Thursday, December 18, 2014

Uimara wetu ndio kitisho kwa wapinzani asema rais Vladmir Putin.

Wabunge nchi Kenya watwangana.

Nairobi, Kenya - 18/12/2014. Wabunge nchini Kenya, wametwangana na kutupiana usoni nyaraka zilizo andikwa muswaada  wa kiulinzi na kiusalama kwa madai kuwa unakwenda kinyume na haki za wananchi Wakenya.

Vurugu hiyo ambayo ilianzishwa na wabunge wa kundi la upinzani, kwa kudai kuwa kupitishwa kwa muswaaada huo, kutafanya nchi ya Kenya kuwa taifa la kipolisi.

"Muswaada huu utafanya uhuru wa Wakenya kuwa hatarini, na watakao faidika ni matajiri ambao wapo na karibu na serikali tawala ya Jubilee."  Alisema Moses Wetangula, kiongozi wa wabunge wapinzani.

Sheria hii iliyopitishwa, imewapa uwezo maafisa usalama kuwa na uwezo wa kuwaweka kizuizini washukuwa wa ugaidi kwa kipindi cha mwaka mmoja, kurekodi mawasiliano na kufatilia nyendo za uandishi wa habari na pia kuwawekea vizuizi katika kazi zao za kiandishi.

 Muswaada huo wa kiusalama na kiulinzi, umepitishwa kutokana na kuongezeka kwa mashambuliz ya kigaidi nchini Kenya kutoka kwa kundi la Alshabab ambalo ni mkondo wa kundi mama la Alqaeda.

 Uimara wetu ndio kitisho kwa wapinzani asema raia Putin.

Moscow, Urusi - 18/12/2014. Rais Vladmir Putin, ametangaza kuwa kushuka kwa thamani Lubo, fedha ambayo inatumika nchini Urusi, kunasababishwa na  myumbo wa uchumi wa kimataifa na kuwa uchumi wa nchi hiyo utakuwa imara baada ya miaka miwili.

Akionya rais Putini alisema "Japo vikwazo vilivyo wekwa na nchi za Ulaya na Washiriki wake vinachangia, Urusi kama taifa tutaweza imarisha uchumi wetu na tupo imara hakuna wa kututishia wala wa kutuyumbisha."

Kuhusu suaa la Ukraine na Crimea, rais Putin amehaidi kuwa Urusi haita yumbishwa na itabaki na msimamo wake ambao iliiuweka toka awali.

Kwenye mkutano huo wa Rais Putin, waandishi wa habari 1200 waliudhuria. Na ni wa kwanza  kwa tangu thamani ya pesa ya nchini hiyo kushuka ghafla katika masoko ya kifedha. Jambo ambalo limesababishwa na kushuka kwa bei ya mafuta, ambayo huwa yanachangia kwa kiasi kikubwa cha uchumi wa Urusi.
  
Wapiganaji wa M23 watoroka kutoka katika kambi ya jeshi nchini Uganda. 

Kampala, Uganda - 18/12/2014.Wapiganaji 1000 wa kundi la M23 waliokuwa katika kambi ya kijeshi ya Bihanga nchini Uganda, wametoroka baada ya ya kudhainia kuwa hali ya usalama wao ni mdogo pindipo watakapo rudishwa nchini JD Kongo.

Akiongelea kuhusu kutoroka huko, Bertrand Bisimwa, ambaye ni mmoja wa viongozi wa kundi la M23, alisema "Wapiganaji hao walikimbia  baada ya kukataa kupanda lori la kijeshi ambalo lilikuwa tayari kuwapeleka uwanja wa ndege ili kuelekea makwao, jambo ambalo lilifanya wanajeshi wa Uganda kufyatua risasi na kuwaumiza baadhi ya wapiganaji wa M23."

Kitendo cha kuwarudisha kwa nguvu wapiganaji wa M23 nchi JDKongo ni kukiuka masharti ya amani yaliyowekwa hapo mwanzo wa makubaliano ya kusimamisha mapigano nchini KOngo."Added Bisimwa.

Hata hivyo msemaji wa wa jeshi la Uganda Kanali Paddy Ankunda, amesema kwa kupitia mtandao wa twitter kuwa jeshi la Uganda lipo linawasaka wapiganaji hao wa M23 ambao wamekimbia.

Kufuatia kukimbia huko kwa wapiganaji 1000 wa M23, kumekuwa ma wasiwasi kuwa huenda wapiganaji hao wakarudi na kujiunga na baadhi ya makundi ambayo bado yanapingana na jeshi la serikali la JC Kongo.



No comments: