Saturday, October 20, 2007

Kabla ya Mandela, alikuwepo Julius Nyerere, mpigania haki za waafrika.

Maaelfu wamzika mfalme wa ragge nchi Afrika ya Kusini. Hayati Luck Dube enzi za uhai wake, akiwa jukwaani. Wakati mwanamuziki anapo imba nyimbo, watu hukaa na kusikiliza, anamaana gani? hapo yanapo tokea, ndipo tunakumbuka yaliongelewa na mwanamusiki huyu. Mwana muziki wa rege wa Afrika na Dunia nzima kutoka Afrika ya Kusini amefariki dunia, baada ya kupigwa risasi wakati wa majaribu ya kutaka kuiba gari lake, nje kidogo ya jiji la Johannesburg. Luck Dube aliyekuwa na miaka 43, alikutana na majambazi hayo pembeni mwanyumba ya kaka yake, alipo kuwa amekwenda kutembe. majambazi hayo yalimpiga risasi baada ya Luck Dube kushusha watoto wake kutoka kwenye gari aliyo kuwa akiendesha. Mauaji hayo yalitokea mbele ya kijana wake wa kiume, ambaye ameshikwa na mshituko mkubwa. Kutokana na msemaji wa polisi , watoto ni wazima hawakuumizwa na majambazi haya. Kifo cha Dube kimeshutusha watu wengi,dunia nzima na hasa wapenzi wa muziki wa rege. Rambirambi zinazidi miminika, kwa ukoo wake na familia kwa ujumla. Hayati, Luck Dube akiwa amepiga picha katika moja ya albumu ya nyimbo zake alizo toa enzi za uhai wake na kupendwa saana duniani kote. Wana soka wa Afrika, huru kucheza Uispania kufuatia mkataba wa Catonou - Benin"

Samweli Eto'o apata uraia wa Uispania. Na wati huu habari za kufurahisha kwa wana soka wa Afrika wanaotaka kucheza soka nchini Uispania karibuni

Wachezaji wa kabumbu kutoka Afrika wapo huru kucheza mapira nchini Uispania, bila matatizo yoyote,kama raia mwingine wa Ulaya ya Magharibi. Hii ina tokana na mkataba wa makubaliano uulio sainiwa 2000 Benin Catonou, kupitishwa na kukubalika na chama champira cha Uispania. Mkataba huu unazijumuisha nchi zisizo pungua 77 za Afrika na Carribeani. Hapa anaonekana mwana soka maili kutoka Afrika Samweli Etoo aki fanya vitu vyake ndani ya jezi ya timu yake Barca iliyopo Uispania. Kabla ya Mandela, alikuwepo Julius Nyerere, mpigania haki za waafrika. Ucheshi na tabasamu la mwalimu, lilionyesha utu wake kwa watu wengine. Mwalimu anapo elezea kitu alikuwa makini Afrika imeondokewa na viongozi waliokuwa na mapenzi ya waafrika na Afrika kwa ujumla. Haya ni maneno ya mzee mmoja,ambaye anaeleza haya kutokana na mtazamo wake. Kama nchii Tanzania bila rais wake wa kwanza hayati Julius Nyerere, asinge kuwa na mapenzi na watu wake, basi hii amani inge kuwa ndoto. Nyerere alikuwapepo kabla ya Mandela, na dunia nzima inajua Julius ni nani kwa kuwapa ukweli mabepari. Haya yaliongewa wakati Tanzania, Afrika na Dunia kwa ujumla inadhimisha kumbukumbu ya siku 14/Okt/1999,aliyo aga dunia rais wa kwanza wa Tanzania bwana Julia Kamabarage Nyerere. Hayati Julius Nyerere, alikuwa mstari wa mbele kutete haki za wanyonge, kupiganai uhuru wa bara zima la Afrika, na alichangi kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa usawa nchini Afrika ya Kusini, Uhuru wa Zimbabwe ,Mozambiki,na kusini mwa afrika kwa ujumla Mungu aiweke roha yake peponi 'Amina'
Burkina Faso, ya mkumbuka "Che Guevara wa Afrika" Kapteni Thomas Sankara
Wanachi wa Burkina Faso wanaadhimisha kifo cha aliyekuwa Che Guevara wa Afrika, rais wa ( Kapteni) Thomas Sankara, amabaye aliuwawa wakati wa mapinduzi ya nchii hiyo 1987.
Wapenzi na wanaomkubali marehemu Sankara, walimpoke mke wa hayati Thomas Sankara kwa shangwe alipo wasili mjini Ouagadouguo, kuhudhulia maadhimisho hayo.
Bwana,Thomas Sankara alikuwa mstri wa mbele kutete wanyonge na haki za wanawake, na alisaidia kuinua hali za wanawake nchini mwake , wakati wa kipindi cha utawala wake.
Pichani anaonekana hayati bwana Thomas Sankara, akifikiria nini la kufanya kuinua maisha ya walala hoi
Muuaji amaliza taifa la Kenya taratibu kwa asilimia 10% kila mwaka.
Halai ina zidi kutisha, kutokana na kuongezeka kwa wagonjwa wa kisukari nchini Kenya, Kutokana na msemaji mmoja wa wizara ya afya amesema wangonjwa wanaongezeka kwa kila mwaka kwa asilimia 3.5%, na hii ni hatari, kwani hapo mwanzoni, watu wazima juu ya miaka 50, ndiyo waliyo kuwa wanaonekana kuathirika na ugonjwa huu wa kisukari.Muaji huyu anamaliza taifa letu bila wanachi kujua, lazima tujiadhali" Msemaji"
Lakini hivi sasa ugonjwa huu upo hata kwa vijana.
Hii ina sababishwa na lishe hafifu, kutokufanya mazoezi japo mara moja kwa wiki aliongezea msemaji huyu.
Ugonjwa huu wa kisukari unachangia vifo vya wananchi nchini Kenya kwa asilimia 10%. alimalizia kwa kusema, msemaji huyu.
Pichani wananchi wakingoja kupima ugonjwa wa kisukari sehemu moja nchini Kenya.
Haya jamani bandugu, mazoezi ni muhimu saana,hata mara moja kwa wiki siyo mbaya.
Kifo cha rais wa zamani wa Rwanda bwana Habyalimana kuchunguzwa.
Serilkali ya Rwanda ya anza uchunguzi, ajali iliyo sababisha kifo cha eliye kuwa rais wa Rwanda bwana Juveneil Habayalimana.
Kifo cha Habayalimana kilipelekea mauaji ya alaiki yaliyo tokea 1994, ambayo ya lisikitisha jumuiya ya kimataifa
Kutokana na msemaji mmoja wa serikali amesema , wanachunguza ajali hii, ambayo inaaminika ndiyo chanzo cha mauaji haya yakutisha katika eneo la Afrika ya mashariki na kati,tangu kuondoka wakoloni.
Tunajenga Rwanda, kwa kila Mrwanda, na maendeleo ni yetu sote. "Rais Paul Kagame"
Bado nipo naendelea na matibabu, muda nitarudi kazini kama kawaida rais wa Kuba.
Rais wa Kuba bwana Fidel Castroa, hivi majuzi aliongea, na wanainchi wa Kuba, nakuezea ya kuwa bado anaendelea vizuri.
Mmoja ya watu waliokuja kumtembelea ni rafiki yake mkubwa na kipenzi rais wa Venezula, bwana Hugo Chavez.
Habari kutoka kwa watu wakaribu wa maris hawa, ni kwamba bwana Castro anaendelea vizuri na matibabu, na muda simrefu atakuwa tayari kuendelea na kazi za kila siku.
Kwa wale wanao wapenda viongozi hawa , huwa wana sema siku zote, Viva la Castro, viva la Chavez
Hapa pichani, anaonekana rais Castro akimkaribisha rais wa Venezuela Hugo Chavez, alipo kuja kumtembelea kujua hali yake. Blair nahisi kama bado tupo miaaka ile ya urubaini na saba.
Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza, bwana Toni
Blair, ameomba dunia itafute kila mbinu kupapambana na waislamu wenye itikadi kali,kwani ni tishiao kwa jumuia ya kimataifa.
Bwana Blair aliyaongea hayo hivi karibuni mjini New York, aliendelea kwa kusema, wakati mwingine nahisi kama bado, tupo kwe kipindi cha miaka ya arubaini, kabla ya vita vya pili vya duniani
Kwani kipindi hicho wale wa NAZI walisumbua saana. Hivyo lazima tukabiliane na hali hii ya itikadi kali.
Pichani anaonekana bwana Blair akisisitiza umuhimu wa kupambana na itikadi kali.
Wanunuzi wa madini watakiwa kuwasaidia wenyeji.
Uongozi wa moja ya kampuni kubwa ya kuchimba na kuuza almasi De Beers Group ambato ina asilimia 40% ya uchimbaji na uuzaji, imeziomba nchi amabazo ni wanunuzi na wanaosaidia kupatikana kwa almasi, zisaidie bara la Afrika, kwani ndiyo, bara pekee linalo toa almasi na madini mengine kwa wingi duniani.
Moja ya nchi hizo zilizo tajwa ni USA , Israel na nchi za Ulaya ya magharibi. Pichani, ina oneka ulimbwende na nakshi hii ikiwa kwenye mkono mwa mmoja wa nunuzi na watumiaji wa zao hili ambalo wakati mwingine hupatikanaji wake,husababisha damu kumwagika.

3 comments:

Anonymous said...

Aksante kwa habari motomoto endelea na moto huo
Froma mpenda habari

Anonymous said...

Endelea vivyo hivyo bwana mkubwa,we like the news and the pictures are of a very good quality.
From Mpenda Franco Makiadi

Sindbad said...

kajumulo kazi nzuri lakini kiswahili bado sio safi na pia unaandika maneno kimakosa mara nyingi sana na pia jaribu kuyasoma kabla ya kuyaweka hapo juu.
Naamini utayajali haya maana ni ya maana kwani kuna baadhi ya watu wakiona makosa kila mara watakimbia maana makosa mengine yanabadili maana halisi na kuona mahali pengine ni tofauti na hapa
kaka fanya kweli acha bora liende.