Tuesday, December 30, 2014

Marekani yataka nguvu za kijeshi kutumika nchini JD Kongo.
 

Kinshasa, JD ya Kongo - 30/12/2014. Wanajeshi wa umoja wa mataifa waliopo nchini JD Kongo, wametakiwa kutumia nguvu za kijeshi, ikiwa kundi la apiganaji wa DFLR ( Democratic Force for the Liberation of Rwanda) litashidwa kusalimisha siraha walizo nazo itakapofikia January 2.

Russ Feingold, ambaye ni mwakilishi wa Marekani katika ukanda wa Maziwa makuu amesema "
"Ikiwa kutatokea ucheleweshaji wa kukabidhisha siraha, kundi la DFLR ndilo litakalo faidika, huenda wakazitumia siraha hizo katika ukiukaji wa haki za binadamu. 

"Hivyo  jeshi la umonja wa mataifa - MUNUSCO, lipo tayari pindipo hili nilisemalo litatokea ili kukabiliana na kundi hilo, na napenda hili lieleweke kuwa nguvu za kijeshi zitatumika."

 Kundi la DFLR ambalo ni la Wahutu wenye mlengo mkali na wanaopingana na serikali ya Kigali, wamekuwa wakishutumiwa kwa kuhusika na ukiukwaji wa haki za binadamu na inaaminika bado kuna wapiganaji 1400  ambo bado wanashirikiria siraha zao.

 Iran yadai haita buruzwa katika mazungumzo ya kinyulia.
Tehran, Iran - 30/12/2014. Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Mohammad Javad Zalif, amesemakuwa Iran itasimama imara katika majadiliano yake kinyuklia  yatakayo anza 15/01/2015.

Akiongea Javad Zalif alisema " bado kuna upana ambao unatakiwa kipunguzwa katika mazungumzo hayo. Hatupo tayari kusukumwa sukumwa.

"Tutakuwa Imara kama mwanzo na la muhimu ni kuhakikisha vikwazo vyote vinaondolewa kama tulivyo sema hapo awali. Nakama hakutakuwa na makubaliano, Iran ipo tayari kwa hali na mali kukabiliana na lolote litakalotokeo."

Mazungumzo hayo ya Iran na mpango wake wa kuendelea na muzalisha nyuklia yanangojewa, kwani matokeo ya katika mkutano huo yanaweza badirisha sura ya dunia katika ulimwengu wa kinyuklia.
 
Mazungumzo ya kinyuklia ya Iran  yanajulikana kamaya nchi 5+1 ambayo yanajumuisha Urusi, Marekani, China, Unigereza na Ufaransa. 

Uingereza kupingwa muswaada wa Wapelestina UN.
New York, Marekani - 30/12.2014. Uingereza imetamka kuwa itapinga muswaada wa Wapalestina  walio uwakilisha umoja wa mataifa, ambao unaitaka Izrael kusimamisha chukuaji wake wa ardhi ya Wapelestina kinguu, na kurudisha maeneo yote wanayo miliki Waizrael.

Mark Lyall, ambaye ni balozi wa Uingereza wa Umoja wa mataifa ameseama kuwa " jibu la Uingereza ni hapana kwa muswaada huo.

"Kwani lugha ambayo imetumika inaleta walakini, hasa kuongezeka kwa lugha ya wakimbizi, na hivyo kunaugumu katika sualazima la hali hiyo."

Matamshi hayo ya Uingereza, yamekuja baada ya hapo awali Marekani kutamka kuwa inapinga muswaada huo wa Wapalestina kwa kuwa haukuelezakuhusu usalama wa Izrael

Muswaada wa Wapalestina umekuwa ukipigiwa chepuo na Jordan, ambapo  inataka kura ya kupitisha muswaada huo ipigwe siku ya Alhamis, jambo ambalo kwa sasa linaelekea kuwa na ugumu. Kwani Uingereza na Marekani zaweza tumia kura zao za vito kupinga muswaada huu.
 


No comments: