi ya watu 8,00,000, wengi wao wakiwa wa jamii ya Kitutsi na Wahutu wenye msimamo wawastani.
Picha hapo juu anaonekana, Theoneste Bagosora, akiwa mahakama kusikilaza hukumu yake.
Chini anaonekana, mlinzi wa mahakama, akimwelekeza yakuwa asimame, huku anaonekana Theoneste Bagasora, akimwangalia mlinzi tayari kunyanyuka kwenda kuanza kutumikia kifungo.
Nguvu za kijeshi za Kirusi bado zazunguka Latini Amerika.
Havana, Kuba - 18/12/08. Serikali ya Kuba, imezikaribisha nguvu za kijeshi kutoka nchi ya Urusi hivi karibuni, akiongea hayo,Capt. Igor Dygolo, alisema hii ni moja ya safari, ambapo ya melikebu za kijeshi zinafanya ziara katika maeneo ya Latini Amerika.
PIcha hapo juu,wanaonekana rais wa Urusi, Dmitry Medvedev akikaribishwa na mwenyeji wake rais wa Kuba Raul Castro, mapema walipo kutana mjini Havana.
Chini ni zinaonekana melikebu, zikiwa njiani kuelekea kwenye bahari ya Kuba.
Hali yawa ngumu kwa Joseph Koni"Umoja wa mataifa waombwa kuunga mkono'.
Kampala,Uganda - 17/12/08 . Mwakilishi maalumu wa anayeshughulikia suruhisho la kuleta amani nchini Uganda kati ya serikali na kundi linalo pinga serikali ya Uganda LRA Load Resistance Army , na ambaye ni rais wa zamini wa Msumbiji, Joachim Chissano, ameiomba Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa,kuunga mkono nguvu za kijeshi zilizoanza hivi karibuni kaskazini mwa Uganda,ili kumshinikiza Joseph Koni kutia saini mkataba wa amani.
Hata hivyo, Joseph Koni, alitoa sharti ya kuwa ni lazima,hati ya kukamatwa kwake na wenzake ifutwe, ndipo maswala mengine ya tufuatilia. Picha hapo juu ni ya rais wa zamani wa Msumbiji, ambaye ndiye msuruhishi wa matazizo yaliopo nchini Uganda.
Picha yapili anaonekana,Joseph Koni, akiwa amezungukwa na walinzi wake huko mafichoni.
Bei yamfuta kupunguzwa, wasema viongozi wa OPEC.
Oran,Algeria - 17/12/08 . Jumuia ya nchi zinazo toa mafuta duniani (OPEC) - Organisation of Petroleum Exporting Countries, zimekubaliana kwa pamoja kupunguza bei ya mafuta,ili kuweza kukizi mahitaji ya jamii.
Akiongea hayo,Chekib Khelil, ambaye ni rais wa OPEC, alisema nimatumaini yangu tumewashangaza wengi,na hii itasaidia kupunguza bei ya baadhi ya vitu vingine.
Picha hapo juu anaonekana, rais wa OPEC, Chekib Khelil, akiongea na waandishi wa habara baada ya mkutano mjini Oran.

No comments: