Monday, April 7, 2014

Rais Paul Kagame awakalia kidede waliohusika na mauaji ya kimbari.

Rais Paul Kagame awakalia kidede waliohusika na mauaji ya kimbari.

Kigali, Rwanda - 07/04/2014.
Wanachi wa Rwanda wameadhimisha kumbumbu  ya mauaji ua kimbari yaliyotokea mwaka 1994 ambapo zaidi ya watu 800,000 waliuwawa katika mauaji ambayo yalichukua zaidi ya siku miamoja.

Rais Paul Kagame, akilihutubia taifa katika kuadhimisha siku ya mauaji ya kimbari amesema " japokuwa muda umepita ukweli upo katika historia ambayo ipo na itajiandika, kwani watu au nchi hawawezi kuhonga au kulazimisha kubadirisha historia japo wawe na nguvu au kuwa nguvu kwani ukweli upo wazi"

" Na miaka 20 sasa cha muhimu ni  kuwa hawa kuwa na imani ya kusimamisha mauaji ya Wanyarwanda na wanachofanya ni kukanusha."
 "Wanyarwanda wanatakiwa kujua uhai na thamani ya mtu ambayo wenzetu hawajui nini maana yake na kuitumia vibaya."

Kabla ya kuhutubia, rais Kagame mbele wa wageni waalikwa aliwasha mwenge wa amani  ambao utakimbizwa kwa kuzungushwa nchi nzima kwa muda wa siku 90 ikiwa ni ishara ya kukumbuka siku ambazo mauaji ya kimbari nchini Rwanda 1994. 

Rais Paul Kagame amekuwa akizilaumu  Belgium na Ufaransa kwa kuhusika na mauaji ya kimbari yaliyo tokea nchi Rwanda mwaka 1994 na kuzitaka nchi hizo kuwa za uwazi katika ukweli, kwani histotoria ya mauaji ya Wanyarwanda itakuwa nao daima japo nchi hizo zimekuwa zikikanusha kuhusika na mauaji hayo.

Aliyekuwa rais wa Pakistani anusurika Kifo.

Rawapindi, Pakistan - 07/04/2014. Aliyekuwa rais wa Pakistani na ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi ya uhaini ameponea chupu chupu na jaribio la kutaka kumwua ambalo lilifanyika hivi karibuni.

Pervez Musharraf alipona hali hiyo ya kutaka kuuwawa baada ya bomu kulipuka katika daraja lililopo njia ambayo muda mchache Musharraf alitakiwa kuitumia kuelekea katika kambi ya jeshi iliyopo Rawapindi ambapo alitakiwa kwenda kufanyiwa uchunguzi wa kiafya.

Musharafu ambaye kwa sasa anaishi nje kidigo ya jiji la Islamabadi alielekea hospital kwa kutumia njia nyingine ambayo ilikaguliwa na walinzi wake.

Kupona huko kwa Pevez Musharraf kumekuja  kwa mara ya pili, baada ya  bomu kulipuka Desemba  2003 katika maeneo ya Rawapindi baada ya msafara wake kupita katika eneo ambalo bomu lilikuwa limetegwa  na kumkosa kwa dakika chache.

Kundi la Taliban limekuwa likihaidi kumwua kiongozi huyo, ambaye alichukua madaraka kwa nguvu za kijeshi mwaka 1999 na baadaye kuwa rais tangu mwaka 2001 -2007.

Rais Assad atuma salamu kamambe  kwa rais wa Urusi.

Damascus, Syria - 07/04/2014. Rais wa Syria amefanya mazungumzo na aliyekuwa waziri mkuu wa Urusi Sergi Stepashin na kujadili ni kwa jinsi gani nchi hizo zitazidi kushikiana.

Rais Bashaar al Assad katika mazungumzo hayo alisema  " naomba kamwambie Vladmir Vladimirovich Putin kuwa mimi  nipo na sitaondoka kama alivyo ondoka rais wa Ukraine Viktor Yanukovich"

"Na hii hali ya kivita tutaimaliza na kushinda, kwani serikali yangu ipo imara na kupambana na  magaidi wanaodhaminiwa na wapinzani wenye nia mbaya na Syria kwa tamaa zao."

 Sergi Stepashim ambaye alikuwa waziri mkuu wakati wa utawala wa  rais Boris Yeltsin amesema " Assad  inaungwa mkono na watu wengi nchi Syria na hata kama kura zikipigwa leo atashida"

" Na kwa kuwa anataka kugombania uchaguzi ujao basi naimani atashida kwa kura nyingi bila shida"Alimalia Sergie Stepashin.

Urusi imekuwa nchi ambayo inaungana mkono serikali ya rais Assad, ambaye kwa sasa nchi yake ipo katika vita ambavyo vimeanza zaidi ya miaka miwili kati yaserikali na makundi ya upinzani ambayo inasadikika kuungwa mkono na badhi ya nchi za Magharibi  na nchi za Kiarabu na huku majeshi ya Assad yakiungwa mkono na kundi Hezhibollah.

No comments: