Saturday, April 24, 2010

G-20 bado ya simama njia panda.

Iran na Zimbabwe zakubaliana kushirikiana.

Harare,Zimbabwe - 24/04/2010. Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad amemaliza ziara yake nchi Zimbabwe.
Katika ziara hiyo rais wa Iran, alifungua maonyesho ya biashara katika mji wa Bulawayo baada ya kumaliza kusaini mkataba wa kiuchumi kati ya Zimbabwe na Iran.
Picha hapo juu wanaonekana rais wa Iran kushoto akiwa na mwenyeji wake rais wa Zimbabwe mara baada ya rais wa Iran kuwasili nchini Zimbabwe.
G-20 bado ya simama njia panda.
Washington, Amerika - 24/04/2010. Serikali za nchi wanachama wa kundi la G-20 wameshindwa kuafikiana kuhusu kodi za mapato katika mabenki yote duniani.
Akiongea hayo waziri wa fedha wa Kanada alisema "katika kikao walikuwepo wajumbe walio kubali na wajumbe wengine walipinga kabisa." Kikao hicho kiliitishwa ili kujaribu kutafuta njia ya kukabiliana na hali ya mzunguko wa pesa za mabenki. Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya mawaziri wa fedha wakijadiliana mara baada ya kikao kilichofanyika kutathmini hali halisi ya mzunguko wa fedha. NATO yajadili mbinu za kukabidhi madaraka kwa Waafghanistan.
Talinn, Estonia 24/04/2010. Viongozi wa NATO wamekutana nchini Estonia kujadili kwa undani jinjia gani watafanya kujiandaa kuondoa majeshi nchini Afghanistan.
Mkutano huo ulioudhuliwa na viongozi wa nchi 28, walikubaliana kwa misingi ya kuimarisha jeshi na polisi la nchi ya Afghanistan ili washike madaraka na kusimamia ulinzi wa nchi.
Akiongea mbele ya wajumbe, katibu mkuu wa NATO, Anders Fogh Rasmussen, alisema"Serikali ya Afghanistani ina endelea vizuri katika ulinzi wa nchi na hivyo kuna haja madaraka yote yawe chini ya uongozi wa serikali ya Afghanistan."
NATO inatarajia kuanza kupunguza majeshi yake nchini Afghanistan kuanzia mwaka 2011.
Vita vya Afghanistan vilinza kwa ajili ya kupambana na makundi ya ugaidi ya Taliban na Al-qaeda.
Picha hapo juu wanaonekana viongozi wa nchi za NATO wakiwa katika mkutano kujadili mbinu mbada kuhusu Afghanistan.

No comments: