Friday, April 4, 2014

Matumizi ya mtandao yatonesha kidondo cha Marekani na Kuba.

Makao makuu ya EU yawa kiwanja cha mapambano.


Brussels, Ubeligiji - 04/04/2014. Polisi katika jiji la Brussels wamepambana na waandamanaji wanao pinga mbinyo wa  matumizi  na mapato yaliyopo katika nchi za jumuiya ya nchi za wanachama wa Ulaya 

Wakitumia majiwasha na mabomu ya kutoa machozi, polisi waliwatawanya wanadamanaji waliyo kuwa katika maeneo ya ofisi za nchi za jumuiya wa umoja wa Ulaya,huku wengi wao walikuwa wanachama wa vyama vya wafanyakazi tofauti vilivyopo katika nchi za hizo.

Waandamanaji walikuwa wamebeba mabango yanayo kosoa mwenendo mzima wa mbinyo wa matumizi na uwekezaji  ambao uongozi wa nchi za jumuiya ya Ulaya umekuwa ukikazania mbinyo huo kama njia pekee ya kuinua uchumi.

Mmoja wa kiongozi wa chama cha wafanyakazi ETUC, Emanuel Bonaciana amesema kuwa "nia ya maandamano ni kuwataka  viongozi kuja na njia mbadala ya kukuza uchumi kwa kuwekeza na ajira iliyo sawa na haki kwa wote."

Hali ya mbinyo wa matumizi na uwekezaji, umeleta hali ya mstuko kwa wananchi wa nchi za jumuiya ya Ulaya na kulaumu kuwa hali ya maisha imekuwa ngumu kwa walio wengi na wachache ndiyo wanaoifaidika na mpango huo  na hasa mabenki.

Matumizi ya mtandao yatonesha kidondo cha Marekani na Kuba.



Havana Kuba 04/04/2014.  Serikali ya Kuba imeilalamikia Marekani kwa kutumia mtandano unao fanya kazi kama  Twita ili kuaandaa mapinduzi nchini Kuba.

Msemaji wa serikali ya Kuba alisema kuwa mtandaa huo ambao una matumizi sawa na twita ulikuwa unalengo la kuhimiza wananchi wa Kuba kupingana na "serikali ya Kuba kwa kuwa ni ya kikomunisti"

Hata hivyo serikali ya Marekani imepinga kuhusika na njama hizo zakuhimiza wananchi wa Kuba kupingana na serikali yao, bali Marekani imekubali kuwepo na mtandao huo kama twita ambao ulikuwana madhumini ya kuwasaidia wa Kuba katika mawasiliano na ujenzi wa demokrasia.

Msemaji wa serikali ya Marekani Marie Harf amesema kuwa "hii siyo siri kwani mradi huo ulikuwa na nia ya kuweka uwazi ukuzaji wa demokrasia na ulikuwa wa miaka mitatu ambapo ulighalimu dola za $1.2 millioni na ulipitia na kudhaminiwa kwa kutumia wakala tofauti"

" Na hatukusambaza maswala ya kisiasa" Alimaliza Marie Harf.

Hata hivyo shirika la habari la AP limeripoti kwa kusema " mradi huu ulibuniwa kuzunguka vikwazo vya kimtandao vilivyo wekwa na serikali ya Kuba kwa kutumia makampunu yenye ubia na shell chini ya uongozi wa USAID shirika ambalo huwa linatoa misaada kwa masikini duniani"

Mzozo wa Kuba na Marekani ni wamuda na kuwa ni moja ya mzozo baridi ambao unaanzia 1962 na kupelekea Marekani kuwa na vikwazo na Kuba tangu kipindi hicho.

Wapalestina na Waizrael wampa kichwa kuuma John Kerry.

Rabat, Moroko - 04/04/2014. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani amesema kuwa kuna nia kubwa ya kuendeleza mazungumzo ya amani ya kati ya Waizrael na  Wapalestina japo kwa sasa  kuna ugumu umejitokeza.

Waziri John Kerry aliyaongea hayo mjini Rabat Moroko, kwa kusema kuwa "hali ya mazungumzo yakuleta amani kati ya Waizrael na Wapalestina inahitaji kuangaliwa kwa njia zote za umakini kwa kuzingatia kwa sasa pande zote mbili simechukua hatua ambazo zinaleta ugumu wa kuendeleza mazungumzo ya kuleta amani."

Kutamka kwa waziri John Kerry kuhusu ugumu wa mazungumzo ya kuleta amani kati ya Wapalestina na Waizrael kumekuja baada ya Uingozi wa Wapalestina  kusaini kwa pamoja kutaka kujulikana kama taifa , ambapo hapo awali ilikuwa ni moja ya makubaliano yaliyowekwa katika ya Izrael na Palestina.

Uongozi wa Palestina pia  umedai "Izrael imevunja mkataba wa makubaliano wa kuwaachi huru wafungwa wa Kipalestina waliopo katika jela za Kiizrael na kusitishwa kwa utanuzi wa ujenzi wa makazi ya Waizrael katika maeneo ya Wapalestina."

Hata hivyo kwa mijibu wa wachunguzi wa maswala ya amani ya mashariki ya kati wanadai kuwa kama "Kama serikali ya Izrael ingekubali kuaachia wafungwa wa Kipalestina, basi kungesababisha kuvunjika kwa serikali ya waziri mkuu Benyamin Netanyahu, jambo ambalo waziri Netanyahu limemletea ugumu kutimiza ahaadi ya kuwaachia wafungwa hao wa Kipalestina."

Mpango wa kuleta amani kati ya Wapalestina na Waizrael umekuwa nawakati mgumu kwa muda mrefu  kwa serikali ya Marekani, jambo jitihada zimekuwa zikifanyika kwa hali na mali ili amani iwepo kati ya Wapalestina na Waizrael.

No comments: