Wednesday, April 9, 2014

Misri nayo ya moto wa kuotea mbali kwa mashoga.

Vurugu na myumbo nchi Ukraine, Marekani yaishutumu Urusi.

Washington, Marekani - 08/04/2014. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani ameishutumu serikali ya Urusi kwa kuendeleza mvurugo na myumbo wa kisiasa nchi Ukraine ambao unapelekea kugawa nchi.

Akiongea mbele ya wajumbe wa Kongresi John Kerry amesema kuwa '' mashushu, makachelo na maafisa usalama wa Urusi wapo nchi Ukraine kusaidia kuyumbisha serikali iliyopo na kuunga mkono wale wote wanao taka mgawanyiko wa nchini Ukraine.''

'' Ushaidi ni kwamba watu ambao wamevamia na kuchukua majengo ya serikali ni wale ambao wanaunga mkono kujiunga na Urusi na na pia kujitenga na serikali ya Kiev, na hii inatokana na ushawishi wa Urusi.''

Hata hivyo serikali ya Urusi imekuwa ikipinga  kwa kudai kuwa vurugu na myumbo wa kisiasa nchi Ukraine umesababishwa na ya Marekani na washiriki  kutokana na malengo na faida wanazojua wenyewe.

Mvurugona wa kuchafuka kwa amani   nchini Ukraine umekuwa  wa kichwa kuuma, tangu kuangushwa kwa serikali ya rais Viktor Yanukovich  ambapo nguvu na maandamano yalitumika na vyama vya upinzani chini Ukraine kwa msaada wa msukumo wa nchi za Ulaya Magharibi na Marekani.na kuleta upya hisia za vita baridi kati na Urusi.

Hadi sasa majimbo ya Donetski na  Kharkiv yamekumbwa na maandamano ya  kutaka kujitenga na serikali ya Kiev, pia baadhi ya watu waliovamia ofisi na majengo ya serikali kudai majimbo hayo yajiunge na Urusi.

Polisi nchini Kenya yasaka wahamiaji haramu.

Nairobi. Kenya - 08/04/2014. Polisi nchi Kenya wapo katika msako mkubwa  kuwakamata watu wote wanao ishi kinyume cha sheria nchini Kenya baada ya matukio ya  mashambuzi ya kigaidi ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa nchi humo.

Katika kufanikikisha zoezi hilo wagtu 4,000 walikamatwa katika jiji la Nairobi, japokuwa polisi wamesema '' ni watu 447 ambao kwa sasa ndiyo bado wanashikiliwa na polisi.''

Kwa mujibu wa balozi wa Somalia nchini Kenya Mohamed Shaik Ali '' watu 82 wamerudishwa nchini Somalia baada ya kukataliwa maombi yao ya kikimbizi.''

Hatua hii ya serikali ya Kenya kufanya msako imekuja baada ya kutoa agizo kuwa watu wote walioomba ukimbizi  kurudi katika makambi ya kikimbizi.

 Agizo hilo lilikuja baada ya shambuli lililotokea katika maeneo ya Elselegh ambapo watu sita walipoeteza maisha kufuatia mashambulizi ya mabomu katika kumbi za starehe kwenye kitongoji hicho.

Kenya imekuwa inakutwa na mashambulizi ya kigaidi, baada ya kundi la Ashabab la Somali kudai kuhusika na ugaidi nchini humo kwa madai yakuwa Kenya imevamia nchini Somalia, jambo ambalo serikali ya Kenya inasema ni katika harakati za kuleta amani katika ukanda wa pembe ya Afrika.

Misri nayo ya moto wa kuotea mbali kwa mashoga.

Kairo, Misri -09/04/2014.  Watu wanne wamehukumiwa kwenda jela na mahakama jijini Kairo, baada ya  kutwa na hatia ya kufanya ushoga na kuwa kimapenzi kwa jinsia moja.

Watu hao ambao wamekutwa na kosa la kupanga na kushiriki kwa makusudi sherehe ya ushoga huku wakiwa wamevaa nguo za kike na ulimbwende wa kina mama walihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka minane na kupewa kazi ngumu wakati wa kipindi chote watakachokuwa jela.

Kufuatia hukumu hiyo, shirika la kutetea haki za binadamu la kutoka Marekani limelaani kitendo hicho na kwa kusema '' kitendo cha kufungwa watu hao ni kimyume za haki za binadamu na kitaleta mlolongo wa hukumu kama katika nchi zenye asili ya  Kiarabu.''

Nchi ya  Misri haina sheria ya kupinga ushoga, lakini mashoga na wale wote wanahusika na tabia hii huwa wanahukumiwa kwa kufuata baadhi ya vifungu ungia vya sheria .

Nchi nyingi za Afrika zimekuwa hazikubaliani na tabia ya ushoga, na hivi karibuni serikali ya Uganda ilipitisha sheria kali ya kupinga ushoga jambo ambalo  nchi za Magharibi zililaani sheria hiyo na pia kutishia kusimamisha baadhi ya misaada kwa Uganda.


2 comments:

Unknown said...
This comment has been removed by a blog administrator.
Nanung Nur Zula said...

nzuri baada ya