Tuesday, June 24, 2008

Jumuia ya waandishi wa habari yapata msiba mkubwa" Tim Russert atupo naye tena"

Hali ya afya ya nyota ya muziki nchini Uingereza yaleta mashaka kwa wapenzi wamuziki wake.

London- Uingereza - Mwanamusiki maarufu nchini Uingereza Amy Winehouse, ameruhusiwakutoka hospital hivi karibuni, baada ya kupata matibabu ya mapafu na tiba nyingine za mwili. Amy Winehouse, ambaye inasemekana amekuwa akiishi maisha yasiyo ya kwaida kwa kujihusihsa saana na vilevi vingi na uvutaji wasigara ndivyo vinasadikiwa vina athiri afya yake. Pichani hapo juu anaonekana bi Amy Winehouse akiwa anatumbwiza wapenzi wake hivi karibuni kabla ya kupelekwa hospitali. Picha ya pili anaonekana bi, Amy Winehouse, akivuta sigara, punde tu alipotoka hospitali kwa matibabu.
Jumuia ya waandishi wa habari yapata msiba mkubwa"Tim atupo naye tena".
Washington, Amerika - Mkubwa wa shirika la utangazaji la NBC lililopo jiji Washington, bwana Tim Russert, alifariki dunia siku ya ijumaa iliyopita kwa ugonjwa wa moyo.
Hayati, Tim Russert aliajisikia vibaya wakati alipo kuwa kazini tayari kuanda kipindi kijulikacho kama 'meet Press' na baadaye kukimbiziwa hospitali ambapo alizidiwa na kuaaga dunia.
Hayati Tim Russert, atakumbukwa kwa umaili wake wakuuliza maswali na umakini wa kuelewa nini la kufanya katika fani hii ya uandishi wa habari.
Picha hapo juu ni picha ya familia ya ya hayati Tim Russert, kati ni picha ya mjane bi, Maureen Orth na kushoto ni mtoto wao Luke Russert.
Chini wanaonekana baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wakilipokea jeneza la hayati Tim Russert wakati walipo kwenda kumwaaga kwa mara ya mwisho.
Picha ya tatu, anaonekana hayati Tim Russert, akizungumza na papa Benedict XVI, wakati alipotembelea nchini Amerika hivi karibuni.
Picha ya mwisho, anaonekana hayati Tim Russert, alipokuwa kazini enzi za uhai wake.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amin.
Hali ya watu wanao penda kuishi kwa jinsia moja ni moto wa mbali nchini Uganda.
Kampala, Uganda - Serikali ya Uganda imewafungulia mashitaka waandamanaji watatu ambao walikuwa wakiandamana hivi karibuni wakati wa kuadhimisha siku ya mkutano wa unaozungumzia ugonjwa wa ukimwi.
Watu hao watatu ambao waliooshutumiwa kwa kupita na kufika maeneo yaliyo zuiliwa kuingia.
Watu hao watatu, walikuwa wakifanya hivyo kwa kutaka uongozi wa serikali ya Uganda kuwakubali watu wainao penda kuishi kijamii moja kama mke na mume au ushoga.
Kwa mujibu wa masemaji mmoja wa watu hao, alisema yakuwa ni muhimu watu wawatambue na kuwakubali watu waina hii wanao pendelea mashoga.
Hata hivyo serikali ya Uganda hairusu ushoga na ni kosa la kisheria katika jamii.
Picha hapo juu ni picha ya bendera ya Uganda.
Picha ya pili na ya tatu ni picha ya baadhi ya watu wanao penda kuishi kijinsia moja huruhusiwa hasa katika nchi za magharibi kisheria.
Kanisa lapiga marufuku kutumia kanisa kupiga picha za sinema.
Rome, Itali - Uongozi wa kanisa Katoliki mjini Rome, umepinga na kukataa kuruhusu upigaji wa picha za sinema zinazo zungumzia habari kuhusi kitabu kijulikanacho Da Vinci Code.
Hadithi za kitabu hiki ambacho kinapingwa vikali na uongozi wa kanisa la jumia ya Kikatoliki kwa kupotoshwa maadili ya Kanisa zima la Katoliki.
Picha za sinema zilitakiwa kupigwa katika makanisa ya Santa Maria del Popolo na Santa Maria della Vittoria ambayo yapo kataika jiji la Rome.
Picha hapo juu inaonesha moja ya sehemu ambazo wapigapicha wanahitaji kutumia katika kupiga picha ya sinema ya Da Vinci Code.
Picha ya pili inaonyesha picha ya kitabu ambacho maandishi yaliyomo yalitakiwa kuwekwa katika wa sinema(film).
Picha ya tatu anonekana mmoja wa wacheza sinema ya Da Vinci Code, akiwa kazini anafanya vitu vyake.
Ajali ya meli yaleta msiba mkubwa nchini Philippinzi.
Cebu, Philippinzi - Wazamiaji ambao wapo mbioni kutafuta miili ya watu ambao waliokuwemo kwenye meli yenye uzito upatao tani 23,824 ,ambayo ilipinduka ilipo kuwa ikifanya safari zake zakawaida.
Meli hii imesadikiwa ya kuwa ilikuwa imechukua (beba) zaidi ya wapatao 8000.
Ajali hiyo ilitokea hivi karibuni, wakati wa machafuko ya hali ya hewa yaliyo tokea hivi karibuni nchini Philippinzi.
Hata hivyo msemaji mmoja wa serikali, alisema yakuwa watu wapatao 43, walipona kutokana na janga la ajali hii ya meli.
Picha hapo juu ni picha ya meli ambayo imepinduka hivi karibuni na inasadikiwa kupoteza maisha ya watu wengi kwa wakati mmoja.
Picha ya pili, wanaonekana baadhi ya ndugu na jamaa wa watu waliosafiri na meli hii iliyo pinduka, wakibandika picha za ndugu zao kwenye ofisi ya shirika la meli ambayo ndiyo mmiliki.
Abu Hamza Al Masri ashindwa" Huenda akapelekwa Amerika kujibu mashitaka".
London - Uingereza - Mahakama kuu ya Uingereza imeidhinisha kupelekwa kwa Abu Hamza Al Masri nchini Amerika kujibu mashitaka ya dhidi ya ugaidi.
Abu Hamza Al Masri, ambaye anatumika kifungo cha miaka saba kwa kosa la kushawishi ugaidi nchini Uingereza.
Abu Hamza Al Marsi 51, ambaye alidai yakuwa alipoteza jicho lake na mkono wake alipo kuwa nchini Afghanistan, anakabiliwa na mashitaka yapatayo 11 ikiwemo kuhusika kwake katika utekaji nyara wa watalii mwaka 1998 nchini Yamen.
Picha hapo juu ya bwana ,Abu Hamza Al Masri anayetuhumiwa kuhusika na makosa ya ugaidi.

No comments: