Thursday, June 5, 2008

Mtuhumiwa wa milipuko ya majengo ya jiji la New York, awakataa mawakili wake"Mola akipenda ifanyike" Adai mtuhumiwa

Kesi ya Robert Kelly , shahidi akataa kutoa ushaidi, na ndugu wawa na wasiwasi .

Chicago, USA- Mwanamziki mashuhuri duniani Robert Kelly au R Kelly, amerudi mahakamani kusikiliza kesi inayo mkabili yakuwa alifanya mapenzi na msicha na ambaye alikuwa ajafika umri wa mtu mzima na kupigwa picha katika mkanda wa video.
Kwa mujibu wa mwanasheria wa serikali,ambaye anasimamia kesi hyo amesema yakuwa R. Kelly alifanya kosa hilo mnamo miaka ya nyuma.
Hata hivyo Robert Kelly, alikana kosa hilo na mwana dada aliyehusika naye kataika kesi hii alikana kosa hilo.
Kesi hiyo imeingia sura mpya baada ya mwandishi wa habari ambaye alikuwa na mkanda hua kukataa kuatoa ushaidi , na mmoja wa ndugu ya msichana huyo kuwa na wasiwasi ya kuwa sura iliyopo kwenye mikanada hiyo ya video ni ndugu yake/yao.
Picha ya hapo juu anaonekana gwiji la muziki wa R&B, R. Kelly akifanya vitu vyake huku nyuma taa za marangi zikimsapoti kumelemeta na kupendeza mbele ya wapenzi wa muziki wa wake .
Picha ya chini anaonekana Robert Kelly - R . Kelly, akitokea ndani ya gari kuelekea mahakamani kusikiliza kesi inayo mkabili.
Majirani wakubaliana kimsingi kupambana na Joseph Koni" Amani mashakani".
Kampala, Uganda - Serikali za Uganda Sudan na Jamuhuri ya Kongo (DRC), zimekubaliana kwa pamoja kupambana kijeshi na kundi la LRA Load Resistance Army linalo ongozwa na bwan Joseph Koni.
Hali ya makubalianao haya yamekuja baada ya serikali ya Uganda kushindwa kuku baliana na kundi la LRA kutia saini mkataba wa amani.
Akihutubia bunge la Uganda, rais wa Uganda bwana, Yoweri Kaguta Mseven, alisema ya kuwa wakati wa kuongea umekwisha na lazima bwana Koni akamtwe kwakutumia nguvu zote, na alisema yakuwa serikali ya Uganda na majirani zake Sudani na Jamuhuri ya Kongo wamekubaliana kimsingi na swala hilo.
Hata hivyo matamshi ya rais Museven, yamekuja baada ya mmoja wa maofisa wa mahakama ya kimataifa mjini Hegue Holland, bi, Silvia Arbia aliyekuwa ziarani nchini Uganda kudai ya kuwa wanacho cheti cha mahakama cha kuruhusu kumkamata bwana Joseph Koni.
Hata hivyo bi Silvia Arbia, alikataa lawama ya kuwa, bwana, Joseph Koni, hakuweza kufika katika vikao vyote, kwani ilijulikana toka mwanzo yakuwa kipo chet cha kumkamaya na kusababisha kutotiwa saini makubaliano ya amani nchini Uganda.
Picha hapo hapo juu ni picha ya bwana, Joseph Koni akiwa amevalia mvazi yake ya kijeshi wakati wa miaka ya nyuma alipo kuwa akionga na mmoja ya waandishi wa habari.
Picha ya pili anaonekana bwana, Josepha Koni, kushoto na katikati makamu wa rais wa Sudani ya Kusini bwana Riek Machar na kulia ni msaidizi wa bwana, Koni, bwana Vicent Otty, wakati walipo kutana mapema kabla yakuanza mazungumzo ya amani ambayo yameshindwa kushikia lengo la kuleta amani nchini Uganda.
Picha ya tatu anaonekana bwna Joseph Koni , akiwa na mmoja wa maafisa wa Umoja wa Mataifa, bwana, Jan Egeland wakati walipokutana mapema miaka ya nyuma ili kuleta mapatano ya amani nchini Uganda.
Mtuhumiwa wa milipuko ya majengo ya jiji la New York, awakataa mawakili wake" Mola akipenda ifanye" Adai mtuhumiwa.
Guantanamo Bay, Kuba (Kyuba) - Mtuhumiwa mkuu wa matukio ya kulipua majengo yenye vitega uchumi na kusababisha maafa makubwa ambayo hayajawai kutokea katika historia ya ya Amerika bwama Kharid Sheikh Mohammed, amefikishwa mahakamani.
Bwana, Khalid Sheikh Mohammed, ambaye inaaminika ndiye aliye kuwa mtaaluma na mpangaji wa mashambulizi hayo yaliyotokea tarehe 11/9/2001 mjini New York.
Huku akisiakia ni nini jaji wa mahakama anasema, bwana Khalidi Sheikh Mohammed, alisema ya kuwa, alikuwa anaomba adhabu ya kifo, kwani hii nilikuwa nasubuli kwa hamu hali hii , kwa uwezo wa Mola yote yawe.
Na vilevile bwana Khalid Sheikh Mohammed aliwakataa mawakili wake na kudai hawaitaji wao kumtetea, ila wakipenda kubaki wanaweza bakia kusikiliza nini kienaendelea na kufanyika.
Picha hapo juu ni picha ya bwana Khalid Sheikh Mohammed wakati alipo kamatwa hapo mwanzoni.
Picha ya pili ni picha ya moshi ukitoka kwenye moja ya majengo ambayo yalilipuliwa na ndege zilizo gonga majengo haya marefu ya jiji la New York na kuleta hathali kubwa katika jiji la New York na kupoteza maisha ya watu wasiopungua mamia.
Baraka Obama aonyesha dunia ya kuwa mabadiliko yanawezekana" Awa mgombea pekeea wa kiti cha Chama cha Demokrati".
Chicago, USA - Mwakilishi wa chama Demokrati cha Ameriaka, bwana Barak Obama, amesema ya kuwa atakuwa bega kwa bega na watu na serikali ya Israel.
Akiongea haya mbele ya mkutano unaojumuiasha wananchi wa jumuia ya AIPAC - America Israel Public Affairs Committee mjini Chicago.
Baraka Obama, ambaye amemshida mpinzani wake bi, Hiraly Clinton kwa kura nyingi na hivyo kuwa mgombea pekee ambaye atawakilisha chama cha Demokrasi, ili kupambana na rais Jonh McCain ambaye ni mgombea pekee wa chama cha republikani.
Mpambano wa uchaguzi huo utafanyika karibu na mwisho wa mwaka 2008.
Hatuitambui mahakama ya kimataifa,"yasema serikali ya Sudani".
Karthoum, Sudan - Serikali ya Sudan, imekataa kuwatoa au kuwakamata baadhi ya viongozi wa nchi hiyo ambao wanashutumiwa katika kukiuka haki zan binadamu kweny maeneo ya Darfur..
Viongozi hao, ambao wamo katika serikali ya Sudan, wanatakiwa kujibu mashitaka katika mahakama ya ICC -(International Criminal Court) iliyopo nchini Uhollanzi.
Watuhumiwa hao ni katibu wa serikali anaye shughulikia haki za binadamu nchini Sudani bwana Ahmed Haroun na kiongozi wa kikundi la Janjawidi Alli Kosheb.
Msemaji mmoja wa serikali, aliseamya kuwa hawawezi kuwapeleka wanchi wao kwenye mahakama hiyo kwani na hawaitambui na Serikali ya Sudani siyo mwanachama wa ICC - International Criminal Court.
Picha hapo juu ni picha ya baadhi ya makazi ya watu wa Darfur yakiwa yamebakia magofu baada ya kushambuliwa na kuungua vibaya.
Matatizo ya usalama nchi Sudani, huwafanya hata vijana wadogo kusasahau nini maana ya ujana , na badala yake kuwa tiyari kutetea haki zao, au wakati mwingine hulazimishwa kupigana vita ambavyo hawavijui mwanzo wa mwisho wake.
Picha ya chini wanaonekana wakina mama na watoto wa Darfur, wakiwa hawajui la kufanya, bali kuangalia nini jumuhia ya kimataifa itawasaidia nini?
Mahujaji wa Kiyaudi kutoka sehemu tofauti duniani wa dhulu Hekalu kuu la zamani.
Djerba, Tunisia - Mahujaji wa Kuyahudi wasiopungua maelfu, walikutana mjini Djerba, ili kuadhimisha baadhi ya nguzo za dini ya Kiyahudi kwenya Hekalu la lililopo mjini humo.
Hekalu hilo ambalo ni moja ya Mahekalu ya zamani kaskazini mwa Afrika
Picha hapo juu kwenye mlango inaonyesha moja ya alama ambayo ipo moja ya Mahekalu ya Kiyahudi.
Picha chini wanaonekana Mahujaji waki wakielekea kwenye Hekalu tayari kutimiza nguzo za dini na picha ya mwisho ni moja ya alama muhimu kwa waumini wa Kiyaudi.
Hali ya Burma - Myanmar bado kiti moto kwa wananchi wa nchi hiyo.
Washington,USA - Serikali ya Amerika , imesema ya kuwa serikali ya kijeshi ya Burma - (Mynmar) imekata kata kuirushusu shehena ya misaaada kupelekwa nchi Burma.
Msemaji mmoja wa serikali bwana, Timoth Keating, amesema yakukwa meli ya ya Amerika ambayo ipo kutoa msaada kwa jamii iliyo pata maafa kutokana na kimbunga kilicho ambatana na mvua kali.
Kimbunga hicho, ambacho kimepoteza maisha ya zaidi ya watu 70,000, wengine wapatao 55,000 bado hawajulikani walipo na watu wapatao millioni wanaishi katika hali ya hatari kiafya na kimazingira.
Pichani hapo juu wanaonekana baadhi ya raia wa Burma wakipokea misaada kutoka kwa wafadhili tofauti ili kukabiliana na janga la njaa.
Picha chini ni picha ya melikebu ya jeshi ambayo ipo katika maji ya kimataifa, ikisubiri kuingia bandarini tayari kutoa midaada ya kibinadamu nchini Burma.

No comments: