Tuesday, April 8, 2014

Mwanajeshi wa Ufaransa atia chumvi kidonda cha kuhusika na mauaji ya Rwanda 1994.

Mwanajeshi wa Ufaransa atia chumvi kidonda cha kuhusika na mauaji ya Rwanda 1994.



Paris, Ufaransa - 08/04/2014. Mmoja wa makamanda waliokuwa katika kikosi cha kijeshi cha Ufaransa kilichokuwa nchi Rwanda wakati wa mauaji wa kimbari ametoa changamoto kwa serikali jiji Paris juu shutuma kutoka kwa serikali ya Rwanda.

Guillaume Ancel ambaye alikuwa kapteni  katika jeshi la Ufaransa jiji Kigali mwaka 1994 kabla  mauaji ya kimbari kuanza amesema '' niliamliwa kupakia siraha katika roli ili ziende Zaire au kwa sasa Kongo DRC na zilikuwa kwa ajili ya askari wa Rwanda ambao watakimbia na ndiyo walikuwa wahusika katika mauaji ya kimbari''

''Pia nilishauriwa kuhakikisha waandishi wa habari wasijue, na nilipo pinga swala hili niliambiwa kuwa ikiwa kama hatutashirikiana na jeshi la Rwanda la wakati hule, basi watatugeuka na tutakuwa katika hali ya mvutano nao.''

''Na hii ilitokea baada ya mauaji ya kimbari ya 7/April/1994 na  ndege iliyombeba rais  wa Rwanda Juvenal Habyalimana kuangushwa katika kiwanja cha ndege cha Kigali.''

''Kwangu nilishangaa kwa  kutokuelewa kuwepo kwa jeshi la Ufaransa kwani tayari jeshi la Umoja wa Mataifa UNAMIR lilikuwa tayari mjini Kigali.'' Aliongezea Ancel.

Tangu kutokea mauaji ya kimbari  ya mwaka 1994 nchini Rwanda, serikali ya  Rwanda chini ya rais Paul Kagame imekuwa ikizishutumu Ufaransa na Ubeligiji kwa kuhusika katika mauaji ya kimbari, ambapo watu baadhi ya watu wenye itikadi kali toka jamii ya Kihutu  waliwaua watu 800,000 wa jamii ya Kitutsi na huku waangalizi  wa umoja wa mataifa wakiwa wapo na butwaa.

No comments: