Saturday, September 20, 2008

Rais, Thabo Mbeki, akubali kung'atuka madarakani"ANC yashinikiza"

Bi,Oprah Winfrey, akonga nyoyo za wanamama na wasichana nchini Saudi Arabia.

Dammam, Saudi Arabia-20/09/08. Maonyesho vipindi vinavyo tangazwa na bi Oprah Winfrey kwenye runinga za nchi Saudi Arabia yamezidi kupendwa na kusaidia upeo wa wanawake nchini humo.
Akiongea haya, mmoja ya wapenzi wa maonyesho ya vipindi ya Opra Winfrey, bi Nayla, alisema vipindi vya Oprah , huwa vinamfanya ajisikie kama anamwongelea yeye(Bi Nayla), na kusema, huwa vinamsaidia kuelewa baadhi ya mambo ambayo alikuwa haya elewi vizuri.
Maonyesho ya Oprah Winfrey,nchini Saudu Arabia, yalianza kuonyeshwa rasmi kwenye runinga nchini humo mwisho wa mwaka 2004 na yamekuwa yaklizidi kupendwa wasichana na wanawake , hasa wenye umri kati ya miaka 25 na kuemdela, kwa mijibi wa ripoti ya wachunguzi wa mambo ya utazamaji wa runinga nchini Saudi Arabia.
Picha hapo juu anaonekana bi Oprah Winfrey akiwa amekaa kwenya kochi, katika moja ya maonyesho yake, huku ameshikilia viatu.
Picha ya pili anaonekana, bi Oprah Winfrey kwenye mtandao, ambao umeandikwa maandishi ya kiarabu.
Chini ni picha ya bi Oprah Winfrey, akiwa amependeza kwa vazi lake la heshima, moja ya mavazi yanayo wavutia wanawake wengi nchini Saudi Arabia.
Rais wa Pakistan atoa onyo"Pakistan haitaruhusu uvamizi wa aina yoyote ndani ya nchi yake" Wakati huo hotel kulipuliwa na bomu.
Islamabad, Pakistan-20/09/08.Watu wapatao 60 wamepoteza maisha yao na wengine 200 kujeruhiwa baada ya bomu kulipuka kwenye maeneo ya hotel Marriot.
Mlipuko huo ulitokea wakati, roli moja lilipo ingia kwenya maeneo haya hotel,na kulipuka.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Pakistan, huu mlipuko ni ule wa kujitolea muhanga.
Hotel Marriot, huwa inapokea wageni wengi kutoka nje ya nchi ya Pakistan, na muda wote huwa na ulinzi mkali, alimalizia kwa kusema.
Mlipupo huu ni wapili , baada ya ule ulio tokea siku ya jumatano katika majengo ya shule za kidini.
Mlipuko huu , umekuja wakati rais,mpya wa Pakistan, Asif Ali Zardari, alipo maliza kuongea mbele ya bunge la Pakistan mapema mchana, na kuhaidi yakuwa nchi yake aitakubali kushambuliwa au kutumika na ugaidi wa aina yoyote, au kushambulia nchi yaye katika jina la gaidi.
Picha hapo juu ni moto mkubwa unaunguza majengo ya hotel Marriot, baada ya kulipuliwa kwa bomu.
Picha ya pili anaonekana rais wa Pakistan , Asif Ali Zardari, akiongea mbele ya bunge, kabla ya mlipuko mkubwa kwenye hotel ya Narriot.
Picha ya tatu wanaonekana baadhi ya watu wakisaidina kuondoa mmoja ya majeruhi wa mlipuko wa bomu lililo tokea kwenye maeneo ya hotel Marriot.
Picha ya chini, wanaonekana, wananchi wakijaribu kuangalia bila mafanikio nini la kufanya kuokoa baadhi ya vitu vyao ambayo vimearibika kutokana na mlipuko wa bomu.
Rais, Thabo Mbeki, akubali kung'atuka madarakani"ANC yashinikiza".
Pretoria, Afrika ya Kusini-20/09/08. Chama tawala nchini Afrika ya Kusini ANC,-African National Congress, kimetangaza rasmi yakuwa rais wa wa nchi hiyo, Thabo Mbeki, ang'atuke madarakani.
Akiongea haya katibu mkuu wa ANC, bwana Gwede Mantashe, alisema yakuwa ANC, imeamua ya kuwa rais Thabo Mbeki, inabidi ang'atuke madaraka.
Kwamujibu wa msemaji wa rais, Mbeki,aliseama yakuwa rais, Thabo Mbeki, amekubali kujing'atua madarakani.
Picha hapo juu anaonekana rais, Thabo Mbeki, akiwa anaongea katika moja ya mikutano na wawekeza vitega uchumi wakati alipo tembelea nchini Nigeria.
Picha ya pili, anaonekana rais Mbeki,alipo kuwa anasalimiana na wananchi wakati wa moja ya kampeni za uchaguzi nchini Afrika ya Kusini.
Picha ya mwisho, inaonesha rais, Thabo Mbeki akiwa maeshikilia kichwa na kuonyesha ya kuwa huwa anakuwa na wakati mgumu kutatua mambo ya kisiasa na kiuchumi, hasa yanapo kuwa yanaleta mvutano.
Mtandao wa kundi la Shia nchini Iraki wakumbwa na virusi.
Baghdad,Iraki-20/09/08. Mtandao unao milikiwa na mkuu wa ya waumini wa jumuia ya Shia, ume kumbwa na matatizo ya mawasiliano,baada yakuingiliwana virusi ambavyo vinazuia kuonekana kwa habari na maelezo ya kidini kwa wafuasi wa jumuia ya Shia.
Kwa mujibu wa kumdi la XP, limesema ya kuwa hayo yamekuwa ni ajili ya kulipiza, kwa yale waliotendewa waumini wa jumuia ya Suni.
Waasimu wakubwa wasiasa wakubalina kuiongoza nchi"Rais ni Mugabe na Tsvangirai ni waziri mkuu".
Harare,Zimbabwe-15/09/08. Rais Robert Mugabe na mpinzani wake bwna Morgan Tsavangirai, wametiliana sahii makubaliano ya kugawana madaraka ya kuongoza wananchi Wazimbabwe.
Makubaliano haya yamefikiwa baada ya muda mrefu wa mvutano wa kisiasa tangu kufanyika uchaguzi wa urais kati ya wafuasi chama cha ZANU-PF na MDC.
Mgogoro huo ulianza tatuliwa kwa majadiliano ya usuruhisi na rais wa Afrika ya Kusini, Thabo Mbeki, na hatimaye walifikia makubaliano, ambapo Rais Mugabe atabaki kuwa rais, Tsvangirai atakuwa ni waziri mkuu wa nchi.
Hapo juu ni picha ya bendera ya bendera ya Zimbabwe, nchi ambayo imekuwa ina mgogoro wa kisiasa tangu kufanyika uchaguzi, na kutatuliwa chini ya uongozi wa rais wa Afrika ya Kusini, bwana Thabo Mbeki.
Picha ya pili wanaonekana rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe,waziri mkuu mpya wa Morgani Tsvangirai na msuruhishi wa mgogora wanasiasi wa Zimbabwe, rais Thabo Mbeki.
Picha ya mwisho, wanaonekana viongozi wapya wa Zimbabwe rais Mogabe na Tsvangirai wakipeana mikono baada ya kukubali kuongoza nchi kwa pamoja.

No comments: