Thursday, November 20, 2008

Syria na Uingereza zafanya mazungumzo ya kiserikali.

Umoja wa mataifa wa pitisha azimio la kupeleka majeshi ya kulinda amani Kongo. Goma, Kongo-20/11/08. Umoja wa mataifa umekubaliana kwa kwapoja kupeleka majeshi ya jumuia hiyo wa wanajeshi wapatao 3100. Uamuzi huo wa kutuma majeshi ya umoja wa matifa umekuja sambamba na uamuzi wa jeshi la upinzani linalo pinga na serikali ya Kongo na linaongozwa na Laurant Nkunda, kusimamisha mapigano. Akiongea hayo, balozi wa Uingereza kwenye umoja wa mataifa, John Sawers, alisema nchi 15 zimekubaliana kwa pamoja kutoa mchango wake. Picha hapo juu wanaonekana wananchi wakiwa wamezingirwa na moshi katika moja ya kambi ya kikimbizi , mmoja ya watu walio kimbia vita alisema "hii yote imeletwa na vita vilivyo tokea hapa nchini kwetu (Kongo ) na kuleta maafa makubwa kwa jamii yetu. Syria na Uingereza zafanya mazungumzo ya kiserikali. Damascus,Syria-19/11/08. Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Miliband,amefanya ziara ya kiserikali nchini Syria na kuongea na rais Bashar al Assad. Ziara hii ni ya kwanza ya kiongozi wa serikali ya Uingereza tangu mwaka 2000. Kukutana kwa viongozi hawa huenda kukarudisha uhusiano wa serikali hizi ambao umekuwa na mvutano kwa kipindi kilefu. Picha hapo juu wanaonekana, rais wa Syria, Bashar al Assad, akiongea na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Miliband, walipo kutana hivi karibuni mjini Damascus. Jaji atoa amri washitakiwe waachiwe huru"Hakuna ushaidi ". Guantanamo Bay, Kuba-20/11/08.Jaji Richard Leon,ameagiza ya kuwa washitakiwa watano wanao tokea Algeria na wanaoshikiliwa katika jela ya Guantanamo Bay waachiliwe kwani kukamatwa kwao ni kinyume cha sheria. Jaji, Richard Leon, alisema ya kuwa hakuna ushahidi kalimi wa kuwahusisha watu hao watano, yakuwa walikuwa na mpango wa kwenda Afghanistani ili kupigana na jeshi la Amerika na washiriki wake. Watu hao watano walikamatwa Bosnia Hercegovina mwaka 2001, tangu mwaka huo wamekuwa chini ya ulinzi katika jela ya Gwantanamo Bay.

No comments: