Monday, August 18, 2008

Pervez Musharraf ang'atuka madarakani" Asema hii ni kwamanufaa ya taifa".

Pervez Musharraf anga'tuka madarakani''Asema hii ni kwamanufaa ya taifa".

Islamabad, Pakistan-18/08/08. Rais wa Pakistan, Pervez Musharraf, ametangaza kujiuzulu rasmi cheo chake cha Urais wa Pakistan.
Akihututubia kupitia runinga ya taifa rais Musharraf, alisema anaipenda nchi yake na watu wake , na katika kipindi chote cha uongozi wake,alijitahidi kwa hali na mali kulinda na kujenga heshima ya nchi yake.
Uamuzi huu wa kujiuzulu kwa rais Musharraf kumekuja, kufuatia kashfa zilizo kuwa zikimuandama, kutoka kwa wapinzani wenzake wa kisiasa,wakiongozwa na viongozi aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo miaka ya nyuma bwana Nawazir Sharif na Asif Al Zardari.
Picha hapo juu anaonekana wanachama na wapinzani wa rais Pervez Musharraf wakishangilia kwa furaha, hukum mmoja wao akipiga risasi juu, baada ya kusikia habar yakuwa rais Pervez Musharaf anajiuzulu cheo chake cha Urais.
Picha ya pili anaonekana rais Pervez Musharaf , akihutubia taifa kwa njia ya runinga ya kua anangatuka kutoka madarakani.
Picha ya mwisho anaonekana , Gen Pervez Musharraf, akiwa katika mavazi yake ya kijeshi, kabla ya kutangaza rasmi yakuwa anajiuzulu rasmi kuvaa magwanda, na tayari kuwa raia wa kawaida ili kuiongoza nchi yake.
Ukraini ya jiweka tayari kupokea msada wa kiulinzi"Ofisi ya mambo ya nje ya nchi yasema hayo"
Kiev, Ukraini-16/08/08. Serikali ya mjini Kiev,imesema yakuwa ipo tayari kuongea na nchi yoyote ya Ulaya kuhusiana na swala na ushirikiano wa maswala ya kijeshi na ulinzi wa nchi hiyo.
Haya yaliongelewa na ofisi ya waziri wa mambo ya nje ya wa Ukrain.
Kwa mujibu wa mmoja ya wachunguzi wa mambo ya ulinzi ya Ukrain,alisema uamuzi wa Ukrain umekuja baada ya kuona hali halisi iliyo tokea nchini Georgia.
Hata hivyo serikali ya Moscow ilipka kura kujitoa kushirikiana na Ukrain katika maswala ya kiulinzi baada ya Ukraini kuomba kuwa mwanachama wa NATO. Picha hapo juu ni bendera ya Urusi, nchi ambayo imekuwa na mvutano mkubwa na serikali za Umjoa wa Ulaya na Amerika mara baada ya kuishambulia kivita Georgia hivi karibuni.
Picha ya pili ni ya alma ya NATO, umoja ambao nchi nyingi ambazo zilikuwa chini ya jumuia ya Urusi (USSR) zinataka kujiunga na umoja huu.
Picha ya mwisho wanaonekana rais wa Urusi kulia akisalimia na rais wa Ukraine Victor Yushchenko walipo kutana pamema mwaka huu.

No comments: