Friday, June 27, 2008

Licha ya joto ya siasa kuwa juu nchini Zimbabwe" Siasa na Uchumi haviko sawa" Kampuni kuendela na uchimbaji madini.

Billy Gates,aamua kutumia muda mwingi kujitolea kwa jamii".

Los Angeles, US - Mwenyekiti na mwanzilishi wa kampuni inayo shughulikia mtandao duniani bwana Billy Gates, ameamua kutangaza ya kuwa atatumia muda wake mwingi , ili kuweza kusimamia na kuendesha shughuli zake za kusaidia na kutoa huduma kwa jamii kupitia shirika alilo lianzisha mapema miaka ya nyuma lijulikanalo kama Billy and Melinda Gate Foundation.
Shirika hilo ambalo Billy pamoja na mkewe Malinnda wamakuwa wakisimamia, limekuwa likitoa misaada kwa jamii kwa kiasi kikubwa sana.
Billy mwenye miaka 52, alianza shughuli za mtandao wakati akiwa na miaka 13.
Billy aliamua kuachana na masomo ya elimu ya juu katika chuo kikuu cha Harvard, na kuamia New Mexico,mahali ambapo yeye na rafiki yake Poul Allen, walianzisha mtandao wa microsoft mwaka 1975. Mwenyekiti , Billy Gates, alisema mafanikio ya microsoft yametokana na jitihada za wafanyakazi wenzake.
Picha ya kwanza anaonekana mstari wa chini kushoto anaonekana Billy Gates, akiwa na washiriki wenzake mwaka 1978.
Picha ya pili, baada ya kucha kuendelea na masomo ya juu, hivi karibuni Billy Gates kushoto, alitunikiwa shahada ya juu na na chuo kikuu cha Harvard mwaka 7/6/2007.
Picha picha ya tatu,anaonekan ni jinsi gani Billy Gates alivyo kuwa anafikilia ni nini afanye ili aweze kufanya dunia iwe sehemu ya usawa na kusaidiana.
Picha ya mwisho , Billy Gates akiwa na Malkia Elizabeth wa Uingereza, wakati alaipo mtunukia nishani mwaka 2005
Lisha ya joto ya siasa kuwa juu nchini Zimbabwe, "Siasa na Uchumi haviko sawa".Kampuni kuendelea na uchimbaji.
Harare, Zimbabwe - Kampuni kubwa duniani inayo shughulikia uchimbaji wa madini Agro American, imesema yakuwa itaendelea na mradi wake wa uchimbaji wa madini aina ya platinum nchini Zimbabwe.
Kwa mujibu wa kampuni hiyo, imesema kuwepo kwa Agro American nchini Zimbabwe tangu miaaka ya 1960 na mradi huu umekuwa ukiendelea tangu mwaka 2003 na vilevile kunainua maisha ya wafanyakazi ambao no raia wa Zimbabwe.
Inaaminika ya kuwa mradi huu utagharimu zaidi ya $US 400million na utakuwa ni wa kwamza katika nchi za kigeni.
Hata hivyo Agro American, imesema ya kuwa serikali ya Zimbabwe imnapaswa kulifikilia swala la kisiasa linavyo kwenda nchini Zimbabwe.
Picha ya kwanza hapo juu wanaonekana wafanyakazi wakiwa ndani ya ardhi wakielekea kuchimba madini.
Picha ya pili hii ni moja ya picha ya maeneo ambayo huwa yanachimwa madini.
Picha ya tatu, wanaonekanawafanyakazi wakiwa wanatumia nyenzo nzito kuchimba madini,
Vita Afriaka, vinaghalimu kiasi cha mabillioni ya US $ dola, "na wanamama wawa waathirika".
UN, New York - Kiasi cha zaidi ya mabillioni ya fedha yanatumika kufadhili vita katika nchi za bara la Afrika imeripoti shilika moja la kutoa huduma la Oxfam lililopo Uingereza.
Kwa mujibu wa ripoti iliyo tolewa na mapema mwisho wa mwaka 2007, imeonyehs aya kuwa tangu mwaka 1990 hadi kufika mwaka 2005 zaidi ya nchi zisizo pungua 23 zilizipo barani Afrika zilimekuwa navita au zilicha wahi kuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe au nchi kwa nchi na kughalimu zaidi ya $ US billioni 300.
Kwa mujibu wa ripoti hii, pesa nyingi zimekuwa zikitumika kununulia siraha, nakuagiza lazima kuwepo na sheria ya kuchunguza ni jinsi gani siraha hizi zinapatikana kutoka nje ya bara la Afrika.
Wati huo huo shirika la jingine linalo shughulikia utoaji wa misaada na huduma kwa watoto, UNICEF, limesema ya kuwa vita vinavyo endelea katika bara la Afrika vimekuwa vinaleta athali nyingi katika jamiii, hasa kwa kina mama na watoto.
UNICEF, ililipoti hivi mapema mwaka huu ya kuwa wanawake wamekuwa wakibakwa, ( kufanya mapenzi kwa kutumia nguvu bila hiyari ya mtu), hali hii imekuwa pia ikifanywa na hata raia na baadhi ya wapiganaji( wanajeshi wa vikundi vinavyo pigana).
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya wanawake wakijaribu kuingia katika moja ya jengo la serikali ili kuokoa maisha yao, baada ya kutokea vurugu na mapigano ya kutumia siraha kwenye maeneo wanaoishi.
Picha ya pili wanaonekana baadhi ya wapiganaji wa moja ya vikundi, ambavyo wakati wanapo pigana na vikundi vingine huwa hali ya ubakaji wa wanawake hutokea na pengine wanawake hawa hupoteza maisha yao.
Picha tatu, anaonekana mmoja ya mwanamama akilia kwa uchungu na huku amejiinamia baada ya kumaliza kueleza yaliyo mkuta wakati wa vurugu na mapigano na pembeni ni mtoto wake akiwa ananagalia na hajui nini kimemkuta mzazi wake.
Nchini zilizopo pembe ya Afrika mashakani"Huenda zikakumbwa na vita".
Bruseli, Belgium - Shirika moja linalo shugulika na kutathmini matatizo na majanga dunia, limesema yakuwa hali ya ilivyo hivi sasa pembezoni mwa pembe ya bara la Afrika huenda ikakumbwa na janga la kuibuka vita kati ya nchi ya Ethiopi na Eritrea.
Shirika hilo ambalo silo la kiserikali, limesema ya kuwa, mbele ya balaza la umoja wa Mataifa, linalo shugulikia usalama, ya kuwa umoja wa mataifa hauangalii kiundani na kutilia mkazo jinsi ya kusuruhisha mgogoro ulipo kati ya nchini hizi mbili.
Hata hivyo shirika hilo , liliagiza ya kuwa ule mkataba wa amani ulikubaliwa mwaka 2000, utekelezwe na nchi hizo mbili zikae na kujadili ni jinsi gani zitatatua mgogoro huo.
Picha hapo juu wanaonekana kijana mmoja akiwa ameshikila pisto ambayo ailikuta imeachwa njiani,katika moja ya maeneo yanayo zungumziwa na shirika linalo shughulika matatizo na kutathmini hali ya majanga duniani.
Picha ya pili inaonyesha ni jinsi gani vita vinapo piganwa katika nchi yoyote, basi watoto na wakina mama ndiyo huwa wanahathirika na hali hii, hapo juu anaonekana mtoto mmoja ambaye afya yake ni dhofu kwa kukosa lishe na matibabu, kwa sasbabu vita bado vinaendelea katika eneo la pembe ya Afrika.
Korea ya Kusini ya onyesha matumaini kwenye jumuia ya Kimataifa.
Pyongyang, Korea ya Kusini - Serikali ya Korea ya Kusini,leo tarehe 27/06/2007, imevunja na kubomoa sehemu moja ya kiwanda kilicho kuwa kikitumika kutengenezea nguvu za kinyuklia.
Mlipuko mkubwa, ulisikika mbele ya waangalizi na wakaguzi wa nguvu za nyuklia wa kimataifa na huku baadhi ya waandishi wa habari wakishuhudia uvunjwaji huo, ilikuiakikishia jumuia ya kimataifa ya kuwa Korea ya Kusini, ipo mbioni kutekeleza azma yake ya kuacha kabisa kuendelea na harakati za kujenga nguvu hizo za kinyuklia.
Kitendo hicho cha serikali ya Korea ya Kusini, kimekaribishwa na jumuia ya kimataifa ikiwemo waasimu wake wasikunyingi ambayo ni serikali ya Amerika.
Picha hapo juu linaonekana moja ya kinu kilicho kuwaa kikitumika kuendeshea mitambo ya nguvu za kinyuklia kiporomoka.
Picha ya pili wanaonekana baadhi ya wafanyakazi wa serikali ya Korea ya Kusini, wakiwa kazini katika moja ya idara zinazo shughulika nguvu za mitambo ya kinyuklia.
Picha ya tatu. serikali ya Korea ya kusini ikionyesha moja ya siraha zake za kivita katika moja ya siku za sherehe za kimataifa.

No comments: