Wednesday, September 24, 2008

Israel yapata waziri mkuu mpya"Ni mwanamke wa kwanza kuwa waziri mkuu".

Nitarudi kuonyesha uwezo wangu muda si mrefu"Asema aliye kuwa nyota wa soka wa dunia mara tatu".

Rio De Janeiro, Brazil-22/09/08.Nyota wa soka wa dunia wa miaka ya ipatayo kama sita iliyo pita Ronaldo, amesema hivi karibuni ya kuwa hatakubali kukaa chini na kuacha kipaji chake cha kutikisa nyavu kina pote hivi hivi.
Aliyasema haya mara baada ya kuanza mazoezi tayari kurudi uwanjani, mara baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti,ambalo lilikuwa linamsumbua saana , na kushindwa kufanya vitu vyake awapo uwanjani.
Alisistiza yakuwa, hatasimamishwa na kitu chochote, kwani mpria ndiyo starehe yake,na wapenzi wa soka wasubiri pindipo atakapo rudi uwanjani, ndipo wata jaji wenyewe.
Picha hapo juu, anaonekana Ronaldo, akianza kufanya mazoezi ya kuchedzea mpira , mara baada ya kupata kupona upasuaji wa giti.
Picha ya pili anaonekan Ronaldo , enzi zake kabla ya kuwa mgonjwa wa giti, akishangilia goli huku akiwa amavalia jezi ya timu yake ya taifa ya Brazil.
Picha ya chini, wanaonekana wafalme walio weka historia ya kusakata soka wa karne ya sasaa 21, Ronaldo na Zidane, wakipeana mikono kabla ya mechi ya kuchangisha pesa kwa ajili ya kupiga vita umasikini duniani.
Israel yapata waziri mkuu mpya" Ni mwanamke wa kwanza kuwa waziri mkuu".
Jerusalem,Israel-22/09/08-Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Israel bi Tzipi Livni , amechaguliwa kuwa waziri mkuu, kuchukua nafasi ya aliyekuwa waziri mkuu Ehud Olmert.
Bi, Livni mwenye miaka 50, amekuwa mwanamke wa kwanza kuwa waziri mkuu wa Israel tangu mwaka 1974 na alishawai kuwa mfanyakazi katika ofisi za maswala ya usalama wa Israel (Mossad).
Kwa kufuatia kuchaguliwa kwakwe kuwa waziri mkuu, bi Livni, amepewa ruhusa na rais wa Israel, Shimon Peres, kuunda serikali kwa muda usiopungua siku 42.
Picha hapo juu ni ya bi Tzipi Livni,akiongea mara baada ya kuchaguliwa kuwa waziri mkuu wa Israel.
Chini, wanaonekana waziri mkuu mpya wa Israel bi, Tzipi Livni na rais Shimon Peres, wakiwa pamoja, wakati bi Livni ,alipo kwenda kumwona na kupewa ruhusa kuunda serikali mpya.
Uchungu kuondoka kwa rais,asema Zuma,"na rais mpya wa muda ateuliwa".
Pretoria,Afrika ya Kusini-23/09/08.Rais wa ANC,(African National Congress), Jacob Zuma, amesema ya kuwa kujiuzuru kwa rais, Thabo Mbeki ni kitendo ambacho kinacho tia uchungu, kwa chama na kwa wananchi wote na wanachama wa ANC.
Hata hivyo, alisema ya kuwa rais, Mbeki, ameshajiuzuru,basi inabidi tuendele mbele kuendeleza nchi.
Na wakati huo huo, bunge la Afrika ya Kusini, limemteua Kgalema Motlanthe, kuwa rais wa wa muda , mpaka hapo uchaguzi mpya wa nchi utakapo fanyika mwezi wa nne - 2009.
Motlanthe, ambaye amekuwa yupo kati ya bwana Zuma na rais Mbeki, kwa kuzingatia ni mmoja wa viongozi ambao walio tetea nchi wakati wa ubaguzi wa rangi nchi humo na kufungwa pamoja na rais wa kwanza wa Afrika ya Kusini , Nelson Mandela.
Picha hapo juu ni ya rais mpya wa Afrika ya Kusini,Kgalema Motlanthe, akoingea mara baada ya kuteuliwa kuwa rais wa mpito hadi hapo uchaguzi wa mapema 2009.
Picha ya pili wanaonekana rais,mstaafu wa Afrika ya Kusini, Thabo Mbeki, akiongea na Kgalema Motlanthe, wakati wa mkutano mkuu wa chama cha ANC.
Picha ya nchini ni ya rais wa chama cha ANC, Jacob Zuma, ambaye kesi zidi yake imepelekea kujiuzuru kwa rais Mbeki.
Iran, haina mpango wa kutengeneza bomu la nyuklia "Asema rais wa Iran".
New York Amerika-24/09/08.Rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad ameutubia tena umoja wa Mataifa, kwa kulaumu nchi zenye nguvu duniani kwa kutumia uwezo wake visivyo.
Aliongeza kwa kusema yakuwa nchi hizo zikiongozwa na Amerika, zimekuwa zinatumia nguvu zao kuonea nchi zisizo na nguvu.
Rais Ahmadinejad, alisema yakuwa sasa Amerika imekuwa ikijihusisha na mambo mengi ya dunia na ndiyo maana uwezo wake kiuchnumi unaporomoka na Amerika inaelekea mwisho wa njia yake.
Na kuhusu mpango wa Iran , kuendelea na kujenga mitambo ya kinyuklia, rais Ahmadinejad, alisema yakuwa nchi yake, ina jenga mitambo kwa matumizi ya kawaida na siyo mitambo ya kutengeneza mabomu,na huo ndio msimamo wa Iran na wananchi wa Iran.
Picha hapo juu, anaonekana rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad, akihutuubia mkutano mkuu wa umoja wa matifa katika kikao cha mwaka 2008, ndani ya jiji la New York.

No comments: