Friday, October 26, 2007

Tupo tayari kuilinda nchi yetu

Maelfu wamuaaga hayati, nyota wa muziki wa rege Luck Dube. Itakuwa siku ya kukumbukwa milele kwa wapenzi wa muziki wa rege, duniani , Afrika na Afrika ya Kusini kwa ujumla.Siku ya tarehe 28/10/07, siku amabayo dunia imemuaaga nyota ya muziki wa rege hayati Luck Dube, amabaye amelazwa leo pale kwe yenye nyumba yake ya milele. Mke wake bibi, Zanele ,watoto wake saba, Bongi,Nonkululeko,Thokozani, Laura,Siyanda,Philani,na Melokuhle , ndugu,jamaa na marafiki. walibubujikwa na mchozi pale walipo shuhudia kulazwa kwakwe. Na hasa ni nyimbo za hayati Luck Dube zilizo kuwa zikipigwa wakati wote wa maombelezi yake katika kijiji cha Ingogo km 250 kusini mashariki mwa Johannesburg . Hayati Luck Dube alitoa album 22 wakati wa huhai wake. Hayati Luck Dube mwenye miaka 43 alifariki dunia mbele ya watoto wake, baada majambazi kutaka kumpora gari lake kwa kumiga risasi,alipo kuwa ameenda kumtembelea ndugu yake. Kwa mujibu wa polisi, watu watano wamekamatwa kuhusiana na kifo cha mwanamusiki huyo. Tupo tayari kuilinda nchi yetu pindipo tukushambuliwa. Marumbano kati ya Iran na Amerika, simapya, kutokana na msemaji wa serikali ya Iran. Kuwekewa vikwazo na Amerika hakuanza leo, na vikwazo hivyo havita tuteteresha, kwani ni kama nyongeza tu. Kutokana hali hii ,hasa baada ya viongozi wa serikali ya Amerika, kuweka wazi upo uwezekano wa kutumia nguvu za kijeshi zidi ya Iran, pindipo haita kubaliana kusimamisha kuendelea kujenga mitambo ya Nyuclia. Lakini msemaji wa jeshi wa Irana alihakikisha ya kuwa jeshi lake lipo tiyari kiulinda Iran kwa wakati wowote pindipo ikishambuliwa. Hapo juu, pichani ni mmoja wa wasemaji wakuu wa serikali ya Iran,akiongea jinsi gani Iran ilivyo jiandaa na hali hii ya kivita pindipo ikitokea.

Mtuhumiwa wa Guantanamo bay, ala miaka nchini mwake.
Katika harakati za kupingana na ugaidi, serikali ya Tunisia ime muhukumu miaka mitatu jela, mmoja ya watuhumiwa wa ugaidi, ambaye alikuwa ameshikiliwa kama gaidi kwenye jela ya Guantanamo Bay Bwana Lfti Lagha ambaye amakaa Guantanamo Bay kwa kipindi cha miaka 5 kama mtuhumiwa wa kigaidi Jichani hapo ni ya baadhi ya watuhumiwa walio kamatwa na kuwekwa kwenye jela ya Guantanamo. Rais, Putin aonya kuhusu ushindani wa siraha.
Rais wa Rusia, bwana Vladimir Putin, amesema hivi karibuni ya kuwa, kitendo cha Amerika kutaka kujenga mizinga ulaya ya masharika, ni sawa na kipindi kile cha wakati wa Kyuba ilipo kuwa na mizingas ya masafa miaka ya 1960s. Bwana putin aliyasema hayo, alipo kuwa akiongea na viongozi wa Umoja wa Ulaya mjini Lisbon Ureno. Kwa kutaka kujenga rada na mizinga hiyo ndani ya jamuhuri ya Czech, kitakuwa kitendo cha kudharirisha, na kudharau Rusia kijeshi. Na kunahabari ya kuwa huenda bwana Putin akwa waziri mkuu, baada ya kumaliza kipindi chake cha urais mwaka 2008. Picha hapo juu ni rais Putin akisikiliza kwa makini swali kutoka kwa mwandishi wa habari. Wapinzani wa siasa wa zamani wa Nigeria wakutana.
Maneno haya ya methibitishwa kwa vitendo na mshindi wa zawadi wa Nobel kwa uandishi bwana Wole Soyinka.
Baada ya miaka isiyo pungua 40, mwandishi wa vitabu Wole Soyinka ambaye ni raia wa Nigeria, amerudi kujionea mwenyewe hali ilivyo eneo la Biafra, ambalo miaka 40 iliyo pita alikuwa ni eneo lililo kuwa halina usalama na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilikuwa havina muhamana, na vilifanya watu wengi kuathirika.
Mmoja ya watu hawa ailikuwa bwana Wole Soyinka, amabye alifunga miezi 22 na kazi ngumu kwa kupinga jinsi hali ilivyo kuwa ikiendeshwa na serikali ya enzi hizo. Bwana Wole alirudi kuonana na watu walio amrisha afungwe, kwa kupinga serikali nyakati zile.
Pichani hapo juu ni bwana Wole Soyinka akiwa na watu walio mfunga miaaka 40.Kushoto bwana Wole Soyinka akiwa na bwana Ojukwu aliye husika kukamatwa kwa bwana Wole na kulia pichani bwana Wole aliwa na Mej Gowon mmoja ya watawala wa enzi hizo.
Martin Jol yamkuta ya Morinho.
Kizaaza cha kuleta matokeo,aukuifanya timu ishinde, nikitu ambacho kinahitaji,bahati kwa wakati uliopo kama kocha, lakini wapenzi na wanachama pamoja na vibopa, wa timu, huwa siku zote, wanataka matokeo mazuri, na wala siyo kuhisi kitu bahati, kinahitajiika kwenye timu.
Hali hii imemkuta kocha Martin Jol,ambaye kuja kwake wapenzi wa Totenham,kulizaniwa ya kuwa atifanya Tot-ham, kurudia enzi zake za kina Poul Gascoine. Lakini bwana Jol, mambo haya kumwendea vizuri, na hivi sasa hana kazi tena.
Na sasa Tot - ham wamempa kazi kocha mwingine bwana Juan Ramos,ambaye alikuwa akifundisha Sevilla fc ya Uispania.Hii ni katika kujaribu kurudisha hadhi ya wana Tot - ham.
Pichani hapo juu kulia ni bwana Jol aamini kama kazi ndiyo hiyooo imepepea, na kushoto chini ni bwana Juan, akiangalia kwa makini nini la kufanya, kwani kiti moto cha ligi ya Uingereza, huwa kina joto lisilo la kawaida.
Rais mstaafu Joaquim Alberto Chissano avuna alicho panda.
Hivi karibuni, rais mstaafu wa Mozambiki, bwana Joaquim Alberto Chissano, amezawadiwa, donge nono la kiasi cha dolla $ 5-Million, kwa kuwa kiongozi wa kwanza wa Afrika, kufaidiaka na tuzo la Ibrahimu Mo.
Tuzo hili, lilianzishwa na bwana Mo, ili kuwapa heshima wale vingozi ambao wametumikia taifa lao,hasa kwa wakati wa matatizo ya kisiasa na kijamii, na hivyo kujaribu kufanikisha maendeleo ya nchi na wananchi kwa ujumla.
Bwana Chissano, alianza kuwa rais wa Mozambiki, baada ya kifo cha rais wa kwanza wa Mozambiki hayati Samora Machel.
Bwana Chissano alikabiliana na matatizo ya kivita vya wenyewe kwa wenye, kati ya serikali FRELIMO na wapinzani wa serikali RENAMO kwenye miaka ya 80,lakini bwana Chissano alikabiliana na haya, kwa kuleta uelewano kati ya chama chake FRELIMO, cha wapinzani RENAMO.
Namibia ya wa moto kwa Amerika baada ya siri kugundulika.
Serikali ya Namibia ime wafukunza wa amerika wawili, amabao walikuwa wapo nchi, kwa madhumuni ya kukusanya na kulaghai wanamibia kujiunga na kampuni ambayo yana fanya kazi nchini Iraki na Afghanistani.
Kutokana na msemaji wa wizara ya mabo ya ndani, amesema watu hawa ni wawakilishi wa makampuni ya ulinzi yanayo fanya kazi katika nchi za Iraki na Afghanistani na wali kuja kwa madhumuni ya kutafuta watu wa kwenda kufanya kazi za ulinzi kwenye kampuni hizo.
China ya kasilishwa na kitendo cha kumpa nishani Dalai Lama.
Uhusianao kati ya China na serikali ya Amerika, umezidi kuingia doa.
Doa hili limekuja baada ya Amerika kumzawadia kiongozi wa Budha bwana Dalai Lama, nishani ya juu ya dhahabu ya bunge la Amerika hivi karibuni.
Bwana,Dalai Lama amabye ameishi ukimbizini kwa muda usiopungua 48 baada ya jaribio la kutaka kuleta mapinduzi nchini China,hii ilitokana na kutokuelewana na wan nchi wa Tibet.
Hapo juu pichani Dalai Lama, akikaribishwa kwenye baraza la wabunge.
Libya yarudisha vitu ilivyo taifisha wakati wa mapinduzi ya kung'oa Mfalme.
Serikali ya Libya imerudisha vitu na mali zote, ambazo zititaifishwa wakati wa mapinduzi ya kuung'oa utawala wa kifalme wa hayati Idris Senussi , mapinduzi haya yalitokea mwaka 1969. Tangu hapo rais Gaddafi akachukua madaraka.
Katika mali na vitu hivyo pamoja na nyumba inatumika na ubalozi wa Uingereza, kuanzia sasa una mmiliki mpya.
Ni muda sasa serikali ya Libya tangu ianze mpango wa kurudisha vitu na mali ambazo ilizitaifisha kipindi hicho. Hii yote ilitokea wakati hule, kwa kupitishwa sheria ya kuwa serikali pekee yake ndiyo yenye uwezo wa kujenga na kumiliki vitu.
Pichani hapo juu ni kanari, na rais wa Libya bwana M. Gadaffi.
Wazawa walalamika kuhusu mali ya asili.
Kuna habari za kuaminika ya kuwa wapinzani wa serikali ya Sudani wamevamia machimbo ya mafuta, ambayo yanachimbuliwa na makampuni ya kigeni, kutoka nchi za India, China, na Malaysia.Kwa mujibu wa wa masemaji wa mapinzania hao, waliamua kuvamia maeneo hayo na kuteka wa fanyakazi wa makampuni hayo, kwa madai, fedha zinazo tolewa na makampuni haya kigeni kwa serikali ya Sudani zinatumika katika kununulia siraha ambazo zinatumika katika kuwapigia wapinzania hawa na na badala ya kuijenga nchi yao. Msemaji huyu aliongeza kwa kusema ya kuwa hii mali ( Mafuta) ya asili "Imekuwa balahaa kwetu sisi wazawa".
Pichani hapo juu ni wapinzani wa serikali ya Sudani, wakiwa katika mazungumzo.

No comments: