Thursday, October 25, 2007

Luck Dube, Mungu akuweke mahali pema peponi. Amina.

Hata Beyonce naye alikuwepo,na wengine wengi tu kwenye Karne mpya. Wakati watu wengine duniani walisha adhimisha kuisha kwa karne ya kale.Lakiniwana Ethiopia walikaribisha karne mpya ya 2000th, kutokana na karenda yao ya asili hivi majuzi. Kati ya hao ni mwana dada Beyonce amabye alifanya vitu vyake kwa masaa mawili, mbele ya watazamaji wasio pungua maelfu mjini Addis Ababa, aliimba nyimbo za zake za zamani na kuimba nyimbo zake za albumu ya B'Day. Mwana dada huyu ambaye amenza maonyesho yake ya kuzunguka dunia kwa kupiga muziki wake, atatembelea nchi kama Russia, Romania,Turkey,India, Indonesia, na China. Hapo juu Beyonceeee, akimwaga vitu vyake mjini Addis Ababa - Ethiopia.

Wapendanao, Pitt na Angelina Jolie wanataka kuja na kitu kipya hewani.
Wana sanaa na wacheza sinema maharufu duniani Pitt na mama Angelina Jolie, wanaanza kuaandaa mchezo wa sinema, au (Drama), ambao utazungumzia maisha ya ndani ya wanasiasa, mashirika ya kimataifa jinsi ya vavyo toa misaada, kazi inayvyo fanywa na wafanyakazi wa mashirika haya.
Kama utakumbuka wapendanao hawa wali cheza kwe sinema ijulikana yao kama Mr and Mrs Smith, amabyo iliwapaita sifa nyingi saanaaaaa tu.
Hapo juu pichani, wapendanao hawa, wakiangaliana kwa jicho la haba, na kuku baliana kwa tabasamu. Habib na habibit Manshalahaah, hakuna kinacho haribika.
Wapenzi wa hudhulia kumwombea hayati Luck Dube kanisani.
Luck Dube Mola akuweke pahali pema peponi
Ndugu,jamaa na marafiki walihudhulia, misa ya mwisho ya kuagana na nyota ya muziki wa regge Afrika, na Afrika ya Kusini hayati Luck Dube, amabaye aliuwawa na majambazi wakati wa kijaribu kunyangaya gari lake.
Hayati Luck Dube, alikuwa akishauri kwa kupitia nyimbo zake, kwamba watu waachane na matendo ya ujangili, rushwa, ukabaji wa aina yoyote na mambo mengine mabaya, na watu wajaribu kuwa wanapendana na kukaa pamoja nchini Afrika ya Kusini.
Kwani zaidi ya watu 20,000 wamepoteza maisha yao kipindi cha miaka ya nyuma nchini humo.
Mmoja wa wapenzi wa muziki wake, alisema "Alikuwa akishauri vizuri,na kupinga vitendo vibaya, na leo hii watu wenye kutenda mabaya ndiyo wamemundoa duniani,"Jamani"
Hayati Luck Dube atazikwa 28/10/07 siku ya jumapili na ndugu na jamaa zake wa karibu, kutokan na msemaji wa familia ya marahemu.
Pichani kulia ni baadhi ya ndugu wa hayati Luck Dube walipoahudhulia maombi kanisani, na kushoto ni picha ya hayati Luck Dube na ujumbe "RESPECT"Luck Dube. Anina
Alpha Blondy, muziki wa wake ni dawa na matumaini kwa walala hoi, na wapiganaji pia.
Nchini, Ivory Coast, hasa mji mkuu Abidjani, muziki wa regge ni dawa yetu,wakati wowote, hasa tunapo kuwa tunapingania haki zetu.Haya yalisemwa na mtummoja ambaye akutaka jina lake litajwe.
Aliongeza kwa kusema hata wanajeshi na askari wana pumzika huwa wana burudika na miziki ya regge hasa ya mwana musiki wa hapa nyumbani Alpha Blondy, kwani huwa anakumbusha mambo mengi na kufundisha jinsi ya kupambana ha hali ya dunia ya sasa.
Pichani juu Alpha Blondy akifanya vitu vyake katiak moja ya maonyesho yake ya muziki wa regge.
Mashindano ya kombe la rugbi la dunia kumbe nayo yamo jamani ?
Ina kadiliwa kiasi cha watazamaji wasiopungua millioni 15 1/2 wali pata huhondo wa kuangalia mibaba yenye miraba minne imenyana ili kutafuta nani zaidi, na nani alikula lishe ya maana tangu akiwa mtoto.
Mvuto huu wa watu kukaa ka kula raha za macho kwenye runinga ( TV), ulielekezwa nchini Ufaransa, wakati wa mashindano ya kombe la dunia la rugbi. Na matokeo yake watoto kutoka bara la Afrika wakatokea kuwa washindi wa mchezo huu wa mwaka 2007
Hapo juu ni wapenzi wa rugbi wakiwa wanajiaandaa kuishangilia timu ya kupitai runinga.
Jina la "Bafana bafana" mmghg. Tafuteni jina linalo lingana na asili yetu " Rais Mbeki"
Rais wa Afrika ya kusini bwana Thabo Mbeki, ameomba timu ya mpira wa miguu ya Afrika ya Kusini, kutafuta jina jingine, badala ya ya la sasa , ninalo julikana kwa wengi ka bafana bafana(The boys the boys), rais Mbeki aliendelea kusema, ya kuwa kwa mantiki na ukweli jina hili alivutii, kwa kuzingatia ya kuwa Afrika ya Kusini ndiyo mwenyeji wa mashindano ya Dunia ya 2010. kama mna kumbuka hapo zamani timu zote za michezo zilitwa kwa jina moja Springboks, lakini sasa kila timu ina jina lake , ukinzia kriketi, na michezo mingine, hivyo haileti maana hata kidogo.
Kuzingatia hoja hii iliyotolewa na rais Mbeki, pia kocha wa zamani wa timu ya taifa ya miguu bwana Jomo Sono, amekubalina na rais, na kuongezea ina bidi itafutwe rangi rasmi ya timu za taifa za mpira wa miguu, kwani zimekuwa zikibadilishwa badilishwa kila mara.
Pichani hapo juu , ni wachezaji wa timu ya taifa ya Afrika ya kusini ndani ya ya Jezi zenye raingi tofauti ya timu ya mpira wa miguu wa taifa la Afrika ya Kusini.
Mashindano ya magari F1 yaingia utata kupatikana mshindi wa kweli. Matumaini kwa Hamilton?
Kim Raikkonen, mkimbizaji wa magari aina ya Ferraris, huenda akwanyang'anywa ushindi wake aaliyo upata havi karibuni nchini Brazil.
Hii yote inatokana na kuwepo kwa mvutano kwa kampuni anayo endesha mwingereza Lewis Hamilton, kampunu nyingine na kampuni ya mbio ya Mc Laren ambayo ndiyo iliyo mtoa mshindi wa mbio hozo mwaka huu bwana Kim.
Kabla ya kumalizika mashindano haya, Lewis Hamilton alitalajiwa kwa mshindi, lakini Hamilton, hakuweza kushinda, hasa baada ya kupoteza mashindano ya magari ya Asia bila kutarajiwa. Hata hivyo wapenzi wake Hamilton wakawa na matumaini atafanaya vizuri nchini Brazil,lakini ikaja kinyume, kwa kushindwa bwana Lewis Hamilton na mpinzani wake mkubwa bwana Kim. Pichani hapo juu, Kim Raikkonen na mwenzake Jean Todt wakipongezana, baada ya ushindi wa Brazil.

No comments: