Nchi za
Africa zatakiwa kushirikiana na mahakama ya ICC.
Akiongea katika ufunguzi huo rais mpya wa Baraza la
mataifa wanachama wa ICC, Sidiki Kaba, ambaye ni Waziri wa sheria wa Senegal,Alisema " Naomba kuwepo na ushirikiano barani Afrika, ili kubadili mawazo potofu yanayo
haribu mahakama hiyo ya ICC.
"Nana penda kusisitiza kwamba malalamiko ya nchi wanachama yanapaswa kusikilizwa, na kutafutiwa ufumbuzi." Aliongeza Kaba.
Mkutano huo ambao unajumuisha nchi wanachama 122, Pia
uliudhuliwa na wajumbe kutoka Palestina ambapo walikubaliwa rasmi kuwa
waangalizi katika mkutano.
Na kwa mujibu wa Mahakamaya ICC uamuzi huo wa kuruhusu kuwepo kwa Wapalestina
ni hatua moja muhimu ambayo inafungua njia kwa Wapalestina kujiunga kama mwanachama kamili wa mahaka hiyo
ya uhalifu ya kimataifa.
Liberia
yasifiwa na Ban Ki-moon zidi vita vya Ebola.
Hii
itakuwa ni mara ya pili kwa Ban Ki-moon kutembelea Liberia, tangu ugonjwa wa
Ebola ulipozuka ambao hadi sasa umeshaua watu zaidi ya 7000 katika eneo zima la
Afrika ya Magharibi.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema kuwa Mogherini atakutana na kufanya mazungumzo na Waziri mkuu Haider Al-Abadi, na baadaye siku ya Jumanne atakuwa na mazungumzo na rais wa jimbo la Kurdi, Masoud Barzani katika mji wa Irbil.
Ziara hiyo za Mogherini itakuwa na madhumuni ya kuona ni kwa jinsi gani Umoja wa Ulaya, utasaidia katika kupambana na kundi na dola la Kiislaam , ambapo hadi sasa Umoja wa Ulaya umeshatoa euro milioni 20 kusaidia kutatua matatizo ya kiutu ambayo yamesababishwa na kundi hilo wapiganaji wa IS wanaoshikiria maeneo kadhaa nchini Iraq.
Waziri Frank Walter Steinmeier aonya kuhusu Urusi.
Waziri wa mambo ya nje ya nchi wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier,ameleezea wasiwasi wake kuhusu msukumo uliyopo wa vikwazo kutoka kwa nchi wanachama wa nchi za umoja wa Ulaya kuwa hutahatarisha na kuiyumbisha Urusi, ambapo wimbi lake litaleta mtikiso katika bara la Ulaya.
Walter Steinmeier alisema kuwa, kushuka kwa tahamni ya Lubo, fedha inayo tumika Urusi, hakutakuwa na faida kwa nchi za Ulaya, hivyo ni bora kuwepo na uangalizi katika sheria za kuweka vikwazo kwa Urusi.
Mazungumzo hayo ya Steinmeier, yamekuja baada kikao cha wakuu wanchi za jumuiya ya Ulaya, kuionya Urusi kuwa kama haitabadiri msimamo wake dhidi ya Ukraine, nchi za Umoja wa Ulaya hazita sita kuongeza vikwazo zidi ya Urusi.
No comments:
Post a Comment