Saturday, September 6, 2008

Rais wa Bolivia atembelea Iran.

Afrika ya Kusini na Venezuela za endeleza huusiano"Watiliana mkataba wa kimaendeleo" Pretoria,Afrika ya Kusini-2/09/08.Serikali ya Afrika ya Kusini na serikali ya Venezuela, zimetiliana sahii mkataba wa kiushirikiano katika nyanja za kiuchumi na viwanda na hasa mafuta na gesi. Mkataba huu ulisainiwa wakati rais, Hugo Charvez, alipo tembelea nchini Afrika ya Kusini, Rais, Charvez, alitoa mwanya kwa wananchi wa Afrika ya Kusini kuweka vitega uchumi nchini Venezuela. Picha hapo juu, wanaonekana rais, Thabo Mbeki na Hugo Charvez ,wakielekea kwenye ofisi za Ikulu ya serikali ya Afrika ya Kusini mjini Pretoria, mara baada ya rais Charvez alipo wasili nchini Afrika ya Kusini.

Angola yaingia katika sura mpya ya kidemokrasi, waaanza uchaguzi leo.
Luanda, Angola,6/09/08-Wananchi wa Angola wanaanza kupiga kura leo.
Uchaguzi huu utakuwa ni wa kihistoria kwa kipindi kisicho pungua miaka 16 iliyo pita.
Kwa mujibu wa wasemaji wa na wasimamizi wa uchaguzi, wamesema ya kuwa kumekuwa na utata katika siku za mwanzo za uchaguzi.
Hata hivyo inasadikiwa chama tawala cha MPLA huenda kikashinda dhidi ya vyama vaya upinzani vikiongozwa na chama cha UNITA.
Picha ya kwanza kina mama wakishangilia katika kampeni za uchaguzi hivi karibuni.
Juu ni picha ya bendera ya Angola nchi ambayo wanachi wake wanapiga kura kumchagua rais wa nchi yao.
Rais wa Bolivia atambelea Iran.
Tehran,Iran- 2/09/08. Rais wa Bolivia Evo Morales, alifanya ziara ya kiserikali nchini Iran siku ya jumatatu.
Katika ziara hiyo rais Evo Morales,alikutana na rais wa wa Iran Mahamoud Ahamadinejadna kujadili mbinu za kudumisha uhusiano wao. Rais, Evo Morales, aliwasili nchini Iran akitokea nchini Libya.
Picha hapo juu ni ya marais wawilli walipo kutana hivi karibuni nchini Iran, kulia ni rais wa Iran Mahmoud Ahamadinejad na kushoto ni rais wa Bolivia Evo Morales.
China na Iraki zaingia mkataba wa karne tangu kuangushwa kwa serikali ya Saddam Hussein.
Baghdad, Iraki-30/08/08.Serikali ya Iraki imetiliana mkataba na serikali ya China tangu kuangushwa kwa serikali ya Saddam Hussein.
Mkataba huo wenye thamani ya $ 3 billion utawezesha makampuni kutoka China kuanza kuchimba mafuta na kutoa misaada ya kiufundi kwa ushirikiano na serikali ya Iraki.
Kwa mujibu wa wataalamu wa mafuta wanasema yakuwa Iraki, inauwezo wa kutoa mapipa ya mafuta 2.5 million.
Picha hapo juu ni ya sehemu moja ambapo mafuta yatachimbwa kwa ushirikiano wa serikali ya China na serikali ya Iraki
Kutokukubaliaana kimsingi''serikali ya ya Korea ya Kaskazini ya anza upya ujenzi wa mitambo ya Nuklia".
Yongbyon,Korea Kaskazini- 3/09/08. Serikali ya Korea ya Kaskazini, imeanza upya kujenga mitambo yake ya nuklia, baada ya kusimamisha kwa muda mpango wake.
Kuanza kwa ujenzi huu kumekuja baada ya serikali ya Kora ya Kaskazini kudai ya kuwa serikali ya Amerika imeshindwa kuifuta Korea ya Kaskazini ya kuwa ni moja ya nchi zinazo shirikiana na makundi ya kigaidi yanayo daiwa kutishia amani duniani.
Picha hapo juu ni ya moja ya majengo ambayo mitambo ya nuklia ilikuwamo, ilipo bomolewa kipindi cha siku za nyuma.

No comments: