Sunday, January 24, 2010

Evo Morales aapishwa kuwa rais wa Bolivia.

Evo Morales aapishwa kuwa raia wa Bolivia La Pazi, Bolivia - 24/01/2010. Wanachi wa Bolivia kwa maro nyingine tena wameshuhudia kuapishwa kwa raia Evo Morales kuwa rais wa nchi hiyo. Evo Morales, alichaguliwa kufatia uchaguzi uliofanyika mwaka jana. Kwenye sherehe hiyo iliudhuliwa na raiwa Venezuela Hugo Chavez, na rais wa Ekuador Rafael Correa. Picha hapo juu ni rais wa Bolivia, Evo Morales, mara baada ya kuapishwa kuwa rais wa Bolivia baada ya kushinda uchaguzi wa urais Bolivia. Korea ya Kaskazini yatishia kutumia nguvu za kijeshi.

Pyongyang, Korea ya Kaskazini - 24/01/2010. Serikali ya Korea ya Kaskazini imeonya ya kuwa itakuwa tayari kuishambulia Korea ya Kaskazini kutokana na kauli iliyotolewa na wakuuwa jeshi wa nchini hiyo.
Onyo hilo limekuja baada ya viongozi wa jeshi la Korea ya Kaskazini kudai hawakubaliani na Korea ya Kaskazini kuwa na mitambo ya nyuklia.
Kufuatia maelezo hayo, serikali ya Korea ya Kaskazini, inalichukulia kama tishio la usalama wa nchi na hivyo hii swala lina weza kuleta vita.
Picha hapo juu, ni bendera ya Korea ya Kaskazini, nchi amabyo imekuwa na mvutano na jumuia ya Kimataifa kuhusu swala la nguvu za nyuklia katika nchi hiyo.
NATO kutumia mbwa kunusa mabomu ardhini.

Kandahar, Afghanistan - 24/01/2010. Jeshi la NATO na washirika wake limeanza kutumia mbwa kujaribu kunusa na kutambua yaliyo tegwa ardhini.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana, zinasema yakuwa hadi kufikia hivi sasa kuna mbwa wapatao 20 na idadi hiyo itaongezeka hadi kufikia zaidi ya mbwa 200.

Mbwa hao amabo huenda wakaghalimu $ dola 40,000 kwa mwaka huwa wanafunzwa kwa muda wa miezi mitano.

Picha hapo juu anaonekana mmoja ya mbwa akiwa kazini kunusa wapi mabomu yametegwa.

No comments: