Friday, September 12, 2008

Putin aonya nchi za Ulaya Magharibi, kukubali Amerika kuweka mitambo yake ya kivita.

Moto wasababisha usafiri kuwa mgumu kwa wakazi wa Ulaya watumiao daraja.

Paris,Ufaransa-11/09/08.Daraja linalo unganisha Ufaransa na Uingereza ambalo linapita chini ya maji lime ungua na moto kutokana na moja ya magari yanayopita kwenye daraja hilo kulipuka na kusababisha moto.
Kampuni inayo shughulikia daraja hilo, (Eurotunnel's) lilisema yakuwa daraja hilo limeungua kiasi cha maili 7 za urefu na bado wanaendelea na uchunguzi.
Kufuatia moto huo,daraja limefungwa mpaka hapo litakapo fanyiwamatengenezo upya, alisema mmoja ya viongozi wanao simamia daraja hili.
Picha hapo juu wanaonekana wafanyakazi wanaoshughulikia kuzima moto wakiwa wanajadiliana jinsi gani ya kukabiliana na moto huo.
Chini ni msururu wa magari ambayo yamekwam, baada ya daraja kuungua na kuzuia usafiri katika eno hili.
Putin, aonya nchi za Ulaya Magharibi, kukubali Amerika kuweka mitambo yake ya kivita.
Moscow,Russia-11/09/08-Aliyekuwa rais wa Urusi na sasa ni waziri mkuu wa nchi, Vladimir Putin ,ameonya yakuwa nchi za jumuia ya Ulaya zishiruhusu mitambo ya kijeshi kutoka Amerika kuwekwa katika nchi zake.
Bwana, Putin aliyaongea haya, wakati alipo kutana na waandishi wahabari katika maeneo ya Bahari Nyeusi.
Alisistiza kwa kusema ya kuwa nchi za Ulaya magharibi na Amerika zimekuwa zikilaumu na kuchafua Urusi, kwa kudai ya kuwa Urusi ina fanya mambo yake kwa kufuata njia za zamani za enzi za vita baridi kati ya NATO na Rusia(USSR).
Nchi ambazo, alizizungumzia, ni Poland na Czech, nchi ambazo zimekuwa zinampango wa kuruhusu mitambo ya kijeshi kuwekwa katika nchi zake na Amerika.
Picha hapo juu ni bendera ya Jumuia ya Ulaya, ambapo nchi za jumuia wanachama zinadaiwa yakuwa zisiruhusu Amerika kuweka mitambo yake ya kijeshi.
Picha ya pili ni ya waziri mkuu wa Urusi, Vladimir Putin akionga mapema na wandishi wahabari, alipo kutana noa kuzungumzia hali halisi ya Urusi kuhusu siasa na uchumi kwenye jumuia ya kimataifa.

No comments: