Tuesday, January 5, 2010

Iceland mashakani kulipa madeni.

Mshitakiwa wa 9/11 akataliwa rufaa. Washington, Amerika - 05.01/2010.Mahakama ya imetupilia mbali rufaa iliyokuwa ime ombwa na mshitakiwa Zakaria Massaoui, anayeshukiwa kuhusika na mashambulizi ya Septemba 11.2001 yaliyo tokea jijini New York na kupoteza maisha ya watu wapatao 3000 na wengine kujeruhiwa vibaya. Kufuatia uamuzi huo wa mahakama, Zakaria Massaoui ambaye ndiye mshitakiwa ataendelea kutumikia kifungo cha maisha. Picha hapo juu ni ya mtuhumiwa wa mauaji ya Septemba 11 2001, ambaye rufaa yake imekataliwa na mahakama.

Iceland mashakani kulipa madeni.
Reykjavik, Iceland - 05/01/2010. Rais wa Iceland amekataa kusaini muswada uliopitishwa na bunge la nchini hiyo ili kulipa madeni ambayo nchi hiyo inadaiwa na Uhollanzi na Uingereza.
Rais wa Iceland Olafur Ragnar Grimsson, alisema "swala hili litaamuliwa na wananchi kwa kupigwa kura ya maoni,"kwani wanchindiyo wakatao amua nini mbeleni watakabiliana nacho.
Hata hivyo viongozi wa Uhollanzi na Uingereza wamesikishwa na uamuzi huo na wameitaka nchi hiyo kulipa deni hili la pesa ambazo Iceland ilipewa wakati wa mporomoko wa masoko ya fedha yaliyo tokea mapema miaka miwili iliyo pita.
Picha hapo juu wanaonekana wanchi wa Iceland, wakiandamana kupinga uamuzi wa serikali yao kutaka kulipa deni ya pesa zilizo kopwa kutoka wa Uhollanzi na Uingereza.
Kachero wa ajitolea muhanga.
Jimbo la Khost Afghanistan - 05/01/2010.Muaji wa kujitolea muhanga aliye sababisha vifo vya makachero wa Amerika CIA na Joradan, ametambuliwa ya kuwa alikuwa kachero aliyekuwa akifanya sehemu mbili tofauti za upererezi.
Kachero huyo raia wa Jordan Hammam Khalil al Balawi, "inasemekana alikuwa amechaguliwa na ofisi ya makachero ya Jordan kufanya kazi nao, ili kujua mbinu za kundi la al Qaeda."
Hammam Khalil al Balawi, alidai "ataweza kutoa habari wapi moja wa viongozi wa al Qaeda
walipo."
Picha hapo juu wanaonekana mwili wa mmoja wa makachero wa Jordan ukiwa umbebwa mara baada ya kuwasili Jordan tayari kwa mazoshi.
Rais Zuma aongeza jiko la tatu.
Kwazulu Natal, 05/01/2010. Afrika ya Kusin - Rais wa Afrika ya Kusini Jokob Zuma, amefunga pingu kwa mara ya nne mapema wiki hii.
Harusi hiyo iliyo fanyika Nkandla, 67 rais Jakob Zuma, amefunga pingu za maisha na bi Tobeka Madiba 37 ambaye tayari anawatoto watatu wa Jakob Zuma.
Sherehe hiyo iliyo udhuliwa na viongozi wa serikali na wa kitamaduni pamoja na wafanya biashara kutoka sehemu tofauti nchini Afrika ya Kusini.
Picha hapo wanaonekana wapendanao walio funga pingu za maisha Tobeka Zuma kushoto na kulia Jakob Zuma wakicheza ngoma ya kiasili ya Kizulu wa wakati wa sherhe yao ya kufunga pingu zamaisha iliyo fanyika siku ya Jumatatu.
Picha ya pili, anaonekana rais wa Afrika ya Kusini Jakob Zuma, wa pili kulia akiwa na wake zake watatu mara baada ya kufunga ndoa na bi Tobela wa pili kulia.

No comments: