Wednesday, September 10, 2008

Urusi ya aidi kutoa majeshi yake nchini Georgia" Yataka vikwazo zidi ya Georgia"

Waziri mkuu apoteza kibarua cha uongozi wa nchi "Chaota majani" , kazi ya zamani yawa chanzo".

Bengkok, Thailand-10/09/08.Aliyekuwa waziri mkuu wa Thailand, Samak Sundaravej, amefukuzwa kazi na hakama ya katiba.
Uamuzi huu umekuja baada ya kuonekana ya kuwa bwana, Samak Sundaravej, amekiuka miko ya kuwa kiongozi wa serikali na wakati huo huo ana fanya kazi na kampuni binafsi.
Kufukuzwa huko kwa bwana Sundaravej, kuendela kufanya maonyasho ya mapishi katika runinga.
Kabla ya kuwa waziri mkuu , bwana Sundaravej, alikuwa anajulikana saana hasa ka kipindi chake cha mapishi katika runinga za nchini Thailand.
Picha hapo juu anaonekana bwana, Samak Sundaravej, akisalimiana na wapenzi na wanachama wake mara baada ya kuchaguliwa kuwa zaziri mkuu wa Thailand.
Picha ya pili, anonekana bwana Samak Sundaravej, akinunu anyama tayari kwa maandalizi ya mapishi ambayo huonyeshwa kwenya runinga nchini Thailand.
Urusi ya aidi kutoa majeshi yake nchini Georgia," Yataka vikwazo zidi ya Georgia".
Moscow ,Urusi-09/09/08. Serikali ya Urusi imesema itataoa majeshi yake nchini Georgia, baada ya kukutana na viongozi wa jumuia ya Ulaya.
Ujumbe huu wa Jumuia ya Ulaya, uliongozwa na rais wa Ufaransa , Nicolas Sarkozy pamoja na Jose Manuel Baros, ulikutana na uongozi wa Urusi, ukiongozwa na rais wa Urusi, Dmitry Medvedev mjini Moscow.
Wakati huo huo Urusi imepeleka mswada kwenye kamati ya usalama ya umoja wa mataifa ya kuwa serikali ya Georgia iwekewe vikwazo vya kuuziwa siraha, lakini hata hivyo, serikali ya Amerika imepinga mswada huo na kudai ya kuwa ni mbinu za Urusi za kutaka kuamisha hoja ya kutaka kutoa majeshi nchini Georgia.
Picha hapo juu wanaonekan rais wa Urusi Dmitry Medvedev akisalimiana na rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy, wakati walipo kutana mjini Moscow kujadili hali ya Georgia.
Chini ni vinaonekan vifaru vya Urusi, vikiwa ninapiga doria kwa ajili ya usalama wa raia wake.
Kundi la Alqaeda la zishambuaria kwa maneno baadhi ya nchi"Ikiwemo Iran".
Tehran, Iran-08/09/08. Kiongozi msaidizi wa kundi la Alqaeda bwana Ayaman al Zawahiri, ameonekana kupitia mikanda ya video iliyopatikana kupitia vyombo habari na kuonya na kulaumu dhidi ya baadhi ya serikali ambazo zinashirikiana na Amerika kupambana na kundi lake.
Nchi ambazo zilitajwa ni pamoja na Iran na Lebanese Afganistani na Pakistani.
Katika video hii , Al Zawahiri, aliilaumu Iran kwa kushiriki katika kuhiruhusu Amerika kuishambulia Afganistan na Irak.
Picha hapo juu ni ya bendera ya Iran, nchi ambayo inadaiwa na kushirikiana na Amerika kwa njia moja au nyingine.
Picha ya pili ni ya Ayan al Zawahiri, akiongea kwenya video hivi karibuni.
Korea ya Kaskazini yadai ya kuwa kiongozi wao yupo mzima.
Pyongyang,Korea ya Kaskazini-10/09/08. Serikali ya Korae ya Kaskazini imetangaza yakuwa Kiongozi wa nchi yao bwana, Kim Jong II ya kuwa anaumwa ugonjwa wa kupooza, siyo ya kweli.
Kiongozi msaidizi wa nchi hiyo bwana, Yong Nam, alisema ya kuwa habari ya kuugua kwa kiongozi wao ni wa uzushi mtupu japokuwa hakueleza ni kwanini kiongozi huyo hakuudhulia sherehe hiyo..
Habari hizi zili kuja baada ya Kim Jong II, kushindwa kuudhulia maazimisho ya miaaka 60 ya kutengana kwa Korea moja, na kuwa Korea ya kusini na Korea ya Kaskazini.
Picha hapo juu ni ya kiongozi wa Korea ya Kaskazini bwana, Kim Jong II,ambaye inasadikiwa anamatatizo ya kiafya.
Chini ni picha ya baadhi ya viongozi wa Korea ya Kaskazini, wakiwa wanashangilia wakati gwaride la askari walinzi wa nchi walipo pita mbele yao siku ya 09/09/08 mjini Pyongyang.

1 comment:

Anonymous said...

Biblia inasema: "Kwa wakati uliowekwa [mfalme wa kaskazini = Urusi] atarudi," (Danieli 11:29a) Hii pia ina maana ya kutengana wa Umoja wa Ulaya na NATO.

Danieli 11:29b,30a = Mathayo 24:7 = Ufunuo 6:4 = ulimwengu wa tatu vita.
"Upanga mkubwa" = silaha ya nyuklia – upanga.

Danieli 11:31-35 = Mathayo 24:15,21,22 = Ufunuo 6:9-11 = dhiki kubwa (na dhiki kuu) kwa makanisa madogo. (Angalia pia Ufunuo 11:2; Luka 21:24b)
"Chukizo la uharibifu" = "yule mnyama" = serikali ya ulimwengu. (Danieli 11:31; Ufunuo 13:1,2,7)

Danieli 11:40-43 = Mathayo 24:29 = Ufunuo 6:12 = ulimwengu wa nne vita. (Angalia pia Luka 21:25; Isaya 5:26-30; Danieli 7:11; Ufunuo 13:3; Ezekieli 32:2-16; Habakuki 1:5-17; Sefania 1:14-18, Yoeli 2:1-11).

Ewiak Ryszard