Saturday, January 2, 2010

Yamen kupata misaada kupambana na Al Qaeda

Mwasisi wa chama tawala Tanzania aiaga dunia

Dar es Salaam,Tanzania - 02/01/2010. Wananchi wa Tanzania wameaanza kuombeleza kifao cha aliyekuwa kiongozi imara wakati wa kupigania uhuru hayati Rashid Kawawa.
Rashid Kawawa alifariki dunia katika hospitali ya Muhimbili iliyoko jijini Dar es Salaam Tanzania
Rashidi Kawawa alikuwa mwasisi wa chama tawala cha Tanzania CCM, pia aliwahi kushika nyazifa mbalimbali wakati wa serikali ya hayati Mwalimu Julius Nyerere, na kuwa mmoja wa viongozi walioaminika saana na Mwalimu Julias Nyerere wakati wa uongoziwake.
Picha hapo juu anaonekana hayati Rashid Kawawa akiwa tayari kuchezesha mechi ya mpira wa miguu enzi zake kama mwamuzi wa soka.
Picha ya pili, aanaonekana hayati Rashid Kawawawa tatu kulia, akiwa na viongozi wenzake mara baada ya muungano wa Zanziba na Tanganyika.
Picha ya tatu , anaonekana enzi za uahai wa Rashid Kawawa, akiwa amevalia shati la kijani ambalo ni vazi lasmi la cham tawala CCM.
Picha ya mwisho anaonekana rais wa Tanzania , Jakaya Kikwete, kushoto akiongea na hayati Rashid Kawawa,wakati rais Kikwete alipo kwenda kumtembela nyumbani kwake.
Yemen kupata misaada kupambana na Al Qaeda.
Washington, Amerika - 02/01/2010. Rais wa Amerika, Baraka Obama ameseama yakuwa shambulizi lililo shindwa kufanyika siku ya Krismas kwenye ndege ya shirika la Delta ilyo kuwa ikitokea Amsterdam kuelekea Detroit lilikuwa limepangwa na kundi la Al Qaeda.
Baraka Obama, aliyasema yakuwa mtuhumiwa wa tukio hili raia wa Nigeria, Umar Farouk Abdulmutallab, alipewa mafunzo hayo wakati alipo kuwa nchini Yemen na kuhaidi kuzidisha ulinzi wa usalama wa Amerika na kuhaidi kuongea misaada kwa serikali ya Yemen kwa ajili ya kupambana na kundi la Al Qaeda na washiriki wake.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya wanachama wa kundi la Al Qaeda wakiwa katika mkutano nchini Yemeni.
Wafanyakazi wa Blackwater waachiwa huru na mahakama.
Baghdad, Irak - 02/01/2010. Serikali ya Irak, inapanga kufungua kesi dhizi ya kampuni ya ulinzi ya Blackweter ambao waliusika katika mauaji ya raia wa Irak.
Uamuzi wa serikali ya Irak, kutaka kufungua tena kesi hiyo, kumekuja baada ya hakimu wa mahakama Ricardo Urbina, kufuta kesi iliyo kuwa ikiwakabili wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya Blackwater.
Kwa mijibu wa mshauri wa serikali,Saad al Muttalib, alisema "uamuzi wa mahakama hiyo, umeleta mshangao mkubwa kwa wanchi wa Irak na uhenda ukaleta utata wa ushirikiano wa nchi mbili hizi."
Hata hivyo, wafanyakazi wa kampuni hiyo ya ulinzi Blackwater, "walidai yakuwa walianza
kushwambuliwa na ndipo walijibu mashambulizi hayo"
Kampuni ya Blackwater inashughulika na ulinzi wa aina tofauti duniani.
Picha hapo juu inaonekana moja ya gari ambalo lilimelipuliwa kutokama na hali ya kutokuwa na usalama wakuridhisha.

No comments: