Bingwa wa musiki wa soulo,atutoka" Wanamuziki wapigwa na mshituko".
Tennessee,Amerika - 13/08/08. Mwanamusiki bingwa wa musiki wa soulo, Isaak Heyis, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 65.
Mwanamusiki huyo alifariki dunia kutokana na ugonjwa wa kupooza, kwa mujibu wa mganga wake.
Mganga huyu, Mr Steve Shular,alisema Isaak Hayes, aliaanza kuugua mapema mwaka 2006.
Isaak Heyes, alishinda zawadi ya Oscar mwaka 1971 na mwaka 2002, alijumuishwa katika kundi la wanasanaa maarufu duniani lijulikanalo kama (US Rock and Roll Hall of Fame).
Mwanamusiki huyu ambaye alioa mara nne ameacha watoto 12.
Kufuatia kifo chake, wanamuziki wengi wamepigwa na mshituko mkubwa saana, hasa kwa mwanamusiki Gloria Gaynor na alisema ya kuwa jumuia nzima ya wanamuziki wa soul ilikuwa inamjua kwa umairi wake.
Mazishi ya marehemu Isaak Heyis yatafanyika Tennessee, misa ya kumwaga na kumwombea itafanyika katika kanisa la Hope Presbyterian kwenye kitongoji cha Cordova.
Picha hapo juu anaonekana marehemu Isaak Heyis, akiimba na kutumwiza wapenzi wake enzi ya uahai wake.
Picha ya pili anaonekana, marehemu Isaak Heyis, akiwa ameshikilia zawadi ya kujulikana kama mmoja ya wana sanaa maarufu duniani wakati wa enzi za uhai wake.
Mafua ya ndege yaibuka magharibi mwa Afrika"FAO ipo mbioni kukabili janga hili".
Lagos,Nigeria - 12/08/08. Wanasayansi nchini Nigeria, wamesema yakuwa wamegundua ya kuwa kumekuwepo na ugonjwa wa mafua ya ndege nchini humo.
Kwea mujibu wa wanasayansi, ugonjwa wa mafua ya ndege,umegunduliwa kuwepo katika majimbo ya Katsina na Kano.
Kwa kufuatia mfumuko huo wa ugonjwa wa mafua ya ndege,(FAO) Food and Agriculture Organisation, limesema ya kuwa,mpaka sasa ni vigumu kujua ni kwa kiasi gani ugonjwa huu umesambaa na umeibuka vipi katika Afrika, hata hivyo FAO imesema ipo mbioni kukabilina na janga hili.
Chini ni picha ya mkulima mmoja wakitembelea ndani ya shamba lake huku amefunika pua yake.
Picha ya chini,Mbuni ni ndege mkubwa kulikono wote , akiwa amekufa baada ya kukumbwa na ugonjwa wa mafua ya ndege.
Tawi la Al Qaeda kaskazini mwa Afrika la sema Mauritania ijiandae" Baada ya mapinduzi".
Nouakchott,Mauritania - 12/08/08. Kikundi ambacho ni tawi la kundi kubwa la Al-Qaeda, kilichopoo nchini Algeria, kimesema yakuwa mapinduzi yaliyo fanyika nchini Mauritania ni kinyume na yamesadidiwa na nchi za Ulaya Magharibi na Amerika.
Mauritania, nchi ambayo ilikuwa koloni la Kifaransa,imekuwa katika hali ya utata tangu ilipo pata uhuru.
Mauritani ni nchi yenye utajiri wa mafuta, dhahabu na chuma.
Mapinduzi hayo baridi, yalimtoa madarakani rais Sidi Mohamed Ould Cheikh Abdallah.
Picha hapo juu wanaonekan viongozi vinara wa kundi la Al-Qaeda, Osama Bin Laden kushoto na msaidizi wake, Imar Al Zawahiri walipo onekana kwa mara ya mwisho miaka ya nyuma, na kundi lao Al Qaeda limekuwa likisumbua vichwa vya jumuia ya kimataifa kwa muda mrefu.Picha ya chini ni ya bendera ya Mauritania,nchi ambayo wananchi wake wametakiwa kijiandaa na mapambano ya Al Qaeda baada ya mapinduzi yalioyo mngo'a rais Sidi Mohamed Ould Cheikh Abdallah.
Musharraf na wapinzani wavutana "Wapinzani wadai Musharraf ang'olewa".
Islamabad,Pakistan - 12/08/08. Viongozi wa cham cha upinzani nchini Pakistan, wamesema yakuwa inabidi rais, Pervez Musharraf, atolewe madarakani, kwa kushindwa kuwajibika ipasavyo.
Wakiyaongea hay mbele ya waandishi wa habari, alisema ya kuwa rais, Musharraf anatakiwa aonolewe madarakani kwa kukiuka sheria ya nchi na kushindwa kudhibiti mgogoro wa kisiasa ulipo nchini humo na ina bidi bunge ilfanye hivyo.
Hata hivyo, kwa upande waserikali, walikanusha , na kusema yakuwa haitawezekana kwa rais Pervez Musharraf, kutolewa madarakani n a nikitu ambacho hakitatoke.
Picha hapo juu, wanaonekana viongozi wa vyama vya upinzani Muslimu League N party bwana Nawazir Sharif kulia na kushoto ni, kiongozi wa Pakistani Peoples Party Asif Ali Zardari , wakiongea na wandishi wa habari kwa kutaka rais Musharraf atolewe ofisini.
Picha ya pili, anaonekana rais, Pervez Musharraf akisalimiana na baadhi ya watu wakati alipo tembelea katika moja maeneo yanafanyiwa ukarabati.
Picha ya chini, wanaonekana baadhi ya watu na wanachama wambao wanapendelea rais, Musharraf aendelee kuwa rais wa nchi yao.
Urusi yasimamisha vita dhidi ya Georgia"Tumetimiza matakwa yetu serikali yadai"
Moscow, Urusi - 12/08/08. Serilikali ya Urusi, ilitangaza rasmi ya kuwa itasimamisha mapigano ya kivita dhidi ya nchi ya Georgia.
Akiongea haya rais wa Urusi, Dmitri Medvedev, alisema yakuwa ameamuru majeshi kusimamisha mapigano, kwani Urusi, imeweza kutimiza matakwa yake, ya kuzikomboa yaye maeneo ambayo yalikuwa yamechkuliwa na wanajeshi wa Georgia.
Maeneo ambayo yalikuwa yanashikiliwa na wanajeshi wa Georgia, yanajulikana kama Ossetia na Abakhazia.
Na Wakati huo rais wa Urusi akitangaza haya, rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy alikuwa mbioni kujadili na viongozi wa pande zote ili kuleta amani katika eneo hilo.
Picha ya juu, anaonekana rais wa Urusi, Dmitri Medvedev,akiongea hivi karibuni kwenye katika moja ya mikutano iliyofanyika nchini humo.
Picha ya pili wanaonekana wanajeshi wakipigana wakati wa mapambano ambayo yamechukua muda wa siku tano.
Picha ya tatu inaonekana helkopta ya Urusi, ikitua katika moja maeneo ambayo vita vilikuwa vinaendea kabla ya kusimamishwa kwa vita dhidi ya nchi hizi mbili.
Chini anaonekana rais wa Georgia, Mikhael Saakhashvili,akijisugua kichwa, wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu hali halisi ya vita vya nchi yake dhidi ya Urusi.