Sunday, February 1, 2009

Hekalu la Kiyaudi lavamiwa "La chorwa na kuandikwa maneno ya kutisha"

Rwanda na JKK, kudumisha uhusiano zaidi. Kinshasa, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo - 01/02/09.Serikali ya Kinshasa na serikali ya Kigali, zipo mbioni kudumisha uhusiano ambao umekuwa ukiyumba kwa muda mrefu. Kwa mujibu wa serikali zote mbili,hali ya ushirikiano inaanza kuonekana na itadumishwa zaidi. Kurudisha uhusiano kati ya JKK na Rwanda, kulisaidia kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani wa Serikali ya JKK,Mej, Laurent Nkunda hivi karibuni na majeshi ya Rwanda. Picha hapo juu ni wanaonekana watoto wawili wakiwa wamesimama , huku hawajui waende wapi,hii inatokana na hali iliyopo kiusamalama nchini JKK. Matukio ya moto yapoteza maisha ya watu na mali nchini Kenya. Nairobi,Kenya - 01/02/09.Moto mkubwa ume poteza maisha ya watu zaidi ya 100,bada ya ya lori la kubebea mafuta kuanguka na kumwaga mafuta barabarani. Watu hao wapatao 100, alipoteza maisha yao baada ya kuanza kukusanya mafuta yaliyo mwagika na kuanza kuyazoa, ndipo moto ulipo lipuka ghafla na kuwaunguza watu wote walio kuwa wakikusanya mafuta hayo, aliseama raia mmoja aliyekuwepo kwenye tukio hilo. Wakati huo huo moto mkubwa mwingine uliunguza duka moja kubwa lijulikanalo kama Nakumatt, nakupoteaz maisha ya watu 24, hata hivyo chanzo cha motoi huo bado hakijajulikana na polisi bao inaendela na uchunguzi zaidi. Hekalu la Kiyaudi lavamiwa"La chorwa na kuandikwa maneno ya kutisha. Caracas, Venezuela-01/02/09.Watu wapatao 15 wasiojulikana wamevamia Hekalu la Kiyaudi jijini Caracas, na kuharibu mandhali ya Hekalu hilo. Watu hao waliwashinda nguvu , walinzi wa Hekalu hilo, nakuingia ndani nakuanza kuchora katika ukuta kwa rangi nyekundu, na kuandika maandishi ya kutishia jamii ya Kuyaudi. Kwa mujibu wa kiongozi wa Kiyaudi nchini Venezuela,alisema tukio hili ni la kutisha, la hatari na kuashiria hatari inayo ikabili jamii ya Kiyaudi. Picha hapo juu ni ndani ya Hekalu la Kiyaudi ambalo limechorwa picha za kutisha na maelezo ya kuhatarisha jamii ya Wayaudi waishio jijini Caracas. Somalia yapata rais mpya. Ahaidi kuleta mabadiliko ya nchi nzima"

Djibouti, Djiubouti - Sheikh Sharif Ahmed, amechaguliwa kuwa rais wa Somalia, katika uchaguzi ulio fanyika jiji Djibout, 31/01/09.
Sheikh Sharif Ahmed, ambaye hapo mwanzo alikuwa adui mkubwa wa Amerika,ameungwa mkono na nchi nyingi za Magharibi ikiwemo Amerika.
Hata hivyo kwa mujibu wa wachunguzi wa mambo ya kisiasa ya Somalia, wamesema rais Sheikh Sharif Ahmed anayokazi ngumu ya kurudisha amani nchini Somalia, nchi ambayo imekuwa katika vita kwa kipindi kisicho pungua miaka 20.
Wakati huo Maharamia wa kundi moja nchini Somalia, wameteka nyara meli ya mafuta ya Kijerumani.
Picha hapo juu ni ya rais mpya wa Somalia Sheikh Sharif Ahmed, akiongea mara maada ya kuchaguliwa kwake kuwa raia wa Somalia.
Picha ya pili, raia mpya wa Somalia, Sheikh Sharif Ahmed,akiongea na Kanali Omar Hashi, mara baada ya uchaguzi wa rais.
Picha ya tatu ni ya meli iliyotekwa na maharamia wa Kisomalia.
Viongozi wa Kuba na Urusi,wakutana nchini Urusi"Ni ziara ya Kwanza tangu kuisha vita barudi".
Moscow,Urusi - 29/01/09.Rais wa Kuba,Raul Castro amefanya ziara ya kiserikali nchini Urusi.
Katika ziara hiyo rais Raulu Castro, atafanya mazungumzo na rais wa Urusi Dmitry Medvedev.
Ziara ya ya rais wa Kuba Raul Castro nchini Urusi, ni ya kwanza tangu kuisha kwa vita baridi kati ya jumuia ya NATO na WARSAW PAST.
Picha hapo juu,anaonekna rais wa Kuba, Raul Castro akikagua gwaride la heshima alilo andaliwa na mwenyeji wake rais wa Urusi Dmirty Medvedev.

No comments: