Kiongozi wa mlango wa kulia nchini Afrika ya Kusini auwawa.
Havana Kuba - 05/04/2010. Rais wa Kuba amesema ya kuwa serikali na wanchi wa Kuba hawata kubali kuyumbishwa wala kutetereka kwa njama za watu amabo wanaacha kula kwa sababu fulani.
Rais Raul Castro, aliyasema haya wakati alipokuwa akiwahutubiwa wanachi wa Kuba siku ya Jumapili kwa kusema "nchi za Ulaya na Amerika zina jitahidi kwa kwakila njia kuleta matatizo ndani ya nchi," "Kuba" "kwa kuwawashawisha wapinzani wa serikali kufanya mambo yasiyo ya kawaida."
Wakati huo huo mwandishi wa habari Guillermo Firinas amegoma kula kwa kudai wafungwa wa kisiasa waachiwe huru
Kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu, zinasema "Kuba inawafungwa wapatao 55 ambao wapo jela."
Picha hapo juu anaonekana Guillermo Firinas, akipelekwa hospital ili kupata matibabu baada ya kugoma kula mpaka madi yake yatimizwe.
Wananchi wa China wajawa na furaha kubwa.
Shanxi, China - 05/04/2010. Watu wapata 110 wameokolewa kutaka ndania ya machimbo ( migodi) ambayo ilipasuka na kujaa maji kwa kipindi cha wiki moja iliyo pita.
Watu hao walichukuliwa na kupelekwa hospitali kwa ajili ya kuangaliwa afya zao zaidi.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali Liu Dezheng alisema, " maajabu na ni kweli na imetokea kama tulivyo kuwa tunaamini na hatimaye tume fanikiwa kuwaokoa wenzetu"
Viongozi na wanchi wa China wamewapongeza waokoaji wote kwa kazi nzuri waliyoifanya na nifuraha kubwa kwa wanchi wote wa China.
Picha hapo juu wanaonekana wakiwa wamembeba mmoja ya wafanyakzai waliokuwa wamekwama ndani ya mgodi baada ya kumtoa ndani ya mgodi.

No comments:
Post a Comment