Thursday, August 14, 2008

Nigeria yakabidhi rasmi eneo la Abakassi kwa Wakameroon"Ndoto yatimia"

Wajumbe wa upinzani na serikali wakubaliana kwa pamoja nchini Zimbabwe "Wataka haadi itimizwe".

Harare, Zimbabwe- 14/08/08. Mkutanao wa mazungumzo yakulea suruhisho la kisiasa nchi Zimbabwe yanaendelea kati ya rais Robert Mugabe na viongozi wa chama cha upinzani cha MDC, kinacho ongozwa na Morgan Tsvangirai zimnefikia katika hali ja juu zaidi.
Kwa mijibu ya wajumbe waliokuwepo kwenye mkutano huo,walisema yakuwa wajumbe wa kambi zote mbili walikubaliana na ule mkataba wa Lancaster, ambapo makubaliano yaliwekwa kati ya serikali ya Uingereza na Zimbabwe mwaka 1979, yakuwa serikali ya Uingereza itasaidiana serikali ya Zimbabwe katika swala la ardhi, yakuwa lazima utimizwe.
Kwa mujibu wa msemaji wa MDC,alisema haya yote ni kuakikisha yakuwa kila Mzimbabwe ana kuwa na imani na viongozi wao ya kuwa wanajali maslahi ya wananchi wa nchi.
Picha ya hapo juu ni ya moja ya shamba ambalo halijalimwa kitu tangu mgogoro wa kisiasa na ardhi ulipo anza nchni Zimbabwe.
Picha ya pili wanaonekan rais Robert Mugabe na kiongozi wa MDC-Democratic Movement Change, Morgan Tsvangirai wakiwa katika taswila tofauti kutetea hoja zao kwa wamnanchi wakati wa kampeni za uchaguzi uliofanyka mapema mwa mka huu wa 2008.
Picha ya tatu inaonyesha ni jinsi gani ardhi ya Zimbabwe, ilivyo na rutuba,hapo linaonekana moja ya zao lililopandwa shambani likiwa limestawi vizuri.
Picha ya mwisho,anaonekana , rais wa Afrika ya Kusini, Thabo Mbeki akikijibu maswali toka kwa waandishi wa habari, mara baada ya kutoka kwenye mkutano unao kutanisha viongozi wa Zimbabwe, ili kujadili njia za kufika muafaka kumaliza tatizo la kisisasa lililopo nchini humo.
Haya ni maendeleo ya jumuia ya Afrika Mashariki"Rais Paul Kagame".
Kigali, Rwanda-13/08/08. Rais wa Rwanda, Paul Kagame amekaribisha na kukubaliana na waziri mku wa Kenya , Raila Odinga yakuwa hipo haja kupunguza vituo vya kupimia uzito wa mizigo kutokea bandari ya Mombasa kutoka 13 hadi 2 itakapo fikia mwisho wa mwaka 2008.
Akiongea haya rais Kagame alisema hii ni moja ya mambo ya maendeleo ambayo yanahitajika yafanyike na viongozi wa Afrika ya Mashariki ili kuleta maendeleo katika eneo la Afrika ya mashariki.
Jumuia ya nchi za Afrika ya mashariki unazijumuisha nchi za Uganda Burundi Tanzania Rwanda na Kenya.
Picha ya hapo juu anaonekana rais Paul Kagame akiongea na wajumbe waliohudhulia katika walsha ya maendeleo na biashara katika eneo zima la Afrika Mashariki mjini Kigali.
Picha ya pili ni ya waziri mkuu wa Kenya, Raila Odinga, akiwa anasikiliza kwa makini katika mkuno ulio wakutanisha viongozi wa jumuia ya Afrika Mashariki.
Rais wa Tanzania azindua ujenzi wa kiwanda cha aina yake"Katani kutoa umeme"
Tanga, Tanzania-14/08/08. Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, imefungua rasmi ujenzi kiwanda kitakacho toa nguvu za umeme kwa kutumia mabaki ambayo yanatokana na zao la katani.
Ujenzi huo wakiwanda cha aina yake, umeghalamiwa na UNIDO-United National Industrial Develepment Organasation na kampuni ya kusindika zao la katani.
Kiwamnda hicho kikikamilika kitawezesha kutoa nguvu za nishati ya umeme kwa kiwanda hicho na mwingine utauzwa kwa shirika la umeme la taifa.
Na wakati huo hu serikali ay Norway imetoa jumla ya dola za Kimarekani million 56 kwa visiwa cha Zanzibar, kwa ajili ya kutandaza waya zitakazo peleka umeme viziwani humo.
Umeme huu utachukuliwa kutoka katika mji wa Tanga, haya ni kwa mujibu wa watalaamu na wasimamizi wa mpango huu.
Picha ya hapo juu anaonekana rais, Jakaya Kikwete akiongea hivi karibuni kuhusu maendeleo ya nchi yake, wakati alipo kutana na waandishi wa habari.
Picha ya pili nina onyesha shamba la mkonge,zao ambalo linatarajiwa kutumika katika uzalishaji wa umeme nchini Tanzania.
Nigeria yakabidhi rasmi eneo la Abakassi kwa Wakameroon."Ndoto yatimia"
Abakassi, Kameroon-14/08/08. Serikali ya Nigeria imekabidhi rasmi kwa serikali ya Kameroon eneo lijulikanalo kama Abakassi, lililopo kwenye eneo la ghuba ambayo inautajiri wa mafuta na gesi ya asili.
Kameroon ilipeleka kesi hii ya madai ya ardhi mwaka 1994 kwenywe mahakama ya kimataifa iliyopo mjini Hague
Kukabidhiwa kwa eneo hili, kumekuja baada ya mahakama ya ya kimataifa kutoa uamuzi ya kuwa eneo hili ni la nchi ya Kameroon mnamo mwaka 2002 kufuatia makubaliano ya Uingereza na Ujerumani ya mwaka 1913 nchi ambazo zilitalawa eneo hili.
Kufuatia uamuzi huu wa mahakama ya kimataifa, serikali ya Nigeria na serikali ya Kameroon, zilitiliana sahii mkataba uliojulikana kama (Green Tree ) mjini Newyork mwaka 2006, ambao ulikubalika ya kuwa Nigeria ilikabidhi eneo hili kwa Kamaroon.
Kukabidhiwa kwa eneo hili,kumepokelewa kwa hisia tofauti, na mwannchi mmoja alisikika akisema hatimaye ndoto imetimilika.
Picha ya hopo juu ni ya ramani ya eneo la Abakassi ambalo limekabidhiwa kwa serikali ya Kameroon.
Picha ya pili wanaonekana viongozi wa serikali wa pande zote mbili wakikumbatiana mara baada ya kumaliza kukabidhiana hati za makubaliano yakuwa eneo la Abakassi kuanzia sasa ni la wa Kamereoon.
Mwana wa Mfalme atoa onyo," wakulima wadogo wadogo hatarini".
London,Uingereza- 14/08/08.Mwana wa Mfalme wa na mfalme mtarajiwa wa Uingereza, Charles Philiip, amesema ya kuwa ulimaji wa kutumia mbegu zinazotokana na madawa, au kutengenezwa katika maaabara, zitaleta maafa makubwa katika jamii na mazingira kwa ujumla.
Akiongezea maafa ya ukulima wa aina hii,Mwana wa Mfalme, alisema yakuwa itadidimiza saana wakulima wadogo wadogo, hasa waliopo kwenye dunia ya tatu.
Picha hapo juu anaonekana mwana wa mfalme wa Uingereza na mfalme mtarajiwa Charles Philip, akisalimia wanachi hivi karibuni wakati wa ziara ya kikazi.
Syria na Lebanon za rudisha uhusuano wa karibu.
Damascus, Syria - 12/08/08. Serikali za Syria na Lebanon, zimekubaliana kimsingi kushirikiana na hasa katika matumizi ya mipaka ya nchi hizo mbili.
Makubaliano hayo yalifikiwa, baada ya rais wa Lebanon kutembelea kikazi nchini Syria.
Kufuatia dhiara hiyo marais wote wawili, rais wa Syria Bashar AL Assad na rais wa Lebanon Michel Sleiman, wamekubaliana kuendeleza uhusiano wa nchi hizo mbili.
Uhusiano wa nchi hizi mbili,uliingia doa tangu miaka 1975 wakati wa vita vya wenye kwa wenyewe vilipo anza.
Picha ya hapo juu ni ya bendera ya Lebanon nchi ambayo imekuwa katika hali ya mvutano wa kisiasa kwa muda mrefu.
Picha ya pili wanaonekana rais wa Lebanon, Michel Sleiman akikagua gwaride pamoja na mwenyeji wake rais Assad.
Picha ya chini ni ya bendera ya Syria, nchi ambayo imekuwa haina uhusiano mzuri na Lebanon, kwa muda wa kipindi kirefu, hadi hivi sasa wakati viongozi wa nchi hizi mbili walipo kubalina kurudisha uhusiano wao nchi hizi mbili.

No comments: