Monday, September 1, 2014

Urusi yapata jibu la kitendawili kutoka EU.

Joto la Urusi la iweka NATO mkao wa chonjo.

Brusells, Ubeligiji - 01/09/2014. Muungano wa kijeshi wa kujihami wa NATO, umetangaza rasmi kuunda kikosi maalumu cha kijeshi ndani ya jeshi hilo ili kuweza kupambana na vitisho kutoka Urusi.

Akiongea, katibu mkuu wa muungano wa NATO, Anders Fogh Rasmussen amesema '' NATO imeshaa andaa kikosi cha wanajeshi 4,000 ambao watakuwa na kazi maarumu ya kukabiliana na vitisho kutoka kwa Urusi na vitisho vingine vitakavyo onekana kuhatarisha nchi wanachama wa NATO.''

'' Kikosi hiki kimeundwa baada  yali halisi ya Ukraini, kwani hali hii inatisha, NATO imeona haja ya kuunda kikosi  hiki maalumu, ambacho kitakuwa na uwezo wa kuwa tayari kwa muda wa masaa 48, na hivyo mkutano wakuu wa nchi wanachama utakao fanyika mjini Newport Weles ndiyo utakao idhinisha kikosi hicho.''

Kuundwa kwa kikosi hicho maalumu cha NATO na ambacho  kitakuwa  kikuzunguka katika nchi za Baltik kimakazi,  kumetiliwa mashaka na wataalamu wa masuala ya ulinzi wa kimataifa kwa kudai kuwa  ''kunaweza vuruga makubaliano ya mwaka 1997 ambapo NATO na Urusi zilikubaliana kuwa hakutakuwepo na kambi ya NATO katika maeneo ya nchi za Baltik.''

Habari za ndani za NATO zinasema ''wanajeshi hao 4,000 hawa takuwa ni  sehemu ya wanajeshi 10,000 ambao Uingereza ilipendekeza hapo awali.

Mkutano wa wakuu wa nchi za NATO unatarajiwa kuaanza siku ya Alkhamisi wiki hii ambapo utatawaliwa na hali ya  Afghanistan baada ya NATO kuondoa majeshi yake nchini humo na pia wimbi la vita vya Ukraini

Ujerumani yabadiri mwelekeo wa mambo yake ya kigeni.

Berlin, Ujerumani - 01/09/2014. Ujerumani imekubali kuwa imesha peleka siraha  nchini Irak ilikusaidia serikali ya Wakurdishi katika kupambana na kundi la ISI ambalo limekuwa likipambana na serikali  kuu ya Irak kivita.

Akilihutubia bunge la Ujerumani, Kansela Angela Merkel alisema ''Kundi la ISIS, ni kundi ambalo ni hatari sana, na inabidi kukabiliana nalo kwa hali na mali, nikundi la kigaidi ambalo linatishia, usalama  wa Wajerumani na Ulaya kwa ujumla.''

''Kama kundi hili likiachiwa litafika Ulaya hadi Ujerumani na siraha walizo nao  watazitumia katika kuhatarisha usalama wa raia wa Ulaya kwa kuendeleza ugaidi, na ndomaana Ujerumani imeamua kuisaidiana na serikali ya Wakurdi ili kulitokomeza kundi hili la ISI.''

Siraha ambazo Ujerumani imezipeleka nchini Irak ni, G3 16,000, G36 Raifo, Siraha za kuzua mabomu ya kulipua vifazu 30, roketi 240, na mabomu ya mkono 10,000.

Kansela Angela Merkel, ilielezea uamuzi huo wa serikali, baada ya vyombo vya habari kutangaza kuwa Ujerumani imesha peleka vifaa vya kivita nchi Irak katika jimbo la Wakurdishi ili wazitumie katika kupambana na kundi la ISI.

Uamuzi huo wa serikali ya Kansela Angela Merkel, ulmeshutumiwa na baadhi ya Wajerumani ambao wanapinga kitendo cha Ujerumani kushiriki katika vita au kutoa msaada wa vyombo vya kivita kwa kuamini unakwenda kinyume na maamuzi ya kihistoria ya Wajerumani.

Lakini hata hivyo, Wajerumani wengine wamekuwa wakiunga mkono uamuzi huo wa serikali, kwa kusema kuwa lazima Ujerumani sasa ibadirike na iwe kipao mbele katika masuala ya kigeni.

Urusi yapata jibu la kitendawili kutoka EU.

Moscow, Urusi - 01/09/2014. Viongozi wa China na Urusi wamefungua rasmi ujenzi wa bomba la gesi ambalo litatumika kusafririshia gesi kutoka Urusi kueleke nchini China.

Akifungua ujenzi huo, rais wa Urusi Vladmir Putin,alisema '' hili bomba la kupitishia gesi, likikalimilika lita saidia katika kukuza uchumi wa nchi, hasa kwa nchi za Asia-Pasifiki na kutakuwa na uhakika wa kuuuza zao la gesi bila matatizo.''

'' Makubaliano haya na  China yamekuja kutokana na umakini tunaokuwanao katika masuala ya mahusiano katika masuala ya kigeni, na China ni rafiki mkubwa wa Urusi na  siku zote tumekuwa hatuna vipingamizi kati yetu.''

Bomba ilio ambalo litakuwa na urefu wa  kilomita 3,968 na kupitia Siberia na linatarajiwa kuwa kubwa na lenye urefu kuliko mabomba  yote duniani la litasafirisha gesi yenye ujazo wa meta tillion 4 kwa muda wa miaka 30 na bomba hilo la gesi litamilikiwa na shirika la nishati Gazprom la Urusi.

Kuanza kwa ujenzi wa bomba hili la gesi kuelekea China, kutaifanya Urusi na ambao utakamilika 2018 utaleta unafuu, kwani Urusi  imekuwa ikivutana na nchi za jumuiya ya Ulaya katika suala la zao la gesi, na hasa tangu kuzuka kwa mchafuko wa siasa nchini Ukraini

No comments: