Wednesday, April 21, 2010

Hatimaye mama asilia atoa ruhusa kwa ndege kuruka.

Hatimaye mama asilia atoa ruhusa kwa ndege kuruka.

Brussel,Ubeligiji - 21/04/2010. Ndege zimeanza kuruka tena angani baada ya kushindwa kuruka kutokana na mavumbi ya mlipuko wa volkano yaliyo tokea katika kisiwa cha Iceland kwenywe milima ya Eyjafllajoekull siku sita zilizo pita.
Kwamujibu wa habari kutoka kwa shirika la anga la Ulaya zinasema "bado kuna baadhi ya maeneo hali ya hewa hijawa safi kwa usafiri wa anga."
"Hata hivyo huenda safari za ndege zikaanza mapema mwisho wa wiki hii zilimalizia habari kutoka kwenye shirika hilo la anga la Ulaya".
Picha hapo juu inaonekana ndege ikielekea kutua kwenye kiwanja cha ndege cha Heathrow lilichopo Uingereza mapama hivi leo,baada ya siku sita za kushindwa kuruka angani kutokana na madhara yaliyo sababishwa na mama asilia.

No comments: