Monday, December 22, 2014

Muhammad Ali alazwa hospitalin.


Obama alaani mauaji ya Polisi.



New York, Marekani - 21/12/2014. Rais wa Marekani Barack Obama amelaani mauaji ya polisi wawili katika jiji la New York, ambao walikuwa wakishika doria ndani ya gari lao. 

Kamishna wa polisi wa New York Bill Bratton, amesema "Ismaaiyl Brinsley, mwenye umri wa miaka 28, aliwapiga risasi kichwani polisi hao bila kuwepo onyo lolote. Na kabla ya hapo Brinsley ambaye anaasili ya kiafrika, alimpiga risasi mchumba wake wazami kabla ya kuwauwa  polisi hayo wa mji wa Brookyl."

Mauaji ya polisi hao wawili, yametoke,  wiki chache baada ya  maandamano ya watu wenye hasira, kupinga vitendo vya polisi kuhusika na matukio ya polisi kuwauwa watu weusi ambao hawakuwa na silaha. 

Ismail Brinsley alijiua mwenyewe kwa risasi baada ya kukimbilia kwenye kituo cha treni zinazopita chini ya ardhi. 

Polisi imesema alikuwa ameweka ujumbe kwenye mtandao wa wake kuwa alipanga kuwauwa "nguruwe" wawili kama hatua ya kulipiza kisasi kifo cha Eric Garner, Mmarekani mweusi aliyeuawa kwa kukabwa koo na polisi.

 Rais wa Misri amfuta kazi Mkuu wa ujasusi

Kairo Misri - 21/12/2014. Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi leo amemfukuza kazi mkuu wa upelelezi  Jenerali Mohamed Farid el- Tohamy aliyeteuliwa siku chache tu baada ya kuondolewa madarakani rais wa zamani Mohamed Mursi mwezi Julai mwaka jana. 

Jenerali Khaled Mahmoud Fuad Fawzy ambaye alikuwa msaidizi wa Farid el Tohany ndiye aliyeteuliwa kuchukua nafasi yake. 

Hata hivyo hakuna sababu zozote zilizo elezwa za kufukuzwa kazi kwa Jenera Farid el 
Tohan.

Wakati huo huo, Misri leo imekifungua  mpaka wa Rafah, ambao utawawezesha  wakazi wa Ukanda wa Gaza, kwa mara ya kwanza katika kipindi cha karibu miwezi miwili kuweza kuingia na  kutoka Misri. 

Misri ilifunga mpaka wa kuingia Gaza, Oktoba 25 baada ya wanamgambo wenye itikadi kali za Kiislamu katika eneo la Sinai kuwauwa wanajeshi wake 33.




Marekani  kuchunguza uvamizi wa mtandao wa Sony.


Marekani ,Washington -21/12/2014 Rais wa Marekani Mabaka Obama, amesema kuwa Marekani inachunguza ili kuweza kujua kama Korea ya Kaskazini inahusika na ushambuliaji wa mtandao wa Sony, na kama ikigundulika ilihusika, basi hatua za kisheria zitachukuliwa.

Obama alisema, "tunalianagalia hili  suala la kushambuliwa kwa Kampuni ya Sony kwa makini, nakuwa kila sheria ya kukabiliana na jambo hili zipo tiyari.

"Kwani hatufanyi maamuzi kwa kupitia vyombo vya habari, bali ukweli utakapo patikana basi sheria zitafuata."

Mazungumzo hayo ya rais Obama yamekuja  baada ya Korea ya Kaskazini kukanusha kuhusika na mashambulizi ya kimtandao kwa kampuni ya Sony, na kuitaka  Marekani  kuonyesha ushirikino ili kulitafutia ukweli suala la uvamiaji wa mtandao wa kampuni ya Sony.  


Muhammad Ali alazwa hospitalini.

 

Kentaki, Marekani - 21/12/2014. Aliyekuwa bingwa  ndondi kwa uzito wa juu duniani Muhammad Ali  mwenye miaka 72, amelazwa katika hospitali ya mji wa Loiseville ili kutibiwa  homa ya mapafu. 

Bob Gunnell, ambaye ni msemaji wa Ali, alisema " Ali anatibiwa na kundi la madaktari wake na yuko anaendelea vyema.

Mohammed Ali, ameshakuwa hospitali kwa siku moja na anatarajiwa kuruhusuhusiwa kutoka hopitalini baada ya Madaktari kulidhika na mwenendo wa afya yake .



 


 


 

No comments: