Tuesday, June 3, 2008

Mwanasayansi wa nyuklia akanusha na kusema alilazimishwa, kinyume na matwakwa yake

Bingwa wa musiki wa kunja mwili na kuzunguka majoka na mwasisi wa muziki wa risimu na blues , afariki dunia.

Mississipii, USA - Bingwa wa musiki wa risimu na Blues duniani , Bo Diddley amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79.
Bo Diddley, ambapo hapo mwanzoni alikuwa akipiga musiki wa aina ya rock en roll - au vunja mwili na kuzunguka ,kwenye miaka ya 1955.
Marehemu Bo Diddley atakumbukwa kwa nyimbo zake za awali zilizo julikana kama Buddy Holly's,Not Fade Away, ambapo miziki hii ilionekana mara kwa mara kwenya album za Rolling Stone.
Marehemu Bo Diddley, alifariki dunia na ameacha watoto wanne na mke wake Kay.
Lawama za tupiwa nchi tajiri kwa ukosefu wa lishe duniani"Dunia yatumia faranga kwa matumizi mengine".
Rome, Itali - Kikao kinachosimamiwa na shirika la chakula duniani FAO ( Food and Agriculture Organization) kimefunguliwa rasmi mjini Rome Itali kutathimini hali ya upungufu wa chakula duniani.
Akoingea haya, mkurugenzi mkuu wa shirika hilo la chakula duniani, bwana Jacques Diof, alisema ya kuwa pesa nyingi zimekuwa zikipotea na wakati watu wapatao mamilioni wanakufa na njaa.
Kikao hicho amabcho kinaudhuiwa na rais wa Zimbabwe, bwana Robert Mugabe, na kuhutubia kikao hicho ,rais Mugabe , alisema ya kuwa nchi za Ulaya ziache kutumia matatizo ya chakul;a duniani kwa kuyaingiza kwenye siasa na kusababisha matatizo kataika nchi ya Zimbabwe.
Vile vile kikao hiki kimeudhuliwa na rais wa Iran, bwanaMahamoud Ahamadinejad ambaye pia alilaumu nchi za Ulaya kwa kusababisha matatizo ya lishe duniani.
Picha hapo juu ni picha ya rais wa Iran, anaye hudhulia kikao cha kutathmini hali ya lishe duniani mjini Rome.
Picha ya kati wanaonekana watu waishio dunia ya tatu wanavyo pata tabu kupata lishe bora,hapo pichani wanaonekana wakichakuwa kwenye majalalal ili kutata chochote ili wakapate ridhiki.
Picha ya mwisho anaonekana rais Robert Mugabe, amabye kuhudhulia kwake kwenye kikao cha Rome , kumeleta msuguano wa vichwa kwa nchi za Ulaya Magharibi.
Mwana sayansi wa nyuklia akanusha na kusema alilazimishwa kinyume na matwakwa kwa yake.
Islamabad, Pakistan. Aliyekuwa mtaaalamu ambaye anadaiwa kuwa alihusika na uuzaji wa utalaalamu wa kutengeneza nguvu za nyuklia bwana, Abdul Qadeer Kahn,amesema hivin karibuni ya kuwa, kutubu kwakwe kulikuwa kwa msukumo wa serikali ya rais, Pevez Musharraf. Akiongezea , bwana Kahn, alisema yakuwa alikuwa hajahapishwa wa kukubalina kushirikiana na shirika la kuchuguza nguvu za kinyuklia, International Atomic Enegy Agency.
Bwana Kahna, mwenye miaka 72, amabye yupo katika kizuizi cha nyumbani , amambaye ana matatizo ya kiafya, alisema ya kuwa hakukuwa na haja ya yeye kuongea na IAEA, kwani haikuwa na huusiano na shirika hilo la IAEA.
Picha hapo juu ni ya rais, Pevez Musharraf alipokuwa Amerika hivi siku za karibuni.
Picha ya kati ni picha ya rais, Musharraf ambaye anonekana amevalia nguo zake za kazi za kijeshi, kabla ya kuacha rasmi kuwa mwanajeshi na kuwa raia na baadaye kuchaguliwa kuwa rais wa Pakistan.
Picha ya katikati,ni picha ya Abdul Qareed Kahn, ambaye anadaiwa kuuza siri za nyuklia kwa nchi kama Korea ya Kusini , Libya na Iran.
Picha hapo chini anaonekana bwana, Abdul Kahn alipo kuwa akiongea kuhusu swala la yeye kukubali ya kutubu hadharani.
Australia kuyatoa majeshi yake nchini Irak.
Sydney, Australia - Serikali ya Australia imeanza kuyatoa majeshi yake nchini Iraq, baada ya miezi tangu kuchaguliwa waziri mkuu mpya wa Australia bwana Kevin Rudd ambaye alihidi haya wakati wa kampeni zake zauchaguzi.
Wanajeshi wapatao 500, walikuwa kusini mwa nchi ya Irak, ikiwa ni moja ya harakati ya kusaidia kulinda amani nchini Irak.
Hata hivyo wanajeshi ambao wanafundisha jeshi la nchi ya Irak ,ili kujijenga kiusalama watabaki humo nchini Irak kwa kipindi fulani.
Pichani hapo juu, wanaonekana wanajeshi wa jeshi la Australia wakiwa kazini kulinda nchi ya Irak, kabla ya kuanza kuondoka nchni Irak.
Picha ya pili ni picha ya moja ya vifaa vya kivita, ambavyo Australia ilikuwa ikivitumia katika vita nchi Irak.
Dunia yakubaliana kimsingi kusimamisha matumizi ya mabomu mkawio kulipuka.
Dublin, Irish - Wajumbe wapatao 111, wamakubaliana kimsingi kupiga marufuku matumizi ya mabomu ya aina ya Kalista au mabomu mkawio kulipuka.,aina ya mabomu ambayo hupasuka baada ya muda kudondoshwa katika eneo lililo kusudiwa.
Makubaliano yayo yalifikwa baada ya mijadala iliyochukuwa zaidi ya wiki mbili.
Makubaliano hayo yamekumbana na vikwazo, baada ya nchi wazalishaji wa mabomu haya, kama, Amerika , Urusi , Israel , China na Pakistan, zimekuwa zikipinga kupitishwa muswadaa huu.
Picha hapo juu ni picha ya aina ya mabomu ambayo huwa zinadondoshwa nabaadaye kulipuka kusababisha maafa makubwa kwa jamii.
Huhusiano wa Belgium na Kinshasa waingia kihoro,kuwa kama miaka ya nyuma ya 47 "Enzi za miaka ya tisini".
Kinshasa, Jamuhuri ya Kongo - Serikali ya Kinshasa, imefunga ofisi zake za kibalozi nchini Belgium, baada ya kiongozi wa serikali, Karel De Gucht kusema yakuwa ni muhimu kwa serikali ya Belgium kufautilia matumizi ya fedha wanazo toa kwa serikali ya Kinshasa, kwa kuzingatia DRC ilikuwa ni koloni la zamani la Belgium.
Serikali ya Belgium, huwa inatoa kiasi kisicho pungua 200 million euro kwa mwaka kwa serikali ya DRC.
Ofisi hizi zilizofungwa ni za mji wa Antwepe na huhusiano wote wa kiserikali kati ya serikali hizi mbili.
Msemaji wa serikali ya Kinshasa, alisema ya kuwa DRC ni nchi iliyo huru na inajiamulia mambo yake yenyewe.
Na wakati huhuo, kiongozi wa wa chama cha upinzani nchini DRC kijulikancho kama Movement for the Liberation of Congo Party, bwana, Jean Pierra Bemba alikamatwa hivi karibuni mjini Brussel, kwa kosa la kushutumiwa kuhusika na makosa ya kivita na haki za kibinadamu.
Picha hapo juu anaonekana rais wa DRC, bwana Joseph Kabila akiwa katika moja ya mikutano ya ya kimataifa.
Chni anaonekana rais , Joseph Kabila akiwa amavalia mavazi yake ya kijeshi, wakati akipo kuwa akiongea kuhusu hali ya usalama wakati alipokuwa karibu kuapishwa kuwa rais wa mpito baada ya nchi ya DRC, na baadaye alichaguliwa kuwa rais wa DRC .
Hali ya kuelewana kati ya Hezbollah na serikali ya Israel kupatikana hivi karibuni?.
Jerusalem,Israel - Serikali ya Israel imemwachia huru mapema mwanzoni mwa wiki, aliyekuwa mpelelezi wa kundi la Hezbollah,bwana Nassim Nissir ambaye alikuwa jela kwa kipindi cha miaka sita.
Hata hivyo kundi la Hezbollah lili wapatia serikali ya Israel mabaki ya mwili wa wanajeshi wa lio uwawa wakati wa mapambano na Israel mwaka 2006.
Na wakati huo huo, serilaka ya Israel ipo katika hali ya utata baada ya kutangaza kuendelea kutanua ujenzi wa makazi mapya.
Utata huu, unakuja baada ya ya kutojulikana ni nini kiliongelewa kati ya waziri mkuu wa Israel, bwana Ehud Olmet na rais wa serikali ya Wapalestina bwana Mahmoud Abbas.
Pichani hapo juu anaonekana bwana, Nassim Nassir akivuka mpaka kuingia Lebanoni baada ya kuachiwa na serikali ya Isreal.
Picha chini anaonekana bwana Nassim Nissir akipokea busu mwanana kutoka moja ya ndugua wa familia yake.

No comments: