Wairak wavutana kuongezewa muda kwa jeshi la Amerika.








Wairak wavutana kuongezewa muda kwa jeshi la Amerika.
Posted by
Kibatala
at
Wednesday, November 26, 2008
0
comments
Umoja wa mataifa wa pitisha azimio la kupeleka majeshi ya kulinda amani Kongo.
Goma, Kongo-20/11/08. Umoja wa mataifa umekubaliana kwa kwapoja kupeleka majeshi ya jumuia hiyo wa wanajeshi wapatao 3100.
Uamuzi huo wa kutuma majeshi ya umoja wa matifa umekuja sambamba na uamuzi wa jeshi la upinzani linalo pinga na serikali ya Kongo na linaongozwa na Laurant Nkunda, kusimamisha mapigano.
Akiongea hayo, balozi wa Uingereza kwenye umoja wa mataifa, John Sawers, alisema nchi 15 zimekubaliana kwa pamoja kutoa mchango wake.
Picha hapo juu wanaonekana wananchi wakiwa wamezingirwa na moshi katika moja ya kambi ya kikimbizi , mmoja ya watu walio kimbia vita alisema "hii yote imeletwa na vita vilivyo tokea hapa nchini kwetu (Kongo ) na kuleta maafa makubwa kwa jamii yetu.
Syria na Uingereza zafanya mazungumzo ya kiserikali.
Damascus,Syria-19/11/08. Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Miliband,amefanya ziara ya kiserikali nchini Syria na kuongea na rais Bashar al Assad.
Ziara hii ni ya kwanza ya kiongozi wa serikali ya Uingereza tangu mwaka 2000.
Kukutana kwa viongozi hawa huenda kukarudisha uhusiano wa serikali hizi ambao umekuwa na mvutano kwa kipindi kilefu.
Picha hapo juu wanaonekana, rais wa Syria, Bashar al Assad, akiongea na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Miliband, walipo kutana hivi karibuni mjini Damascus.
Jaji atoa amri washitakiwe waachiwe huru"Hakuna ushaidi ".
Guantanamo Bay, Kuba-20/11/08.Jaji Richard Leon,ameagiza ya kuwa washitakiwa watano wanao tokea Algeria na wanaoshikiliwa katika jela ya Guantanamo Bay waachiliwe kwani kukamatwa kwao ni kinyume cha sheria.
Jaji, Richard Leon, alisema ya kuwa hakuna ushahidi kalimi wa kuwahusisha watu hao watano, yakuwa walikuwa na mpango wa kwenda Afghanistani ili kupigana na jeshi la Amerika na washiriki wake.
Watu hao watano walikamatwa Bosnia Hercegovina mwaka 2001, tangu mwaka huo wamekuwa chini ya ulinzi katika jela ya Gwantanamo Bay.
Posted by
Kibatala
at
Thursday, November 20, 2008
0
comments
Matumaini ya kumpata, Baraka Obama mwingine bara la Ulaya yapo"Asema mbunge".
Posted by
Kibatala
at
Thursday, November 20, 2008
0
comments
Mama Afrika, MIRIAM MAKEBA, atutoka, atuko naye tena"MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI, AMINA".
Posted by
Kibatala
at
Monday, November 10, 2008
0
comments
Bara la Afrika lajianda na mapokezi ya Papa Benedict XVI mwaka 2009.
Vatican City, Vatican,09/11/08. Papa Benedict XVI, anatarajiwa kufanya ziara katika bara la Afrika mapema mwakani.
Kwa mujibu wa msemaji wa Vatican, Papa Benedict XVI,atafanya ziara hii ikiwa moja ya maandalizi ya mkutano na maaskofu kutoka bara la Afrika, utakao fanyika mwezi wa Oktoba 2009.
Kwa mijibu wa msemaji huyo, alisema yakuwa Papa, atafanya ziara katika nchi za Angola na Kamerooni. Kamerooni itaandaa mkutano utakao wajumuisha viongozi Afrika wa kanisa Katoliki. Picha hapo juu ni ya Papa Benedict XVI,ambaye anatarajiwa kufanya ziara katika bara la Afrika mapema mwaka wa 2009.
Posted by
Kibatala
at
Sunday, November 09, 2008
0
comments
Demokrasi yaleta historia nchini Amerika, Baraka Obama, mwafrika wa kwanza kuwa rais wa Amerika.
Posted by
Kibatala
at
Thursday, November 06, 2008
0
comments