Thursday, January 14, 2010

Google hatarini kufungwa nchini China.

Kiongozi wa Guinea awasili Bukinafaso kuepuka utata. Conakri, Guinea-14/01/2010. Kiongozi wa kijeshi wa Guinea, Moussa Dadia kamara, amewasili nchini Bukinafaso kwa mujibu wa wizara ya mambo yanchi za nje wa nchini hiyo. Moussa Dadis Kamara, aliwasili Ouagadougou siku ya Jumanne kutokea nchini Moroka ambapo alikuwa kwaajili ya matibabu baada ya kunusulika kuuwawa kwa kupigwa risasi ya kichwa na mmoja ya walinzi wake. Kuwasili kwa Moussa Dadia Kamara nchini Bukinafaso kumekuja baada ya habari yakuwa serikali ya Moroko imekuwa ikitakiwa kumpeleka mkuu huyo wa nchini ya Guinea katika nchi za Ulaya ili ashitakiwe kwa makosa ya mauaji ya raia wakati wa maandamano yaliyo fanyika mwaka jana. Picha hapo juu anaonekana mkuu wa jeshi na kiongozi wa Guinea, Moussa Dadis Kamara, baada ya jeshi ya kuchukua madaraka nchi Guinea japo kulipingwa na wengi. Google hatarini kufungwa nchini China. Beijing,China -14/01/2010.Serikali ya Chini imesema kampuni yoyote inayo taka kufanya biashara nchini humo lazima ifuate sheria za nchi -China. Msemaji wa serikali ya China, Wang Che alisema" ikiwa kampuni ya internet itaenda kinyume na sheria ya serikali basi hatua za kisheria zitachukuliwa na hata kampuni kufungwa." Maelezo hayo yametolewa baada ya kamuni ya mtandao ya Google kulalamika ya kuwa mitandao yake imekuwa ikishabuliwa na kushindwa kutoa huduma nzuri kwa jamii nzima iliyopo China na huenda wakafunga ofisi zao nchini humo. Picha hapo juu in nembo ya Google nchini China, ambapo kampuni hiyo imekuwa ina vutana na serikali ya China katika kutoa huduma za kimtandao kwa wanchini wa nchi hiyo. Viongozi wa dini nchini Yemeni watoa onyo. Sanaa, Yemen-14/01/2010. Viongozi wa kidini nchini Yemen, wamesema yakuwa ikiwa nguvu za kijeshi zitatumika na jeshi la kigeni kuingia nchini mwao, basi litakuwa ni jikumu la kila Myameni kuilinda nchi yao kufautia sheria za dini. Katika barua ambao imesainiwa na vingozi wa kidini wapatao 150 ulisema "itakapo fikia hatua ya nchi za nje kushambulia Yemeni, basi lazima wajue yakuwa vita vitakuwa vita vya jihadi." Kwa mujibu wa wachunguzi wa mambo ya kisiasa nchini Yemeni, wanasema" ikiwa viongozi wa kidini wameingilia swala la hali ya Yemeni, basi huenda kukalete mabadiliko makubwa na mwelekeo mzima wa kuitizama Yemeni." Hata hivyo, Amerika na nchi za Ulaya zimekuwa ziliilaumu Yemeni kwa kuwa kituo kikubwa cha kufunzia wapiganaji wa kundi la Al-Qaeda. Picha hapo juu ni ya jiji la Sanaa, mji mkuu wa Yemen, nchi ambayo imekuwa na mvutano wa kisiasa kwa muda mrefu Wananchi wa Haiti wakumbwa na tetemeko la ardhi.

Port-au-Prince,Haiti -14/01/2010.Maelfu ya watu wamepoteza makazi yao na mamia kupoteza maisha baada ya tetemeko la ardhi lenye nguvu za nyuzi 7.0 kutokea nchini Haiti.
Kwa mujibu wa habari zinasema tetemeko hilo la ardhi limeleta maafa makubwa kwa jamii nzima ya Haiti.
Kufuatia tetemeko hilo la ardhi, umoja wa mataifa na nchi tofauti duniani zimeanza kutoa misaada yakila aina ili kuwasaidia rais wa Haiti.
Picha hapo juu, wanaonekana vijanawakimsaadia mmoja wa watu ambao wameumia kuktokana na tetemeko la ardhi.
Picha ya pili anaonekana mwamama akiwa amezungukwa na vumbi na matofari ya nyumba iliyobomoka wakati akiwa katika eneo analo kaa na kusababisha majeruhi kwa watu waliokuwa karibu na jengo hilo.

No comments: