Saturday, January 9, 2010

Timu ya taifa ya Togo yashambuliwa kwa risasi nchini Angola.

Timu ya taifa ya Togo yashambuliwa kwa risasi nchini Angola. Kabinda, Angola-09/01/2010. Mashindano ya kutafuta bingwa wa mchezo wa Soka katika bara la Afrika, yaliongia dosali baada ya timu ya taifa ya Togo kushambuliwa kwa risasi na kundi linalo pigania kujitenga na kutete eneola Kabinda. Mashambulizi hayo yalitokea wakati timu ya taifa ya Togo ilipo vuka mpaka wa Kongo na kuingia nchini Angola kwa kutumia usafiri wa basi. Kufuatia mashambulizi hayo, dereva wa basi aliuwawa hapo hapo, kocha msaidizi alipoteza maisha baadaye na baadhi ya wachezaji kujeruhiwa vibaya. Picha hapo juuanaonekana, kaptain wa timu ya taifa ta Togo, Emmanuel Adebayor, akisaidiwa na mmoja wa mchezaji mwenzake mara baada ya kuokolewa na vyombo vya usalama vya serikali yaAngola. Kiongozi wa mkuu wa Iran aagiza atua kali zichukuliwe. Tehran, Iran - 09/01/2010. Kiongozi mkuu wa Iran ameagiza vyombo vya usalama nchini Iran kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya viongozi wa na wanachama wa vyama pinzani vinavyo leta vurugu na kuipinga serikali. Kiongozi huyo Ayatollah Ali Khamenei alizilaumi nchi za kigeni kwa kuchochea vurugu nchini Iran kwa kutumia vyama vya upinzani. Hata hivyo habari kutoka kambi ya vyama vya upinzani zina sema watu wapatao 180, walikamatwa hivi karibuni wakiwepo waandishi wa habari. Akithibitisha kukamatwa kwa watu waliokuwa wakiandamana, wakili wa serikali Abbs Jafari Dolatabadi alisema"kesi dhidi ya watu wote waliokamatwa zitaanza wiki hii." Amani yaingia utata Sudan ya Kusini. Khartoum, Sudan -09/01/2010. Vita vya ukabila vimeanza tena kusini mwa nchi ya Sudan, na kusababisha zaidi ya watu wapatao 139 kupoteza maisha yao. Kwa mujibu wa msemaji wa serikali Sabino Makana, alisema "vita hivyo vilitokea kati ya kabila la Nuer na Dinka wakati walipo kuwa wakigombania mifugo." Habari kutoka ofisi za UN zinasema ya kuwa mapambano hayo yameanza mapema mwaka huu na yanaweza kuhatarisha mkataba wa amani uliokubalika miaka ya nyuma. Picha hapo anaonekana mmoja ya mkazi wa Sudan ya kusini akiwa anachuga mifugo yake, ambayo ilikuwa chanzo cha kuzuka kwa vita vya kikabila katika eneo hilo hivi karibuni. Aliyetaka kuilipua ndege akanusha mashitaka. Detroit, Amerika - 09/01/2010. Raia wa Nigeria, Umar Farouk Abdulmutallab, amekanusha mashitaka yake ambayo yanamkabili kwa kutaka kulipua ndege iliyokuwa imebeba abiria ikitokea Amsterdam. Alikanusha mashitaka hayo wakati alipo tokea mahakamani kusilikiliza mashitaka hayo. Kufuatia kukanusha mashitaka kwa mtuhumiwa huyo kesi hiyo ilihairishwa. Picha hapo juu ni ya mshitakiwa anayeshutumiwa kwa kutaka kulipua ndege iliyokuwa ikitokea Amsterdam kuelekea Amerika.

No comments: