Wednesday, September 17, 2008

Biashara za hisa zapigwa na tetemeko la ukwasi.

Baba wa Kiafrika, aonyesha uwezo wake, "sitoi taraka kwa wake zangu"Hii ni baraka.

Jimbo la Niger , Nigeria- 2/09/09. Bwana mmoja kwa jina, Mohammed Bello, ametakiwa na mahakama ya kislaamu, awape taraka baadhi ya wake zake, ama atachukuliwa atua za kisheria.
Lakini kwa mujibu wa msemaji wa bwana Mohammed Bello,alisema yakuwa hawezi kuwapa taraka wake zake na anampango wakuoa wake wengine, kuoa kwake wanawake hawa ni mipango ya Mungu na anabarikiwa na Mungu kuweza kuwahudumia na kukidhi mahitaji ya famila yake yote, ni kifo ndicho kitakacho tutenganisha.
Picha hapo juu ni ya bwana Mohammed Bello, ambaye ana ameoa wanawake 86, na anadaiwa na mahakama awape taraka wanawake wengine.
Picha ya katikati ni ya nyumba ya bwana Mohammed Bello , ambapo wanaonekana baadhi ya wake na watoto wa bwana Mohammed Bello wakiwa wana endelea na shughuli zao.
Picha ya chini ni ya famili ya bwana, Mohammed Bello,wake zake pamoja na watoto.
Bwana Mohammeda mwenye umri wa miaka 84, ameoa wanawake 86 na watoto 170.
Ofisi za kibalozi za Amerika zashambuliwa na magaidi.
Sanaa, Yamen-17/09/08. Watu wapatao 16 wamepoteza maisha yao, baada ya ubalozi Amerika kushambuliwa kundi moja la kigaidi lijulikanalo Islamiki Jihad lililopo nchini Yamen. Mauaji hayo yalifanya kwa mtu mmoja aliyekuwa akiendesha gari kuelekea ofisi za ubalozi wa Amerika na kulipua gari ambapo ofisi zilishika moto.
Matukio hayo yamelaniwa vikali na serikali ya Amerika, na rais Bush amesema ya kuwa hii inaonyesha ya kuwa vita dhidi ya ugaidi bado kubwa na Amerika itashida vita hivi.
Juu ni picha ya moja ya majengo yakiwa yameshika moto na moshi ukiwa unaonekana mara baada ya kutokea mlipuko wa bomu.
Chini ni jengo la ofisi za ubalozi wa Amerika , ambazo zimeshambuliwa na magaidi.
Biashara za hisa zapigwa na tetemeko la ukwasi.
New York, Amerika- 16/09/08. Masoka ya hisa nchini Amerika yameikumbwa na wakati mgumu, mara baada ya kushindwa kuhimiri mzunguko wa hisa , kutokana kupata hasara ya kifedha na kushuka kwa kiasi cha alama 150.
Hii imekuja mara baaada ya kampuni mama, benki ya kuwekaza, Lehmana Brothers kushindwa kuendelea na shughulizake za kimasoko.
Hata hivyo msemaji mmoja wa serikali alisema yakuwa hali hii ni ya muda tu, na kuwa hali ya masoko na hisa yatarudi katika hali yake ya kawaida hapo baadaye.
Picha hapo juu ni ya jengo ambalo, shughuli za kibiashara za hisa huwa zinaendelea.
Chini ni picha ya mmoja ya wana hisa akiwa ameshikiria masikio, huku akiwaaamini macho yake nini kinaendelea, kwani mtandao wa biashara yake unaelekea kwenye mshare wa hasi, na ajui afanya nini.
Iraq kupata Amiri jeshi mpya" Amiri jeshi wa zamani amaliza muda wake".
Baghdad, Iraq-16/09/08- Aliyekuwa Amir jeshi mkuu wa jeshi la Amerika linalo simamia ulinzi na kupamabana na makundi yanayo pinga demokrasi nchini Iraq Generali, David Petraeus amemaliza muda wake hivi karibuni na kumkabidhi madaraka Generali Ray Odirno ambaye alikuwa makamu wake.
Katika kukabidhiana madaraka haya, kulishuhudiwa na waziri wa ulinzi wa Amerika bwana Robert Gates.
Gen, Petreaus, ndiye aliye fainikwa kuweza kupunguza mashambulizi nchini Iraq kwa mpango na mikakati yake ambayo iliwezesha wanajeshi kuwa karibu na wananchi na kusaidia kushinda na kugundua njama, dhidi ya makundi yanayo pinga serikali na kuwepo kwa majeshi ya Amerika na washiriki wake.
Picha hapo juu wanaonekana , Gen Ray Odierno kushoto akipokea bendera ikiwa ni ishara ya kukubali madaraka ya kuwa mkuu wa majeshi yaliyopo nchini Iraq, huku aaliyekuwa amiri jeshi mkuu wa zamani Gen, David Petreaus na kulia ni waziri wa ulinzi wa Amerika bwana Robert Gates.
Picha ya kati anaonekana, Gen, Ray Odierno akiwa na rais, Geogre Bush, wakati walipo onana hivi karibuni kwenye ikulu ya Amerika.
Chini wanaonekana maamiri jeshi, David Petreaus na Ray Odierno wakipeana mkono mara, baada ya kumaliza kukabidhiana madaraka.
Vita dhidi ugaidi bado, maelfu wakumbuka siku ya Sept 9/11.
New York,Amerika-11/09/08.Siku ya tarehe 11/09/, ya kila mwaka, wananchi wa Amerika huwa wanakumbuka watu waliopoteza maisha yao kutokana mashambulizi yanayo sadikiwa yalifanywa na kundi la Alqaeda.
Katika tukio hilo zaidi ya watu wapatao 2,900 walipoteza maisha yao na wengi kujeruhiwa vibaya.
Mashambulizi hayo yaliustua ulimwengu mzima, na katika hotuba yake rais wa Amerika, alisema ya kuwa vita dhidi ya magaidi bado, na inabidi wananchi kwa kushirikiana na serikali ili kushinda vita hivi.
Picha hapo juu ina onyesha majengo yakiwa yameshika moto mara baada ya kushambuliwa na magaidi.
Picha ya pili ni sehemu ya mabaki ya eneo ambapo majengo hayo yalikuwa yamejengwa yakiwa yametundikwa bendera ya taifa la Amerika wakati wamaombelezo hivi karibuni.
Picha ya tatu ni maua yakiwa yanaelea, baada ya waombelezaji kutoa heshima zao kwa watu waliopoteza maisha yao katika mashambulizi ya kigaidi.

No comments: