Tuesday, June 10, 2008

Rais Gaddafi akataa makubaliano ya Mediterranian" Utavuruga na kuvunja nguvu za uhusiano wetu"

Nani kuwa bingwa wa soka 2008 , "Homa ya panda tena kwa wapenzi wa soka Ulaya".

Viena, Uswis - Mashindano ya kugombea ubingwa wa mataifa ya Ulaya kwa kwenye mchezo wa soka, kabumbu au mpira wa miguu yameanza rasmi siku ya jumamaosi suku ya ya tarehe 7/06/2008.
Mashindano haya ambayo yanazikutanisha timu ambazo zilifaulu kupita mthiani wa kugombania nafasi hii wakati wa awamu ya mwanzo.
Nchi ambazo zinashiriki kinyang'anyiro hiki ,i mabingaw watetezi, Ugiriki , German, Ureno, Sweden, Spania, Uhollanzi,Itali,Uturuki, Urusi, Swisi , Ausrtria,Romania,Cratia, Poland, Ufarannsa na Jamuhuri ya Czech.
Picha hapo juu, wanaonekana baadhi ta wachezaji maarufu duniani katika picha moja, wengine wakiwa na majonzi baada ya kukosa kikombe hiki cha ubingwa wa Ulaya wakati nchi zao zilipo shindwa kunyakua kikombe hiki, na wachezaji wengine wakiwa wamenyaua kikombe cha ubingwa wa Ulaya, wakati nchi zao zilipo fanikiwa kuwa mabingwa wa kikombe hicho.
Chini ni moja ya viwanja ambavyo nyasi za uwanja wake zitakuwa na kazi ngumi kikabili vishindo vya wanaume walioshiba tayari kuonyeshana nani atanyakua kikombe hiki cha Ulaya 2008 hadi 2012.
Picha hapo ya mwisho ni picha ya mrembo ambaye alikuwepo wakati wa ufunguzi wa mashindano ya kugombea ubingfwa wa kombe la Ulaya 2008 nchini Uswisi.
Rais Gaddafi akataa makubaliano ya Mediterranian, Utavuruga na kuvunja nguvu za uhusiano wetu.
Tripol, Libya - Rais Libya, Muhamar Gaddafi, amekataa kuku baliana na mpango wa kuanzisha umoja wa ushirikiano katika nchi zilizopo kaskazini mwa Afrika amabo ungejulikana kama muungano wa Umoja wa Mediteranian.
Rais, Gaddafi alisema yakuwa nchi zilizo udhulia mkutano huu ni wanachama wa jumuia ua muungano wa Afrika na muungano wa Urabuni, na aliongega na kusema muungano wa mediteraniani utaleta madhara katika jumuia ya muungano wa Afrika(AU).
Akiongeza kwa kwa kusisitiza kupinga mswada huu, rais Gaddafi alisema yakuwa Nchi za Ulaya zinazidi imarika kwa kuwa pamoja na kama zinataka kushirikana na si , basi zitashirikiana na muungano wa jumuia hizi AU- African Union na AL- Arab League.
Mkutano huu ulihudhuliwa na nchi za Algeria, Mauritania, Morocco, Siria -Syria na Tunisia.
Picha hapo juu ni picha ya rais Gaddafi, alipo kuwa akiwasili kwenye moja ya mikutano hivi karibuni.
Chini anaonkekana rais, Gaddafi, akiongea katika mkutano hivi karibuni.
Hipo haja ya kuanza kuongea na Lebanoni' Waziri mkuu wa Israel".
Tel Aviv, Israel - Wazri mkuu wa Israel bwana, Ehud Olmert, ameshauri ya kuwa mazungumzo ya amani yanabidi yaanzishwe na Lebanoni, baada ya kurudia mazungumzo na serikali ya Siria(Syria).
Bwana, Olmert, alisema ikiwa tumeanza mazungumzo na Siria, kunauwezekano wa kuanza mazungumzo na Lebanoni, aliyaongea haya alipo kuwa akiongea viongozi wa serikali ya Israel.
Wakati huo huo mmoja wa wanajeshi wa jeshi la Israel korpo Gilad Shalit , aliyekamatwa mwaka 2006, ameandika barua kwa famiia yake na kuomba jitihada zifanyike ili aweze kuachiwa.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Israel,barua hiyo ilipitia kwenye ofisi ya mradi unao simamiwa na bwana Jimmy Carter, aliyekuwa rais wa zamani wa Amerika.
Hata hivyo baba ya Gilad, bwana Noam Shalit, alisema ya kuwa mwanae, hayuko katika mazingira bora na anhitaji kurudi nyumbani salama.
Na hii inaonyesha ya kuwa kopro Gilad Shalit bado ni mzima, na msemaji mmoja wa Hamas, alisema yakuwa hii ni kutokana na juhudi zilizo fanywa na rais wa zamani wa Amerika bwana Jimmy Carter.
Picha hapo anaonekana waziri mkuu wa Israel bwana, Ehud Olmert lipo kuwa akiongea hivi karibuni nchi Amerika katika mkutano wa ushirikiano kati ya Amerika na Israel.
Picha ya pili wanaonekana wanajeshi wa Israel , wakati wa mapambano na kundi la Hezbollah mapema mwaka 2006 mapambano amabayo yalichukua zaid ya siku wiki nne.
Picha ya chini ni picha ya mwanajeshi wa Israel, bwana Gilad Shalit, kabla ya kukamatwa kwake na kundi la wapiganaji kwenye maeneo ya Wapalestina.
Walio husika katika ukamatwaji wa raia wa Kijerumani watakiwa kujibu mashitaka.
Munich, Ujerumani - Kundi la kutetea haki za binadamu nchini Ujerumani, limeishitaki serikali ya Ujerumani kwa kushirikiana shirika la makachero la Amerika (CIA).
Kesi hiyo imefunguliwa kwa kuitaka serikali ya Ujerumani kuwaleta wafanyakazi 13 wa CIA, waliousika katika ukamatwaji husio kihalali wa raia wa Ujerumani bwana, Khaled Al Masri na Wolfgang Kalek hapo miaka ya nyuma.
Msemaji mmoja wa mahakama mjini Munich, alisema yakuwa kesi hiyo imefunguliwa , lakini hakusema ni lini itaanza kusikilizwa.
Bwana, Al Masri , aliachiwa huru mei 2004, na alikamatwa kimakosa.
Hata hivyo serikali ya Amerika imekataa kuzungumzia swala hilo, lakini viongozi wa serikali ya Ujerumani walikubali yakuwa kuna makosa yalifanyika.
Picha hapo juu ni nembo ya CIA.
Picha ya pili ni picha ya bwana Khaled Al Masri, ambaye alikamatwa wakati alipo kuwa mpakani mwa nchi za Serbia na Macedonia, na baadaye aliwekwa chini ya ulinzi kwa kipindi kileferu nchini Afghanistan.
Chini wanaonekana mmoja ya watu waliopo chnini ya ulinzi katika moja ya vizuizi ya watu wanaoshukiwa ni hatari kwa jamii ya kimataifa.
Kiongozi wa kidini wa kabila la rais wa zamani wa Irak, auwawa.
Tirkit, Iraq - Aliyekuwa kiongozi wa kidini wa kabila la aliyekuwa rais wa Irak Saddaam Hussein, Sheikh Ali Al Neda's amefariki dunia siku ya jumannne 9/06/2008, baada ya gari aliyoy kuwa akisafiria kulipuliwa na bomu.
Kiongozi huyo wa kabila la Al Bu Nasir lenye watu wengi jamii ya Sunni na ni moja ya kabila ambalo alilotokea rais wa zamani wa Irak, Saddam Hussein.
Sheikh Ali Al Neda's, alikuwa mwanzilishi wa kampeni ya ya kuwapinga wapiganaji wa Kisuni, ambao wanaopigana na jeshi la Amerika.
Pichani anaonekana mama akilia kwa uchungu baada ya kupoteza mmoja ya ndugu zake kutokana na machafuko na ukosefu wa uturivu nchini Irak.
Katikati ni bendera ya Irak.
Chini ni picha za watu ambao wamepoteza maisha yao, kutokana na hali yakutokuwa na amani nchini Irak.
Iran yawa na mtazamo tofauti na Iraq, "Mkataba na Amerika siyo muafaka" Wairan
Teheran, Iran - Kiongozi mkuu wa Kidini nchini Iran, Ayatollah Ali Khamenei,ameshauri ya kuwa serikali ya Iraki ya kuwa hapendelei mkataba ambao wa serikali ya Irak inafikilia kukubaliana na serikali ya Amerika(US).
Mkataba huo ambao hupo njiani kufikiwa, unahusu kwa jeshi la Amerika kukaa zaidi nchini Iraq, kwa kipindi cha miaka mingi baada ya ya mwaka 2008.
Kiongozi huu mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, alisema haya wakati alipo kutana na waziri mkuu wa Iraq bwana, Nuri Al Maliki ya kuwa wanamatumaini wananchi wa Irak, watakuwa na amani na maisha ya kawaida hapo baadaye , lakini siyo ndoto ya Kiamerika itakayo wawezesha kufikia amani hiyo.
Hata hivyo waziri mkuu wa Irak, bwana Nuri Al Maliki, alisema yakuwa, nchi yake kamwe haitatumika kama, kiwanja cha kuchambualia Irana na nchi majirani zake.
Hata hivyo.
Picha ya hapo juu wanaonekana, viongozi wa serikali ya Iran na serikali ya Iraki,wakati walipo kutana hivi karibuni.
Chini ni picha ya wana mama wakiwa mafunzoni tayari kujianda kulinda nchi yao Iraki.
Mkataba wa amani ya Somalia wawa mashakani, UN bado wanamatumaini.
Mogadishu , Somalia - Kiongozi wa kundi kubwa linali pingana ns serikali ya Somali, Sheikh Dahir Aweys , amekataa kuku bali mkataba wa makubaliano ya kuleta amani nchini Somalia.
Sheikh Dahir Aweys, alisema mkataba huo ni mkataba ambao utawapa nafasi upande wa serikali kujikusanyaia nguvu zaidi za kijeshi.
Akiongea kwa njia ya simu na moja ya mashirika ya habari, Sheikh Aweys, alisema ya kuwa tuna wapa moyo wapiganaji wote na tutajitahidi mpaka hapo tutakapo mshinda adui.
Jeshi la Somalia likisaidiana na jeshi la Ethiopia wanapigana na vita na makundi mbali mbali yaliopo nchini Somalia kwa kipndi kisicho pungua mwaka sasa.
Hata hivyo msemaji wa Umoja wa Mataifa,bwana Ould Abdallah, alisema yakuwa wamekubaliana kimsimgi kuhusu mktaba huo, na wakati huo huo. katubu mkuu wa umoja wa Mataifa, bwana Ban Ki Moon, ameyakaruibishwa makubalianao hayo, na kuagiza ya kuwa hata yele makundi binafsi yatakubaliana na mkataba huu.
Picha hapo juu anaonekana mpiganaji wa moja ya makundi yanayo pingana na jeshi la serikali,akiwa ameshikialia bunduki tayari kupambana na jeshi la serikali.
Picha ya kati wanaonekana, wapiganaji wa kundi la AlShabaab wakipokea mafunzo ya na mbinu zakupigana vita dhidi ya wanajeshi wa serikali.
Picha ya chini ni mmoja wa viongozi wa vyama/ makundi ambayo yamekataa kuukubali mkataba wa amani.

No comments: