Monday, November 10, 2008

Mama Afrika,MIRIAM MAKEBA,atutoka, atuko naye tena"MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI, AMINA

Mama Afrika, MIRIAM MAKEBA, atutoka, atuko naye tena"MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI, AMINA".

Naples,Itali-10/11/08. Mama Afrika,Miriam Makeba amefariki dunia, baada ya kupata mstuko wa ugonjwa wa moyo wakati akiwa na tumbwiza jukwaani.
Mama Afrika, Miriam Makeba,alianguka jukwaani na baadaye kukimbizwa hospitali, lakini jitihada za waganga hazikufaniukiwa kurudisha uzima wa Mama Afrika.
Mama Afrika, Miriam Makeba alizaliwa mwezi wa, Marchi 4/1932, mjini Johannesburg ni Shantytown.
Mama Afrika, Miriam Makeba, aliishi ukibizini kwa muda wa miaka 31, kupinga utawala wa kibaguzi wa wazungu wachache.
Kwa kutumia nyimbo zake mama, Miriam Makeba, alitumia nyimbo zake kwa kueleza matatizo yanayo wakabili Waafika wenzake, hasa wananchini Afrika ya Kusini, kulisababisha kuzuiliwa kwake kurudi nchini Afrika ya Kusini kuuzuria mazisha ya marehemu mama yake.
Mama Afrika Miriam Makeba,alirudi nchini Afrika ya Kusini mwaka 1990, baada ya kuachiliwa kwa rais wa kwanza wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandele Madiba.
Picha ya kwanza hapo juu, anaonekana mama Afrika Miriam Makeba, akitumbwiza enzi ya uai wake huku akiwa amevalia vazi murua la kiafrika.
Picha ya pili anaonekana, Mama Afrika, Miriam Makeba, akionyesha umairi wake, wa mwanamke wa Kiafrika anavyo fanya vitu vyake, hasa anapo cheza muziki ama ngoma za kiasili.
Picha ya tatu wanaonekana, mama Afrika, Miriam Makeba na Huge Masekela wakifanya vitu vyao mbele ya wapenzi wamuziki walio kuja kukongwa roho zao.
Picha ya nne,anaonekana mama Afrika, Miriam Makeba, akifanya vitu vyake enzi za ujana wake.
Picha ya mwisho anaonekana mama Afrika, Miriam Makeba akisikiliza kwa makini na huku akitafakali na alikuwa akitoa majibu yenye mafundisho na kumbukumbu kwa vizazi vipya.
MOLA - MUNGU AILAZE ROHO YAKE KWA AMANI PEPONI AMINA.
Rais mteule, Baraka Obama wa Amerika, atembelea Ikulu"Michelle Obama, akagua na kuangalia nyumba yake tayari kwa maisha mapya".
Washington DC ,Amerika - 10/11/08. Rais mteule wa Amerika, Baraka Obama na mkewe, Michelle Obama, wametembela Ikulu kikazi kuangalia na kuongea na rais wa sasa wa Amerika George Bush, kuhusu maswala ya kiuchumi ya nchi na maswala ya kimataifa.
Wakati rais, Baraka Obama anaongea na rais, George Bush, Bi Laura Bush atakuwa anamwonye bi, Michelle Obama mazingira ya ndani na nje Ikulu.
Picha hapo juu wanaonekana rais wa sasa George Bush, akiwa na rais mteule Baraka Obama, wakitembelea kwa pamoja mazingira ya Ikulu, kabla ya kuanza mazungumzo.
Picha ya pili, wanaonekana marais, George Bush na mke wake Laura kwa pamoja na rais mtarajiwa Baraka Obama na mke wake Michelle Obama, wakipiga picha kwa pamoja, kabla ya kuanza kazungumzo.
Picha yatatu wanaonekana, rais mteule, Baraka Obama na mke wake Michelle Obama, wakisalimiana rais, George Bush na mkewe Laura Bush,baada ya kuwasili Ikulu.
Picha ya nne, wanaonekana rais mtarajiwa wa Amerika, Baraka Obama na mkewe wakishuka kwenye gari, tayari kuanza mazungumzo na rais wa sasa, George Bush na mke wake Laura Bush.
Picha ya mwisho, wanaonekana rais mtarajiwa, Baraka Obama na mke wake Michelle Obama, wakiangalia kwa makini matokeo ya uchaguzi, ambayo Baraka Obama, alichaguliwa kuwa rais wa kwanza mwafrika kushinda uchaguzi na kuwa rais wa Amerika.
Afisa wa ngazi za juu wa serikali ya Rwanda, akamtwa nchini Ujerumani ( Rwanda na Ufaransa moshi wafuka .......)
Frankfurt,Ujerumani-10/11/08. Serikali ya Rwanda imelaani vikali kitendo cha kukamatwa kwa afisa wa ngazi za juu wa serikali bi Rose Kabuye, alipo kuwa kikazi ziarani nchini Ujerumani.
Bi, Rose Kabuye alikamatwa alipo wasili kwenya kiwanja cha ndege Frankfurt siku ya jumapili 09/11/08.
Kukamatwa kwake kumekuja, baada ya serikali ya Ufaransa, kufungua kesi mwaka 2006, zidi yake ambayo ina mshutumu kuhusika na mauaji ya rais wa zamani wa Rwanda.
Rais ,Juvenal Habyalimana alifariki dunia baadaya ndege aliyo kuwa akisafiria kuangushwa.
Picha hapo juu anaonekana bi, Rose Kabuye kulia, akiwa na rais wa Rwanda Paul Kagame hivu karibuni.
Wapiganaji wanao pigana na serikali ya Somali wateka nyara masista.
Nairobi,Kenya- 10/11/08. Wafanyakazi wa shirika la msalaba mwekundu kutoka Kenya na mastista wa wa kanisa Katholik wametekwa nyara na wapiganaji wanao pigana na serikali ya Somalia.
Kwa mujibu wa msemaji wa shirika la msalaba mwekundu, alisema yakuwa masista na wafanyakazi wa shirika lao walitekwa nyara wakiwa kwenye nyumba zao.
Tukio hilo lilitokea wakati wapiganaji hao, walipiga risasi na na kutupa mabomu ya mkono katika kituo cha polisi kabla ya kufanya utekaji nyara huo.
Masista hao Caterina Giraodo mwenye umri wa miaka 67 na Maria Teresa Olivero mwenye umri wa miaka 60.
Picha hapo juu linaonekana gari lililo beba wafanyakazi wa shirika la msalaba mwekundu na masista likiongozwa na kundi moja la wapiganaji wanao pigana na serikali.
Watuhumiwa wa mauaji ya Bali wa hukumu yao yakamilishwa.
Jakarta, Indonesia-09/11/08. Washitakiwa watatu ambao walihukumiwa kwa kunyongwa baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika katika kulipua majumba mawili ya starehe(Disco), mwaka 2002, kwa mabomu na kusababisha mauaji ya watu wasio pungua 202 mjini Jakarta.
Watuhumiwa hao, Imam Samudra, Amrozi bin Nurhasyim na Mukhlas,au kwa jina jingine Ali Ghufron, waliuwawa kwa kupigwa risasi kwenye saa 12:15 asubuhi katika gereza la Nusu Kampangan,alisema msemaji wa serikali Indonesia Jasman Panjaitan.
Kuthibitishwa kwa vifo vyao, kuliidhinishwa na serikali kwa kutumia vipimo vya kitaalaamu.
Picha hapo juu wanaonekana baazi ya wananchi wakiwa wamebeba mwili wa mmoja ya watuhumiwa walio uwawa kwa kupigwa risasi baada kukutwa na hatia ya mauaji.
Picha ya pili wanaonekana wananchi wakiwa wameshika picha za za mmoja ya watuhumiwa wakati walipo andamana kuelekea kuwafanyia mazishi.
Picha ya tatu, anaonekana mmoja ya mtuhumiwa akipelekwa kupewa hukumu zidi yake na baazi ya maofisa wa serikali.
Picha ya mwisho ni za watuhumiwa ambao walihukumiwa, kuuwawa kwa kupigwa risasi.

No comments: