Wednesday, August 27, 2008

Zambia yakumbwa na msiba mkubwa, rais Levy Mwanawasa hatupo naye tena"Ni pigo kwa taifa asema rais wa zamani Kenneth Kaunda"

Lebanoni yafungua mashitaka dhidi ya serikali ya Libya"Rais ashutumiwa"

Beiruti,Lebanoni-27/08/08.Serikali ya Lebanoni, imemfungulia mashitaka rais wa Libya,Muammar Gaddafi kwa kudai ya kuwa serikali ya Libya ilihusika katika upoteaji wa kiongozi wa dhehebu la Kishia, Sheikh Moussa Sadri.
Kupotea kwa Sheikh Moussa Sadri, kulitokea miaka 30 iliyo pita wakati kiongozi huyo alipo tembelea Libya mnamo mwaka 1978.
Hata hivyo serikali ya Libya imekua ikikataa kuhusika na kupotea kwa kiongozi huyo wa dhehebu la Kishia, na kusema alipanda ndege kuelekea mjini Rome.
Picha ya hapo juu ni ya rais Muammar Gaddafi,anaye shutumiwa na serikali ya Lebanoi ya kuwa serikali yake ilihusika katika kupotea kwa Sheik Sadri.
Chini ni picha ya Sheikh Sadri, aliyepotea miaka 30 iliyo potea akiwa safarini nje ya Lebanoni.
Wateka nyara wajisalimisha, baada ya majadiriano ya muda mrefu.
Kufra,Libya- 27/08/08.Watu walioteka nyara ndege ya shirika la ndege la Sudan, wamejisalimisha kwa serikali ya Libya, baada ya muda mrefu wa majadiriano.
Ndege hiyo aina ya boeng 737 ambayo ilikuwa imechukuwa abiria 95 kutoka mji moja wa Nyala Darfur.
Kwa mujibu wa mmoja ya wasemaji wa wateka nyara hawa, walidai wapelekwe Ufaransa.
Hata hivyo ndege hiyo haikuweza kufika ufaransa kutokana na huaba wa nafuta na kulazimika kutua Kufra baada ya kukataliwa kuingia nchini Misri.
Picha hapo juu ni ya moja ya ndege iliyo tekwanyara ikiwa imetua mjini Kufra kusini mwa nchi ya Libya.
Picha ya tatu inaonyesha ramani ya eneo ambolo ndege ya imetua ili kujza mafuta mjini Kufra.
Zambia yakumbwa na msiba mkubwa,rais, Levy Mwanawasa hatupo naye tena"Nipigo kwa taifa asema rais wa zamani Kenneth Kaunda"
Lusaka, Zambia- 20/08/08. Wananchi wa Zambia wapo katika msiba mkubwa uliyoikumba nchi hiyo, baada ya kifo cha rais wa nchi hiiyo Dr Levy Mwanawasa.
Rais Levy Mwanawasa, alifariki dunia mjini Paris, baada ya kuugua kwa muda mrefu kutokana na ogonjwa wa kupooza uliomkuta wakati akiwa katika mkutano wa viongozi wa Afrika uliofanyika nchini Misri mapema mwezi wezi wa sita (Juni)
Rais Levy Mwanawasa alichaguliwa kuwa rais wa Zambia mnamo mwaka 2002, kama rais wa tatu wa Zambia tangu kupata uhuru 1964.
Nae, rais wa zamani wa Zambia, Kenneth Kaunda, alisema ni pigo kwa taifa zima.
Picha hapo juu ni ya rais, Levy Mwanawasa wakati wa uhai wake akihutubia taifa katika moja ya sherehe za kitaifa nchini Zambia.
Picha ya pili wanaonekana ndugu, jamaa na mke wa rais Levy Mwanawas, bi Maureen, akiwa ameshikiliwa wakati wa mwili wa marehemu mume wake ulipo kuwa ukiagwa na wanchi wa Zambia.
Picha ya tatu wanaonekan maelfu ya wananchi wa Zambia wakielekea kutoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa raisi wao Dr Levy Mwanawasa.
Picha ya hapo juu wanaonekana askari wakiwa wamebeba jeneza ambapo mwili wa marehemu rais Levy Mwanawasa umo ndani tayari kwa wananchi wa Zambia kutoa heshima zao za mwisho.
Mola aiweke roho ya marehemu rais. Levy Mwanawasa mahali pema peponi. Amina.
Amerika na Libya zarudisha uhusiano, baada ya mvutano wa ajali ya Lockerbie.
Tripol,Libya-22/08/08. Kaya/Familia za watu waliopoteza maisha wakati wa ajali ya ndege iliyo tekwa nyara na watu wanaoshutumiwa kupata misaada ya mafunzo kutoka kwa serikali ya Libya, wameshutumu kurudiwa kwa uhusiano kati ya serikali ya Libya na serikali ya Amerika ni kinyume.
Haya yalisemwa na mmoja wa wasemaji ya watu walio potelewa na ndugu zao katika ajali hii, bwana, Bert Ammerman ambaye kaka yake alipoteza maisha yake,kwa kusema haelewi ni kwanini serikali yake inashirikaana nchi ambayo imehusika katika ajali hii ya Lockerbie.
Picha hapo juu ni ya bendera ya Amerika nchi ambayo ilikuwa adui mkubwa wa Libya miaaka ya nyuma.
Picha ya pili ni ya mabaki ya ndege ambayo ilipoteza maisha ya watu pale ilipo anguka mjini Lockerbie Scotland.
Picha ya mwisho ni ya bendera ya Libya nchi ambayo imerudisha uhusiano na Amerika hivi karibuni.
Meli zaidi zazidi tekwa nyara pwani ya Somalia.
Mogadishu,Somalia-22/08/08. Zaid ya meli zisizo pungua 4 zimetekwa katika ukanda wa pwani wa unao zunguka nchi ya Somalia.
Kwa mujibu wa shirika moja linalo shughulika maswala ya meli , lililopo mjini Kuala Lumpur(IMB) International Maritime Bureau's, limelipoti yakuwa , kumekuwa na ongewzeko la utekaji nyara wa meli hasa zinapo karibia maeneo ya pwani ya Somalia.
Moja ya meli zilizo tekwa ni kutoka nchi za Japan,Ujerumani, Iran na Malasyia.
Picha hapo juu ni moja ya meli ikiwa katikati ya maji huku imebeba mizigo, lakini meli hizo huwa zinakuwa katika hali ya hatari hasa zifikapo maeneo ya pwani ya Somalia.
Picha ya pili ni ya picha ya meli ya Malasyia ikiwa imetekwa nyara na waharamia katika pwani ya Somalia.
Wanachama wa Muktada Al Sadri waandamana kupinga kukaa kwa muda mrefu kwa wanajeshi ya Amerika na washirki wake.
Bagdad,Iraq -22/08/08.Maelfu ya watu wameandamana mjini Bagdad na kusini mwa mji wa Kufa, kupinga kuwepo kwa muda mrefu kwa jeshi la Amerika nchini humo.
Maandamano hayo yalikuwa yakiongozwa na viongozi, wanachama , wadau na Waumini wa dhehebu la Shia ambao kiongozi wa ni Muqktada Al Sadri.
Mmoja wa kiongozi alisema yakuwa hawataki nchi yao kuwa koloni la Amerika.
Maandamano hayo yalikuja baada ya waziri wa mambo ya nje wa Amerika bi Condoleeza Rice kuwasili nchini Iraq ili kujadili hali halisi ya maswala ya usalama na ushirikianao zaidi.
Picha hapo juu ni Muktada Al Sadri, ambaye amekuwa mstari wa mbele kupinga kuwepo kwa majeshi ya wageni wakiongozwa na Amerika.
Chini ni picha ya wanachama wapenzi na wadu wanao pinga kuwepo kwa jeshi la Amerika na washiriki wake.

No comments: