Waingereza wajiandaa kuchagua waziri mkuu mpya .
London, Uingereze 08/04/2010. Kampeni za uchaguzi nchini Uingereza zimeaanza rasmi, mara baada ya waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown,kutangaza rasmi ya kuwa siku ya uchaguzi mkuu utakuwa April 6 /2010.
Kwa mujibu wa wachunguzi wa maswala ya kisiasa. wanasema uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa ni wa kihistoria, kwa kuzingatia ya kuwa serikali iliyopo madaraka ni ya Gordon Brown, ina upinzani mkubwa sana kutoka kwa David Cameron ambaye anagombe kiti cha uwaziri mkuu kupitia chama cha Conservative.
Picha hapo juu wanaonekana David Cameron kushoto na Gordon Brown kulia ambao wanagombe kiti cha uwaziri mkuu wa Uingereza katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu April 6/ 2010.
Amerika na Urussi za tiliana sahihi mkataba wa kupunguza zana za kivita za kinyuklia.
Prague,Cheksi - 08/04/1020. Marais wa Amerika na Urussi wametia sahii mkataba wa kupunguza uzalishaji wa nguvu za zana za kijeshi za kinyuklia.
Maraias hao Baraka Obama na Dmitri Medvedev walisaini mkataba huo katika mji wa Prague uliopo Jamuhuri ya Cheksi.
Akiongea mara baada ya kutia sahii, rais wa Amerika, Baraka Obama alisema " Amerika na Urussi haziwezi kufanyakazi ikiwa hazita shirikiana hasa katika maswala makubwa ambayo yana husu hali halisi ya dunia."
Naye rais wa Urussi Dmitri Medvedev alisema , hii ni siku ya kukumbukwa kihistoria na itafungua ukurasa mpya na pande zote zitafaidika na mkataba huu."
Picha hapo juu wanaonekana, ais wa Amerika Baraka Obama kushoto na rais wa Urussi, Dmitri Medvedev, wakisaini mkataba wa kupunguza nguvu za zana za kijeshi za nyuklia walipo kutana Prague.
Thursday, April 8, 2010
Waingereza wajiaanda kuchagua waziri mkuu mpya.
Posted by
Kibatala
at
Thursday, April 08, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment