Thursday, August 7, 2008

Mtuhumiwa aponyoka mikononi mwa polisi."Msako waendelea"

Rwanda yataka viongozi wa Ufaransa wafikishwe mahakamani "Yataja majina 33 ya wahusika".

Kigali, Rwanda - 07/08/08. Serikali ya Rwanda, imetangaza ya kuwa serikali ya Ufaransa,ina husika moja kwa moja katika mauji ya alaiki ya watu wasiopungua laki 800,000 yaliyo tokea 1994.
Katika maelezo yake, serikali ya Rwanda imewataja maafisa 33 wa ngazi za juu wa jeshi na wanasiasa wa Ufaransa waliohusika katika mauaji hayo.
Katika majina hayo wamo rais wa zamani wa Ufaransa Francois Mitterrand na waziri mkuu wa zamani wa Ufaransa bwana Dominique de Villepin ambaye serikali ya Rwanda inadai afikishwe kwenye vyombo vya sheria ili kujibu mashitaka.
Hata hivyo serikali ya Ufaransa imekanusha madai hayo.
Picha ya hapo juu, ni ya bendera Rwanda, nchi ambayo ikikumbwa na mauaji yaliyo shangaza dunia nzima.
Picha ya pili ni ya mabaki ya watu walio poteza maisha yao, kutokana na vita vya kikabila kati ya Watutsi na Wahutu, ambapo serikali ya Rwanda inasema ya kuwa serikali ya Ufaransa ilihusika katika mauaji hayo.
Picha ya chini ni bendera ya Ufaransa,nchi ambayo imekuwa ikilaumiwa na Rwanda kwa kushindwa kuzuia mauaji ya alaiki ya mwaka 1994
Mamia waombeleza na kukumbuka milipuko iliyo poteza maisha," Afrika Mashariki".
Dar es Salaam, Tanzania - 07/08/08 .Mamia ya wanachi nchini Tanzania, wamakusanyika leo kuadhimisha miaka kumi ya kumbukumbu ya matukio ya kutisha, wakati mabomu yalipo lipuliwa katika ofisi za kibalozi za Amerika, zilizopo nchini Tanzania na Kenya.
Mabomu hayo ambayo ya lilipuliwa na kundi la kigaidi la Al Qaeda na kupoteza maisha ya watu wapatao 220 na wengine kupata vilema vya maisha.
Katika kuadhimisha siku hiyo,viongozi wa serikali na wakidini walikusanyika na kumba kwa pamoja na kusisitiza amani na utulivu duniani kote ndiyo njia bora kwa maisha ya mwanadamu.
Picha hapo juu, ni bendera ya Amerika, nchi ambayo imekuwa ikiongoza katika mstari wa mbele kupamabana na kundi la Al Qaeda na washirikimwake na kuaidai kulitokomeza kabisa.
Picha ya pili ni ya jengo la moja ya ofisi za balozi za Amerika zilizopo mjini Dar es Salaam, ambapo liliharibiwa vibaya na mabomu.
Picha ya tatu, lina onekana jengo la ofisi za kibalozi nchni Kenya, ambalo nalo lili polomoshwa kabisa kutokana na mlipuko wa bomu.
Jeshi la twaa madaraka, mgogoro wa kisiasa ndiyo chanzo,"Mapinduzi baridi".
Nouakchott, Mauritania - 07/08/08.Viongozi wa jeshi nchini Mauritania wameipindua serikali iliyo kuwa ikiongozwa na rais, Sidi Mohamed Ould Cheikh Abdallahi.
Mapinduzi hayo ambyo hayakumwaga damu yaliongozwa na viongozi wa jeshi kwa kudai yakuwa kwa kushindwa kuongoza nchi, kwa kufuatia mgogoro wa kisiasa, baada ya ya baadhi ya wabunge wapatao 48 kujitoa katika chama tawala na kupiga kura ya maoni ya kuto mwamini rais huyo baada ya kubadiri baraza la mawaziri.
Mapinduzi haya yaliyo fanyika nchni Maurutania, yamelaniwa vikali na nchini nyingi duniani, zikiongozwa na Umoja wa mataifa.
Picha hapo juu wanaonekana viongozi wa kijeshi wakiongozwa na Ould Abdel Aziz, akiongea na vyombo vya habari muda mchache baada ya mapinduzi ya kumtoa madarakani rais wa Mauritania, Sidi Mohamed Ould Cheikh Abdallahi.
Picha ya pili ni ya rais wa zamani wa Mauritania Sidi Mohamed Ould Chikh Abdillahi, ambaye ametolewa madaraka na jeshi la nchi yake.
Picha chini wanaonekana wanajeshi, wakiwa wanalinda mbele ya ofisi za shirika la utangazaji na radio za Mauritania.
Mtuhumiwa aponyoka mikononi mwa polisi,Msako waendelea"
Nairobi, Kenya - 4/08/08. Serikali ya Kenya inafanya msako mkubwa wa kumkamata mtuhumiwa aliyehusika katika milipuko ya mabomu yaliyo tokea katika balozo za Amerika nchini Tanzania na Kenya.
Mtuhumiwa huyo anaye jukilkana kwa jina la Fazul Abdullah Mohammed, amabye inasemekana aliponyoka katika nyayo zapolisi wakati walipo kuwa wakimfuatilia ili kumkamata.
Kwa mujibu wa masemaji wa polisi, Fazul Abdallah Mohammed, alikuwa akiishi sehemu za Malindi kabla ya kutoroka kabla ya vyombo vya dola kumtia nguvuni.
Picha hapo juu, ni ya bendera ya Kenya, nchi ambayo imekuwa katika halingumu ,kukabiliana na ugaidi.
Picha ya pili ni picha ya Fazul Abdallah Mohammed, amaye anasakwa na vyombo vya dola vya Kenya na jumuia ya kimataifa.
Picha ya tatu wanaonekana polisi wakikagua moja ya magari, katika jitihada za kumsaka Fazul Abdallah Mohammed.
Iran bado ya weka kitendawili kwa Amerika na jumuiya ya Ulaya.
Tehran, Iran - 4/08/08 . Serikali ya mjini teherani, imetangaza hivi karibuni ya kuwa imefanya majaribio ya siraha zake ambazo zinaweza kuzamisha meli na chombo chochote kinacho safiri katika maji au bahari, kwa karibu umbali wa miili 200.
Majaribio haya, yamekuja baada ya jumuiya ya Ulaya na Amerika, zinapanga upya kwa pamoja kuweka vikwazo zaidi dhidi ya serikali ya Tehrani.
Na ikiwa njia hii ya Harmuz itafungwa basi, huenda bei ya mafuta ikapanda kwa kiasi kikubwa, kwani 40% ya mafuta yanapita katika ukanda huo.
Hapo juu zinaonekana, baadhi ya siraha ambazo serikali ya Iran imekuwa ikizijaribu hivi karibuni.
Picha pili ya hapo juu, anaonekana rais wa Iran, Mahamoud Ahamadinejad akihutubia mbele ya bunge la Iran hivi karibuni.
Picha ya chini, ni sehemu moja ya mitambo ambayo vinu vya kuendeshea uzalishaji wa nguvu za kinyuklia vimekuwa vikitakiwa na serikali ya Amerika na Jumuiya ya Ulaya vifungwe, lakini nchi ya Iran, imakataa kabisa kufunga mitambo hiyo.

No comments: