Wednesday, June 18, 2008

Viongozi waasimu wawili wa nchi jirani kukutana kwenye mkutano"Asema waziri wa mambo ya nje".

Mfalme wa mtindo wa samba afariki dunia. Rio De Jenairo, Brazil - Aliyekuwa bingwa wa kuimba na kucheza mtindo wa samba nchini Brazil, bwana Jose Bispo Clementino aliye kuwa na miaka 95, amefariki dunia hivi karibuni. Mwana muziki huyu ambaye ametamba katika mtindo huu wa samba zaidi ya miongo mitano alifariki katika hospitali ya Rio. Jose Bispo Clementino, alizaliwa mjini Rio De Jenairo 1913, atakumbukwa kwa maneno yake matamu matamu ya kuwa anapenda miziki na vimwana kwake sio kazi kubwa kuvinjari nao. Pichani hapo juu anaonekana hayati Jose Bispo Clementino, alipo kuwa akifanya vitu vyake enzi ya uai wake.Mungu ailaza mahari pema peponi roho yake Amin. Mtuhumiwa aliyetaka kuongoza mapinduzi ya kupindua serikali ya Ekwetoria Guinea angoja nini pitalato atasema.

Malabo, Ekwetoria Guinea - Aliyekuwa mmoja ya watuhumiwa ambao walihusika katika jaribio la kutaka kumpindua serikali ya Ekwetoria Guinea huenda akahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.
Mtuhumiwa huyu bwana, Simon Mann, ambaye inasadikiwa alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa mstari wa mbele kutaka kuongoza mapinduzi ya kuingoa serikali ya Ekwetoira Guinea.
Bwana Simon Mann, aliye kamatwa nchini Zimbabwe, alikili kwa kukubali makosa haya wakati alaipo kamatwa 2004, muda baada ya kabla ya mapinduzi haya kutokea na alidai ya kuwa hakuwa peke yake wapo wakubwa wake.
Hata hivyo viongozi wa serikali ya Ekwetoria Guinea, walidai ya kuwa bwana, Simon Mann, alikuwa kama chambo lakini wahusika wakuu wapo.
Kesi hiyo ambayo ina muhusisha bwana Mark Thatcher, mtoto wa waziri mkuu wa zamani wa Uingereza,bi Magreth Thatcher,ambaye inasemekana ndiye aliye kuwa mfadhili mkuu,na bwana Mark Thacher, alihukumiwa kwa kutozwa fini na kifungo cha nje.
Picha hapo juu ni picha ya bwana Simon Mann, akielekea mahakamani kusikiliza kesi yake.
Picha ya pili ni picha ya Mark Tharcher, ambaye inasemekana alikuwa mfadhili mkubwa wa mapinduzi yaliyo taka kutokea nchini Ekwetoria Guinea.
Picha ya chini anaonekana Mark na mama yake bi Magreth Tharcher wakati walipo kuwa wakielekea kwenye moja ya sherehe za kiserikali.
Viongozi maasimu wawili wa nchi jirani kukutana kwenye mkutano" Asema waziri wa mambo ya nje".
Paris, Ufaransa - Viongozi wa nchi mbili maasimu na majirani wa kihistoria wa rais wa Syiria bwana Bashir Al Assad na waziri mkuu wa Israel, bwana Ehud Olmert, huenda wakakutana ana kwa ana wakati wa mkutano utakao fanyika mjini Paris hivi karibuni.
Akisema hayo , waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ufaransa, bwana Bernard Kouchner, alisema haya mbele ya bunge.
Alisema ya kuwa katika mkutano huo, ambao utajumuisha nchi zilizopo kwenye ukanda wa Medeteranian, viongozi hawa watakaa meza moja.
Hapo juu ni picha ya rais wa Syiria , bwana Bashar Al Assad ambaye huenda akaudhulia mkutano wa Paris.
Picha ya chini, anaonekana, waziri mkuu wa Israel, bwna Ehud Olmert, anaonekana akifikilia kwa makini nini jinsi gani amani itapatikana kwenye eneo la masharika ya kati.
Rais, George Bush, afanya ziara ya mwisho Ulaya , akiwa kama rais wa Amerika.
London, Uingereza - Rais wa Amerika , bwana, George Bush alikuwa ziarani katika nchi za Ulaya Magharibi hivi karibuni.
Ziara hii itakuwa ya mwisho kwa rais Bush akiwa kama rais wa Amerika.
Kataika ziara yake aliweza tembelea nchi za Ufaransa pamoja na Uingereza, ambapo alikutana na viongozi wa nchi hizo na kujadili maswala mbalimbali ya nayo ikabiri dunia kwa sasa.
Katika mazungumzo hayo na viongozi wa wa nchi hizo, walisisitiza jinsi ya kutokomeza ugaidi duniani na swala la nchi ya Iran kupa nguvu za kinyulia.
Pichani hapo juu anaonekana rai, George Bush akiwa na Malkia wa Uingereza, wakati alipo kwenda kumtembelea Malkia.
Ziara ya rais George Bush, ilikuja na maandamano makubwa yaliyo fanywa nchini Uingereza, kwa kupinga kuja kwa rais Bush nchini humo.
Chini wanaonekana rais George Bush , akiwa na mkewe Laura, wakiwaaga wananchi wa Uingereza kabla ya kuanza safari ya kulekea nyumbani.
Rais wa zamini Kuba, Fidel Castro aonekana mzima wa afya mbele ya wa Kuba.
Havana, Kuba - Rais wazamani wa Kuba , bwana Fidel Castro, ameonekana kwa mara ya kwanza kwenye runinga ya Kuba baada ya kufanyiwa upasuaji kipindi cha miezi sita iliyo pita.
Rais huyo wa zamani wa Kuba bwana Fidel Castro pamoja na mdogo wake Raul Castro, walionekana akiongea na rais wa Venezuela bwana Hugo Charvez.
Pichani wanaqonekana rais wa zamani wa Kuba , bwana Fidel Castro katikati, kulia Raul Castro na kushoto ni rais wa Venezuela bwana Hugo Charvez walipo kutana hivi karibuni.
Picha ya chini anaonekana rais wa zamani wa Kuba bwana, Fidel Castro, akisikiliza kwa makini nini kinaongelewa wakati walipo kutana na rais wa Venezuela.

No comments: