Tuesday, December 30, 2014

Talibani waikejeli NATO.

Wapalestina wawakilisha muswaada wao uhuru umoja wa Mataifa

New York, Marekani - 29/12/2014. Jumuiya ya nchi za muungano wa Kiarabu, zimekubaliana kwa pamoja muswaada uliyo letwa na serikali ya Wapelestina kwenye umoja wa mataifa, ambao unataka Izrael kusitisha vitendo vyake vya kuchukua ardhi ya Wapalestina kinguvu, na kutoka katika maeneno yoye iliyo yachukua kinguvu ifikapo 2017, jambo ambalo Marekani na Izrael zimepinga.

"Ni suala la kuwaunga mkono Wapalestina ni muhimu, na ndio maana nchi za muungano wa nchi za Kiarabu zimeunga mkono muswaadahuo.
Alisema balozi wa Dina Kawar, ambaye ni balozi wa Jordani wa Umoja wa Mataifa.

"Kutakuwa na mazungumzo na wajumbe wa Palestina, nini kifanyike na lini kura zipigwe, ili kupitisha muswaada huo." aliongezea Kawar

Muswaada huo wa Wapalestina, ulipingwa na Marekani na Izrael, kwa madai kuwa hauelezei kuhusu hali ya Amani ya Izrael.

Hata hivyo wajumbe wa Palestina wamesema kuwa katika muswaada huo, lipo suala la majadiliano ya miji ya West Bank, Mashariki ya Jerusalem na Ukanda wa Gaza, miji ambayo michoro yake ya kiramani ilibadirika baada ya vita vya Mashariki ya Kati vya 1967.

Hatung'oi buti nchini Sudani ya Kusini, asema raia Museven.

Kampala, Uganda - 29/12.2014. Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Mseven, amesema kuwa jeshi la Uganda litaondoka nchini Sudani ya Kusini pindipo Amani ya kudumu itakapo patikana.

Akiongea kuhusu hali ya Amani ya Sudani ya Kusini, rais Museven alimeam, "tatizo si la  Uganda, tatizo ni Amani ya kudumu inayo takiwa nchini Sudani ya Kusini.

Kunatakiwa hali ya utulivu na Amani iwepo, kwani jeshi la Uganda haliwezi ondoka na kuachia mwanya wa vurugu kurudia.

Serikali ya Uganda iliamua kupeleka jeshi lake nchini Sudan ya Kusini, baada ya kutokea mvutano wa madaraka kati ya rais Salva Kiir na makamu wake Riek Machar, jambo ambalo lilileta kuvurugika kwa Amani.

Hata hivyo Riek Machar, amekuwa akidai kuwa jeshi la Uganda linatakiwa kuondoka nchini Sudani ya Kusini,kwa kuhisi kuwa lina unga mkono utawala wa SPLM uliopo chini ya raia Salva Kiir.

Talibani waikejeli NATO.

 
Kabul, Afghanistani - 29/12.2014. Kundi la Taliban la Afghanistan limekejeli  kuondoka kwa NATO ni dalili ya kushindwa kwao, na kwamba kundi hilo ndilo lililo ibuka na ushndi, baada ya kampeni ya kivita iliyochukua miaka 13.

"NATO na washiriki wake wamekunja bendera katika mazingira ya kushindwa, na kukabidhi madaraka ya kiulinzi kwa serikali ya Afghanistan, ni jibu kuwa Taliban wameshinda, kwani mpaka leo sisi bado tupo. Alisema msemaji wa Taliban Zabihulla Mujahid.

"Na Kuanzia sasa Taliban itashika usukani, na wale waliofikiliwa kuachiwa madaraka watashughulikiwa kama tulivyo lishughulikia jeshi la NATO na washirikia wake na sasa wanakimbia." Aliongezea  Mujahid.

Vita zidi ya kundi la Taliban vilianza mwaka 2001, vikiwa na madhumuni ya kuungamiza utawala wa Taliban, na kusababisha vifo wanajeshi karibu 3,500, na pia kuleta hasara kijamii nchini Afghanistan na watu wengi kupoteza maisha yao.

 

No comments: